Anadhani kwamba kwa hizi sababu basi CCM itaweza kuondoka wewe unasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anadhani kwamba kwa hizi sababu basi CCM itaweza kuondoka wewe unasemaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Nov 1, 2007.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  KATIKA historia ya mahusiano ya watawala na
  watawaliwa na hasa pale ambako yanawahusisha watu
  wenye historia moja na ambao wanatoka damu moja na
  hatma yao ni moja au watu ambao historia ya maisha yao
  imefungamana tangu enzi za enzi; endapo mahusiano hayo
  baina ya pande hizo mbili hayana budi kukomeshwa na
  kuvunjwa, basi sababu za kuvunja na kuyakomesha kwa
  njia ya kidemokrasia au ya kimapinduzi ni lazima
  zisemwe wazi, kwa ukweli na bayana.

  Kwa vile kuvunja uhusiano huo ni jambo ambalo
  litawaathiri watu wa pande zote hizo mbili, basi hoja
  za kwanini uhusiano huo uvunjwe hazina budi kuwekwa
  hadharani.

  Hili ni lazima lifanyike ili mahusiano hayo
  yatakapovunjwa kusitafutwe kisingizio kingine cha
  kuvunjika kwake. Kwa kutangaza hadharani sababu hizo
  basi hisia za chuki, uonevu, kisasi, uzandiki, au uovu
  wowote zitaweza kuepukwa.

  Mahusiano na watawala yaweza kuvunjwa

  Kuvunja mahusiano na watawala si jambo geni wala
  jepesi kufanywa. Jamii mbalimbali duniani zimeweza
  kushuhudia kuvunjwa kwa mahusiano yaliyodumu kwa muda
  mrefu kati ya watawala na watawaliwa.

  Mahusiano ya namna hiyo yameweza kuvunjwa Marekani na
  utawala wa Uingereza (waliandika Azimio la Uhuru),
  Ukraine (Mapinduzi ya “Chungwa”), Lebanon (Mapinduzi
  ya Mierezi), Georgia (Mapinduzi ya Waridi) na Kenya
  (Ushirikiano wa Upinde wa Mvua). Hivyo, si jambo geni
  na si la pekee kwa watu kuamua kuvunja uhusiano na
  watawala wao, hata kama ni ndugu zao.

  Dhamira ya kuing’oa CCM

  Kwa kuzingatia historia yetu ya mahusiano kati ya
  Watanzania na chama chetu tawala cha CCM, tunaweza
  kudhamiria kukiondoa madarakani ifikapo uchaguzi wa
  mwaka 2010 kwa kuchukua Bunge la Jamhuri na ifikapo
  2015 kuchukua kiti cha urais.

  Vyote viwili vikiwezekana mwaka 2010, basi azma ya
  kuanza hatua za kulibadili taifa letu na kujenga taifa
  jipya la kisasa, lenye kuheshimu katiba, na lenye
  kuhakikisha kuwa wana na mabinti wa Tanzania
  wanafurahia haki sawa na nafasi sawa katika nchi yao,
  itatimia. Kuiondoa CCM madarakani kutafanyika endapo
  mkataba na vyama vya upinzani utakubaliwa na vyama
  hivyo.

  Sababu za kuing’oa CCM madarakani

  Ni kutokana na dhamira hiyo basi, nimeamua kuainisha
  sababu ambazo zinatufanya sisi wana na mabinti wa
  Tanzania bila kujali itikadi zetu, hali zetu za
  maisha, vyeo na hadhi zetu na vitu vingine
  vinavyotutofautisha kama mtu mmoja mmoja kama vile
  rangi, kabila, au dini kuvunja mahusiano yanayotufunga
  sisi na Chama Cha Mapinduzi na kukiondoa madarakani
  kwa njia ya kidemokrasia, kwa nguvu ya sanduku la
  kura, kwa kutumia sheria na taratibu zilizopo.
  Tumeazimia kufanya hivyo kwa sababu zifuatazo:

  Chama Cha Mapinduzi kimeenda kinyume kabisa na katiba
  yake, iliyotangaza kuwa Azimio la Arusha ndiyo dira ya
  taifa letu na iliyoweka maono ya kitaifa na hata
  tafsiri ya azimio hilo iliyotolewa Zanzibar.
  Kwa kufanya hivyo serikali ya CCM imeiingiza nchi
  katika siasa za kibepari (zenye msingi wa unyonyaji)
  bila kuwaambia wananchi wenyewe wakati katiba ya chama
  hicho na ile ya nchi bado vinatamka wazi na bayana
  kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa, yenye kujenga ujamaa
  (usoshalisti) kwa misingi ya kujitegemea.

