Anadolu Agency yatoa Ofisi zake za Gaza kwa Al Jazeera na AP

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Shirika la Habari linalomilikiwa na Serikali ya Uturuki, Anadolu Agency (AA) limetoa kibali cha kutumiwa kwa ofisi zake katika mji wa Gaza kwa Mashirika ya Habari ya Al Jazeera na Associated Press (AP) baada ya ofisi zao kuharibiwa na shambulio la kombora la Israel siku ya Jumamosi.

1621186477685.png


Mkurugenzi Mkuu wa AA, Serdar Karagöz amewaandikia barua Wakurugenzi wa Al Jazeera na AP akionesha kusikitishwa kwake na mashambulio ya Israel yanayolenga vyombo vya habari akisema kuwa kumekuwa na jitihada za makusudi za Jeshi la Israel kuwalenga waandishi wa habari ili kuzuia kinachoendelea Gaza kisijulikane duniani.

Karagöz amesema tangu mashambulizi yalipoanza siku ya Jumatatu, wafanyakazi 6 wa Shirika lake wamejeruhiwa na Jeshi la Israel, akiitaka dunia kusimama kupinga jaribio la kukaba uhuru wa habari linalofanywa na Israel.

“Waandishi wa Habari wanaandika taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita unaofanyika katika eneo hilo,” ameandika Karagöz, akitoa wito pia kwa vyombo vya habari duniani kushikamana kuhakikisha usimamizi wa “uandishi wa habari usioegemea upande wowote, na kuthamini misingi ya uhuru wa habari ambao unatatizwa na Mamlaka za Israel.”

Mashambulizi ya makombora ya Israel yameendelea siku ya Jumapili katika eneo la Gaza na kusababisha vifo vya watu 42, idadi kubwa zaidi ya vifo kushuhudiwa ndani ya siku moja tangu mashambulizi yalipoanza siku ya Jumatatu, na kupelekea jumla ya idadi ya vifo kufikia watu 188 wakiwamo watoto 55. Israeli imeripoti vifo vya watu 10 wakiwamo watoto wawili.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjjamin Netanyahu amesema mashambulio ya Israel hayatakoma licha ya jitihada za Jamii ya Kimataifa kutaka mzozo huo usitishwe.

Chanzo: Daily Sabah
 
Waamue wakubali au Wakatae waendelee kufa
Kama waisrael wenyewe walipitia mateso makali katika nchi nyingi walizoishi kwa miaka 2000 na hawakugive up, Sioni namna Wapalestina watakavyogive up hata kama ni. kwa miaka 5000 ijayo.
Israel hana namna, ajiandae kwa long battle
 
Tuweni realistic; mtu kakuchokoza halafu chombo kimoja cha habari kipo bias unadhani wewe ndio ungekua rais wa Bongo ungefanyaje? Kama unao uwezo, sioni kama ungefanya tofauti na anacho kifanya Benyamin Netanyahu; Juzi Uingereza wananchi wake wameandamana kuhusu Corona, chombo gani chao kimeitanza ile demo? Hakuna, ndio ukweli so kuzuia baadhi ya habari zisitoke ndani ya nchi yako is almost nchi zote zinafanya the same; huwezi ilaumu Israel kwa hatua yao hi, by the way, jamaa walitoa taarifa ya wao kuondoka kwenye hilo jengo and this is why casualities wamekua wachache kwa jengo kubwa kama lile
 
Waandishi wa habari walioegemea upande mmoja na kuleta habari za uongo na wao wanakuwa vitani kwa wanayemchochea kwa watu... Ukitizama video za Gaza yaani ni Maigizo matupu vitoto vimebebwa ati vimepigwa mabomu n.k afu manjemba yanapiga kelele balaa hiyo michezo ilikuwepo miaka ile not now... Umetaka vita pigana kama Dume na sio kulia lia
 
Back
Top Bottom