Anaewaza hakuna mapenzi ya kweli,ndie tapeli wa mapenzi

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,406
Amani kwa wote,

Hebu jaribu kaa chini na kujiuliza, je ni kweli maana ya mapenzi inatambulika na wengi au wengi wanatambua maana ya ngono (ashakum si matusi) na hawaijui maana ya kwanza?Utasikia wengi wakidai kuwa siku hizi mapenzi ya kweli hakuna,hapo panaukweli japo kwa mbali kwa kuwa mfumo wa maisha na tabia za watu zishakuwa kama za wanyama hivyo hawajali kabisa kuhusu maana ya kupendana.Pita mtaani utona kijana wa kike analama kuwa siku hizi hakuna mapenzi ya kweli,hivi uliwahi jiuliza kama hakuna je yeye anayo ama la?

Msingi wa kwanza,kama yeye hana basi ni sehemu ya tatizo.

Msingi wa pili, kama anajua hayapo na akaendelea kubahatisha na kuuza upendo wake hali akijua hapendwi,basi nae ni sehemu ya tatizo.

Msingi wa tatu,ukiona kijana mwenye akili anakubali kuwa mapenzi ya kweli hayapo bila ya kuyatatua tatizo,basi nao ni sehemu ya tatizo.

Siku zote "HAKUNA HISIA YA KWELI ITOKAYO NDANI YA MOYO WA MTU NA IKAWA YA UONGO LABDA HISIA HIYO IWE NI UTAPELI"
tubadili mapenzi yetu,TUISHI KIUHALISIA NI SIYO KIHISIA.

Mapenzi yapo japo wengi tunasalitiwa.
 
Hayajakufika! Yakikufika utakiri kwa kinywa chako kuwa hakuna mapenzi ya kweli
 
Back
Top Bottom