  Chama Cha Mapinduzi kimeruhusu viongozi wake kuvunja
  Azimio la Arusha na maelekezo yaliyotolewa na Rais
  mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuhusu Azimio la Zanzibar
  kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Aprili 25 mwaka 1991.
  Miongoni mwa mambo ambayo viongozi wa chama hicho
  wanajihusisha nayo licha ya kukatazwa na Azimio la
  Zanzibar (Likifafanua Azimio la Arusha) ni pamoja na
  kupangisha majumba, kuwa na shamba la zaidi ya hekta
  20, kupokea mishahara zaidi ya mmoja wakiwa wamevaa
  kofia zaidi ya mbili za serikali au chama.
  Chama hiki hivi karibuni kimefurahia kutimiza miaka 30
  tangu kuzaliwa kwake, na bila hata hofu wameshindwa
  kutaja kabisa miaka 40 ya Azimio la Arusha na hivyo
  kuthibitisha kuwa azimio hilo limekufa kiujanja na
  kuzikwa kinyemela. Kama CCM ingekuwa na wasema kweli
  angalau wangelisema kuwa Azimio la Arusha limekufa, na
  maelezo ya azimio hilo ya kule Zanzibar nayo yamekufa,
  kila mtu na lwake.

  Chama Cha Mapinduzi kwa kupitia Bunge la Jamhuri ya
  Muungano na wabunge wake ambao ndio wengi bungeni,
  kimeshindwa kuisimamia serikali ya Jamhuri ya Muungano
  na hivyo kuifanya isiwajibike kwa wananchi kama
  inavyopaswa.
  Ni Bunge lenye wingi wa wabunge wa CCM ambalo
  limeiacha serikali yake kuingia katika mikataba mibovu
  na isiyo na maslahi kwa nchi kama ile ya madini na
  nishati (mifano ya IPTL, Richmond, na Buzwagi iko
  mawazoni), na mikataba ya uendeshaji wa kampuni za
  Kitanzania kama ile ya Tanesco na Dawasco na mingine
  ya ubinafsishaji.

  Ni wabunge hao ambao wamegoma kutunga sheria ambayo
  ingewapa uwezo wa kuiangalia na hata kuitengua
  mikataba yoyote ambayo haina maslahi kwa taifa au
  yenye athari mbalimbali kwa wananchi, mazingira, na
  usalama wa taifa.

  Ni bunge hili ambalo licha ya vyanzo vingi vya kodi,
  limeshindwa kupitisha vyanzo vipya vya kodi ambavyo
  vingelifanya taifa letu kuwa na uchumi huru zaidi na
  si tegemezi. Bunge letu bado limeshindwa kubuni vyanzo
  vipya vya mapato ili hatimaye bajeti yetu iwe huru
  kutoka kwa wafadhili na wahisani.

  Ni Bunge hilo hilo la wingi wa wabunge wa CCM
  lililoshindwa kabisa kuikemea serikali hasa
  ilipojihusisha na ununuzi wa ndege ya kifahari ya rais
  pamoja na rada isiyokidhi mahitaji yetu, na yenye
  gharama kubwa.
  Bunge hili limeshindwa kumtaka rais kuruhusu ripoti ya
  Benki ya Dunia kupinga ununuzi wa rada hiyo kuwekwa
  hadharani ili wananchi wajue ni jinsi gani ununuzi huo
  ulikosa busara na sababu ya msingi.

  Serikali ya CCM imeshindwa kukemea viongozi wake
  waliotumia ofisi zao za umma vibaya na kuwavumilia kwa
  kuwalinda. Kitendo cha Serikali ya CCM kukubali na
  kutoa baraka yake kwa rais mstaafu kufanya shughuli
  binafsi Ikulu, na kuruhusu maafisa wake kuwa na hisa
  katika kampuni ambazo wao wana maslahi, na kitendo cha
  kutaka wananchi wapuuzie hoja zinazohoji utaratibu
  huo, ni kitendo kinachoonyesha ni jinsi gani chama
  hiki kimelewa madaraka. Kwa kufanya hicho CCM si tu
  imejenga misingi mibovu ya maadili, bali pia
  imeonyesha mfano mbaya kabisa kwa viongozi wa mbeleni.

  Chama Cha Mapinduzi kwa kupitia serikali zake,
  kimeshindwa kuipa sekta ya elimu mkazo na msisitizo
  unaostahili na hivyo kushindwa kuleta mabadiliko ya
  kielimu yanayotakiwa katika kuleta mageuzi makubwa ya
  kiuchumi na kijamii.
  Licha ya kuongeza idadi ya shule, madarasa, wanafunzi
  na vyuo, serikali ya CCM imeshindwa kuinua ubora wa
  elimu ya kati na ya juu na hivyo kushindwa kuandaa
  taifa la wasomi waliobobea, watafiti mahiri, na
  wachunguzi wa mambo waliofuzu.

  Badala yake wasomi wale wachache ambao Tanzania inao
  wameishia kuwa wanasiasa, na wale walioko katika
  taaluma maslahi yao ni duni sana na hivyo wengine
  kuamua kwenda nje ya nchi na wengine kutokujihusisha
  kabisa na mambo ya ndani ya maendeleo ya Tanzania.
  Hili linadumaza elimu ya kizazi kijacho cha wasomi.

  Matokeo yake ni kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kubuni
  mikakati inayowezekana ya kuiinua Tanzania kitaaluma
  na kuipatia faida ya kiushindani katika soko la ajira
  za ndani na za kimataifa.

  Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeshindwa kujenga na
  kuendeleza sekta nzuri, ya kisasa, na iliyo endelevu
  ya afya na badala yake matatizo ya magonjwa ya
  milipuko yasiyo ya lazima bado yanaendelea kuua watu
  wetu na kudhalilisha utu wa Watanzania.
  Licha ya mafanikio kidogo ya hapa na pale ya ujenzi wa
  majengo ya hospitali na kliniki, Serikali ya CCM
  imeshindwa kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya
  magonjwa makubwa, kupunguza vifo vya watoto na hasa
  kuhakikisha upatikanaji wa chanjo za watoto ambazo
  zimepungua kwa kiasi kikubwa sasa hivi.

  Ni serikali ya chama hicho ambayo imeshindwa kufanya
  sekta ya afya kuwa ya kisasa zaidi na inayowafikia
  watu wengi zaidi na kwa muda mfupi zaidi.

  Ni kutokana na kushindwa huku ndio maana Serikali ya
  CCM imejiwekea utaratibu wa kupeleka viongozi wake nje
  ya nchi huku watu wa kawaida wakiendelea kuhangaika
  kila kukicha kutafuta huduma bora za afya. Hata
  zinapotokea ajali, viongozi wao watapelekwa nje, na
  wale waliokuwa nao watatibiwa humu humu nchini.

  Kwa kukimbilia uwekezaji katika madini na utalii na
  kutokuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta
  ya sfya, Serikali ya CCM inatengeneza taifa la watu
  dhaifu na walio goigoi na ambao afya zao ziko shakani.

  Licha ya kuendelea kuimba wimbo wa “Kilimo ndio uti wa
  mgongo wa taifa” na licha ya kutambua kuwa wananchi
  wetu wengi wameajiriwa katika kilimo, Serikali ya CCM
  imeshindwa kabisa kubadilisha kilimo chetu na
  kukifanya kuwa cha kisasa na kinachotosheleza mahitaji
  yetu na ziada.
  Serikali ya chama hiki imeshindwa kuongoza mapinduzi
  ya kilimo licha ya ahadi nyingi, ambayo yangesababisha
  tuachane na jembe la mkono na kuleta kilimo ambacho
  kimeanza kutumia mashine za kisasa, utaalamu wa
  kisasa, na taratibu za kisasa za kilimo na hivyo
  kukifanya kisiwe cha kujihifadhi tu bali kiwe cha
  kutosheleza mahitaji ya nyumbani na ziada. Wameshindwa
  kufanya hivi licha ya nchi yetu kuwa na Chuo Kikuu cha
  Kilimo na taasisi mbalimbali za utafiti wa mazao na
  mifugo ambazo zinafanya kazi chini ya uwezo wake
  kupita kiasi.

  Serikali ya CCM inaamini kuwa Tanzania pasipo CCM
  madarakani haiwezekani. Tabia ya baadhi ya viongozi wa
  chama hicho na vyombo ambavyo vimo kwenye mikono yao
  kuendelea kutishia wananchi kuwa endapo chama kingine
  kitashika madaraka basi nchi itaingia matatani na
  kutatokea machafuko makubwa ni tabia ya watu
  walioishiwa hoja na yenye lengo la kutishia watu.
  Vitisho hivyo vya mara kwa mara vinavyofanywa na
  baadhi ya viongozi hawa vina lengo la kutaka kuendelea
  kujikita zaidi madarakani kwa kutumia hofu na mbinu za
  vitisho. Kwa kuendeleza mbinu hizi zilizopotoka,
  serikali ya CCM inataka kuendeleza utawala wake kwa
  kuchezea hisia na vionjo vya wananchi kwa mbinu chafu
  za kuwatishia.

  Kwa makusudi kabisa wameamua kuziacha na kuzitupilia
  mbali fikra za Mwalimu Nyerere, fikra ambazo msingi
  wake ulikuwa ni “kujenga taifa la watu walio huru na
  sawa”, na taifa ambalo kila mtu ana “haki ya
  kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”. CCM wamejikuta
  wakibadili maana ya maendeleo kutoka maendeleo ya watu
  na kuwa maendeleo ya vitu.
  Kwa kufanya hivyo, wametilia mkazo umwagaji wa mapesa
  na vitu bila kuathiri maisha ya mtu wa kawaida.
  Matokeo yake ni tofauti ya maisha ikiendelea kuonekana
  kati ya watu na vitu, huku wachache wakiendelea
  kunufaika kwa vitu huku wengi wakiendelea kutaabika.

  Azimio

  Kwa kuzingatia sababu zote hizo na nyingine ambazo mtu
  mmoja mmoja anaweza kuwa nazo, tukitambua kuwa Chama
  Cha Mapinduzi kimepewa nafasi nyingi za kujirekebisha,
  na kimeshindwa kufanya hivyo na badala yake kuendelea
  kutawala bila kujali hisia na maslahi ya wananchi,
  tukifahamu kuwa nchi yetu haiwezi kusonga mbele na
  kupiga hatua ya haraka ya maendeleo kwa kadiri ya
  kwamba CCM bado iko madarakani, tunajikuta
  tunakabiliwa na uamuzi mmoja tu wa makusudi, wazi, na
  dhahiri, ambao tunaweza kuuchukua.

  Sisi wananchi wa Tanzania, tulio nyumbani na
  ughaibuni, tukiwa na vingi vinavyotutofautisha kama
  mtu mmoja mmoja, kama vile rangi, dini, nasaba,
  makabila, vyeo, hadhi, nk na ambao tuko ndani na nje
  ya CCM, ndani na nje ya upinzani na wale ambao
  hatufungamani na chama chochote au itikadi yoyote ya
  kisiasa tukiunganishwa na tunu za utii kwa nchi na
  uzalendo kwa taifa, na tukisukumwa na matamanio kuwa
  siku moja watoto na watoto wa watoto wetu wataikuta
  nchi hii iliyojaa fanaka na neema, tunajikuta
  tukitangaza mara moja na daima kuwa:

  Chama Cha Mapinduzi, ni lazima kiondolewe madarakani
  kwa kutumia njia za kidemokrasia na kwa kutumia nguvu
  ya sanduku la kura kwenye uchaguzi wa 2010 kwa
  kuwanyima wagombea wao kura za ubunge na uwakilishi
  mwingine wowote ule.

  Na pia tunakoelekea huko tutaanza kuwanyima kura za
  uwakilishi katika chaguzi ndogondogo zinazofanyika
  kuanzia sasa kama za madiwani, kama ishara ya
  kuonyesha kuwakataa kwetu na kukataa sera zao ambazo
  zimeifikisha nchi yetu hapa ilipo.

  Azimio hilo tunaliingia sisi kama mtu mmoja mmoja na
  kama jumuiya, tukijua kwa hakika kuwa kuondoka kwa CCM
  madarakani kunawezekana, na tukitambua kuwa kushindwa
  kuiondosha CCM madarakani ni kuendeleza utawala wa
  chama kisichojirudi na ambacho kimebadili sera zake za
  kujali wakulima na wafanyakazi wa nchi hii, na badala
  yake kukumbatia kundi la watu wachache wenye kujali
  maslahi binafsi zaidi kuliko ya taifa na mwongozo wa
  katiba.

  Tunaweza kuazimia hayo tukiwa na akili timamu, bila
  shurti, vitisho, ahadi ya cheo au madaraka, tukijua
  wazi kuwa kwa kuweka majina yetu hadharani tutakuwa
  tumeonyesha kitendo kikuu cha kutowakubali CCM.

  Tunaweza kufanya hivi kwa ajili ya mapenzi ya nchi
  zaidi kuliko kitu kingine chochote. Mungu atusaidie.

  Pindi azimio hili likikubalika na wananchi wengi,
  tutaweka hadharani mkataba na vyama vya upinzani ambao
  ni lazima waukubali wote au waukatae wote.

  Wakiukubali tutawapa Bunge mwaka 2010; wakiukataa
  tutawapa tena nafasi CCM lakini tutaendeleza mapambano
  ya kifikra hadi CCM ibadilike au chama kingine
  kiimarike na kuweza kuchukua nafasi ya CCM kwa
  kuzingatia misingi ya mkataba huo.

  Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mada hii ni sawa na mada nyingine ambazo mara nyingi zimekuwa zikitoa tatizo na nadhalia ya suluhisho la matatizo yetu pasipo kutoa mchakato mzima wa utatuzi. Matokeo yake tupo na tutabaki pale pale, na ccm itabaki palepale ikiendeleza ufisadi. JF tutabaki pale pale tukibweka kila siku pasipo kuibadirisha nchi.

  CCM haitang'oka kwa wapinzani kukesha kwenye internet na kuanzisha utitili wa magazeti yanayopinga hata mazuri yanayofanywa na serikali. Huku ni kujidanganya na kuadaa watu.

  CCM haitaondoka madarakani kwa wapinzani kutembea kila mkoa wakitangaza mabaya ya ccm huku wakiacha kutangaza sera zao. Naam, nani hasiyeyajuwa mabaya ya ccm tangu ilipoundwa? Je ni asilimia ngapi huko vijijini wanajuwa sera au ilani za Chadema, Cuf, TLP, DP nk? Wapinzani wamekuwa kichekesho, wamekuwa waigizaji wanaovuta maelfu ya watu kuja kusikiliza orodha ya mafisadi badala ya kusikiliza sera zao. kwa mtaji huu, ccm tunayo, na tutakuwa nayo kwa karne kadhaa.

  CCM ipo madarakani si kwasababu inapendwa lah. Kwasababu haina mpinzani, wapinzani wamekuwa disappointment kwa wananchi. CUF wanasikika tu mara uchaguzi unapoisha wakilalamika kuibiwa kura, uchaguzi ukiisha wakapata maslahi ya muafaka huwasikii tena. Chadema wako busy na list ya mafisadi na kupoteza muda wao mwingi JF kujibu mada za ajabu ajabu zilizoanzishwa na watu walio nje ya nchi wasiopiga kura. Inasikitisha, inakasirisha, inahurumisha. Ufisadi na mabaya mengine yanayofanyika serikalini yamepoteza mwelekeo wa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2010....na hii ni faida kwa ccm ambayo hapa tunaposema inafanya uchaguzi wakujiimarisha huku ikijuwa kwamba mfupa wa ufisadi umesha distruct chembe chembe zozote za juhudi za wapinzani kushika madaraka.

  Sasa ccm itaondoka vipi? Ili ni swali ambalo mara nyingi JF tumekuwa tukilikwepa. Mada nyingi juu ya kuiondoa ccm zimeishia kutoa sababu za kwanini ccm iondoke..kama wanavyofanya wapinzani. Katika kujibu swali hili ni vyema tukajuwa ni nani aiondoe ccm na kwa njia gani? Kwa kawaida tunategemea wapinzani ndio waiondoe ccm kwa njia halali za kidemokrasia.

  Njia hii inahitaji msambao wa upinzani katika ngome za cmm. Hili bado wapinzani wetu hawajalifanya, badala yake wanasambaza list za mafisadi. Vijiji vichache sana vina matawi ya wapinzani, licha ya takwimu kuonyesha kwamba nguvu haswa ya ccm iko vijijini. uhaba wa matawi ya wapinzani katika ngome za ccm ni ishara tosha kwamba upinzani hauna watu na kwamba kupigia kura upinzani kwa matarajio ya kuiondoa ccm ni sawa na kujaribu kuhamishia bahari kwenye kopo.

  Sambamba na hili, wapinzani wameshindwa kabisa kuwapa wananchi chaguo la sera. Ilani za ccm zimejaa vijijini, itakubidi utembee vijiji kadhaa kupata ilani ya cuf na Chadema. Siasa za vyama vingi bado haijaeleweka kwa wapinzani; mwananchi anakesha kuambiwa maovu ya ccm badala ya kuambiwa ubora atakaoupata atakapo amua kukipigia kura chama pinzani. Anakosa chaguo, na, "labda" anakosa mabadiriko ya kweli.

  Njia za kuindoa ccm ni; (i)upinzani lazima uwe na mikakati inayolenga long-term. Mikakati hii itilie mkazo sana juhudi za kusambaza matawi vijijini ambako ccm ndio ina nguzo. Kama upinzani utaendelea kukosa msambao vijijini basi jitihada za kuleta mapinduzi zitaendelea kurudi maili tisini na kenda nyuma kila mwaka. (ii) msambao wa sera za upinzani ufike vijijini ili utoe chaguo kwa wananchi. Kwa usahihi na urahisi mwananchi ajue ubora wa chama pinzani dhidi ya ccm. KUTANGAZA UBAYA WA CCM KAMWE HAKUHUSIANI NA KUTANGAZA UBORA WA UPINZANI. (iii)wapinzani lazima waonyeshe utashi na uelewa kwa wanananchi. Inasikitisha kuona viongozi wa upinzani wanaleta siasa za tunguli kila panapotokea ajali au kifo cha mwanasiasa wa ccm. Inasikitisha kuona kila jambo linaloamuliwa na serikali linapingwa na wapinzani. mishahara hisipopandishwa wapinzani wanalalamika, ikipandishwa bado wanalalamika. Mwananchi anawashangaa nakuwaona wapika majungu...UFIKE WAKATI WAPINZANI WAKUBALI KINACHOKUBALIKA NA WANANCHI NA KUSEMA KWAMBA KUWAPO KWA UPINZANI KUMEFANIKISHA MAENDELEO.

  Hitimisho ni kwamba mchakato wa wapinzani kuiondoa ccm lazima uangalia miaka 20 ijayo. Sera zao ndio zitakazowafanya wauzike kwa wananchi sio list za mafisadi. Watanzania wanajuwa mabaya ya ccm tangu uhuru lakini ni wachache sana wanajuwa ubora wa wapinzani.
   
 3. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  mbaya zaidi source ya hii habari ni freemedia, (tanzania daima)
  ambapo freemedia=Mbowe=Chadema. so am not even paying attention to this !
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni kweli ndugu mgonjwa usemayo lakini Ilani za CCM kujaa huko kijijini kwenu ni kwa vitendo ama maneno na kwenye vitabu? Hivi unaweza kuwa mchambuzi namna hii then uje ukatae kwamba Chadema ama upinzani hawna sera kweli ?Kwa kuwa kuna wana Chadema na CUF hapa at least nitaachwa waje na Ilani yao na sera zao tuone kama hazijawa copied na CCM na wanajaribu kuzitumia lakini hawawezi maana si waasisi na CCM hairuhusu mambo yale kutendewa wananchi.

  Hivi kumbe kutetea kote bado unadhani wapinzani kuusema uozo wa CCM ni dhambi na kupoteza muda ? Ndoto yako ya miaka 20 ijayo CCM kuwa madarakani ondoa na ukiendelea na hili utakuwa unawadanganya wenzio huko mliko.

  Siku CCM itaacha kutumia usalama , polisi na kukimbia na masanduku ya kura na kuwahinga watu nguo na chumvi ndiyo itakuwa mwisho wao .haya wanafanyiana wenyewe kwa wenyewe hata Mangula kasema wewe unasemaje ? Au ndiyo ilani yenyewe hii unayo hubiri hapa ?

  Ufisadi unapashwa kukemewa na kila mtanzania mwenye nia njema maana huu unaweza kulitumbukiza Taifa katika vita au wewe unaona ni dhambi kubwa kwa kuwa wanao semwa no CCM ?
   
 5. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,217
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Tatizo la wakereketwa na makada wanamuona Mangula kama mpinzani, lakini wajue kuwa anajua anachokisema, kwani alishakifanya mwenyewe na ameona madhara yake. Sema shida moja ni kuwa itifaki zote hizi za masanduku na uchafu mwingine alisaidia kuufanikisha, kwa hiyo amesaidia kobomoa chama.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 2, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimeiweka kwenye pdf...
   

  Attached Files:

 7. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Iwe kwa maneno ama vitendo; matokeo ndio yana matter the most. Huko vijijini wananchi wanaichagua ccm, which tells me kwamba ccm inauzika kuliko wapinzani.

  Of course chadema watakuja watujibu hapa kwenye internet badala ya kwenda kujibu wananchi na kusambaza hizo sera zinakotakiwa. Chama cha internet.

  Sasa tatizo hapa liko wapi? At first unaonyesha kwamba ku-copy ni kosa, then unasema kwamba ata wakikopi hawawezi kuzitekeleza. Therefore, copying or not copying won't do harm to Chadema endapo watazianika sera zao hapa.

  Kupoteza muda, ndivyo nilivyoosema. Hiyo ya dhambi unaisema wewe. Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba wananchi wanayajuwa sana madhambi ya ccm, wala hawana haja ya kukumbushwa kila kukicha. Wananchi wanataka chama kinachouzika kwa sera sio kwa kutoa list ya mafisadi. Wapinzani are wasting precious time ambayo wangetumia kujijenga badala ya kubomoa ccm.

  Mzee mwenzangu, wewe ndo umeanzisha hii mada ukisema ccm itaondolewa. Labda nilikosea kuzani kwamba ulimaanisha ccm ingeondolewa kwa kura za wananchi. It seems sasa umepiga U-turn kwamba ccm haitaondolewa kwa kura maana polisi, mbio za masunduku ya kura, kanga, chumvi, na hayo aliyoyasema Mangula bado yako. Labda nikuulize, uliposema ccm itaondolewa ulikuwa na maana itaondolewa kwa njia ipi?


  Kweli kabisa, ufisadi unatakiwa kukemewa! Ila kukemea ufisadi hakutoshi kukifanya chadema kishinde uchaguzi. For your information wanaokemea ufisadi sio Chadema tu, tumeona ccm damu damu wakikemea ufisadi publicly. Upinzani need to do more than simply adding names to the list of shame....they should add their political ideology and number of followers in ccm's strongholds.
   
Loading...