Anachotakiwa kufanya kiongozi wakati wa Crisis

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakati wa “Crisis” watu husubiria kusikia kiongozi anasema nini

Tarehe 4 mwezi wa tatu mwaka 1933, aliapishwa Rais wa 32 wa Marekani...

...Franklin D. Roosevelt baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Herbert Hoover.

Roosevelt alichukua hatamu katikati ya kipindi kigumu sana cha uchumi kudorora (Great Depression).

Katika mengi yanayokumbukwa katika siku zake za awali ni maneno maarufu kutoka katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kuapishwa aliposema...

”The only thing we have to fear… is fear itself..”

(Kitu pekee tunachopaswa kukihofia ni hofu yenyewe).

Baada ya hapo aliendelea kuonesha namna ambavyo Taifa la Marekani lina nguvu...

...na uwezo wa kukabiliana na changamoto kubwa za uchumi ambazo zilikuwepo kwa wakati huo.

“This is no unsolvable problem if we face it wisely and courageously.

There are many ways in which it can be helped, but it can never be helped merely by talking about it.

We must act and act quickly.”

(Hili sio tatizo linaloshindikana kama tukilikabili kwa hekima na ujasiri.

Kuna njia nyingi linaweza kupatiwa ufumbuzi, ila sio kwa kuliongelea bali kwa kuchukua hatua tena kwa haraka).

Maneno haya machache ila yenye nguvu kubwa, yaliinua ari na tumaini la wamarekani katika kupambana...

...na changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili na hatimaye waliishinda.

Aina 2 za Viongozi Wanaoibuka Kwenye “Crisis”

Kila inapotokea changamoto kubwa ambayo inaonekana haina majibu (Crisis)...

...utafiti umeonesha kuwa kuna makundi mawili ya viongozi huibuka.

Hii ni kwa mujibu wa nadharia ya mwanasaikolojia maarufu Julian B. Rotter (1954):

i. Ni wale ambao wanatoa visingizio ili kuonesha kuwa tatizo lililopo halijasababishwa na wao na hakuna suluhisho linaloweza kupatikana ili kulitatua.

Yaani wanataka watu walikubali tatizo na waishi nalo.

Hawa wanawekwa kwenye kundi la “External Locus of Control”.

ii. Pili ni wale ambao wanaamini kuwa kwa kutumia maamuzi yao, ubunifu na kupata mawazo kutoka kwa watu mbalimbali wanaweza kupata suluhisho la tatizo ambalo linawakabili.

Hawa wanawekwa kwenye kundi la “Internal Locus of Control”.

Kundi la kwanza wakiwa wengi kwenye nafasi za uongozi, husababisha tatizo kutokuisha na litachukua muda mrefu sana.

Mara nyingi hawapendi kushirikisha wengine kwenye kutafuta suluhu na wanaishia kulalamika na kulaumu wengine.

Kundi la pili wakiwa wengi kwenye uongozi husaidia kutafuta suluhisho la haraka kwani mara nyingi sio waoga na wako tayari “kurisk” ili wapate suluhisho.

Kiongozi lazima afanye yafuatayo ili kupata suluhisho.

Katika kuwasaidia viongozi mbalimbali, hasa katika nyakati ngumu wanazokabiliana nazo...

...Taasisi ya “National Democratic Institute” ya nchini Marekani iliwahi kutengeneza “Political Decision - Making Framework”...

...ya kumsaidia kila kiongozi kufanya maamuzi haswa wakati wa majanga makubwa na changamoto nzito.

Hii ni muhimu kwa sababu kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu cha “Crisis Leadership” Gene Klann...

...alisema kuwa “During a crisis, your goal is to reduce loss and keep things operating as normal as possible.”

(Wakati wa majanga, lengo lako ni kupunguza hasara na kuhakikisha vitu vinakuwa kawaida kadiri unavyoweza).

Katika mambo mengi ambayo “Political Decision - Making Framework” inatoa muongozo, kuna mambo mawili ya msingi unatakiwa kuyazingatia wakati wa “Crisis”:

a. Uonekane na Upatikane (Be present and Available).

Moja ya kitu mbacho kinaweza kufanya changamoto izidi kuwa kubwa ni...

...kutoonekana au kutopatikana kwa kiongozi.

Wakati huu uwepo wa kiongozi sio wa hiari ni wa lazima.

Hii ni muhimu kwa sababu, kiongozi asipoonekana, huwa anatoa nafasi ya watu kuzungumza kila kilichopo hata vile ambavyo sio vya kweli...

...na kwa sababu ya taharuki, watu wanaamini chochote na wanaweza “kureact” kutokana na taarifa walizonazo.

Hii ndio maana Musa alipoenda kumlilia Mungu walipokwama, mbele bahari ya shamu, nyuma majesho ya Farao, akamwambia...

...“Usininilie mimi, rudi kawaambie wana wa Israel wasonge mbele”.

Kwa maneno mengine, kiongozi hatakiwi kutoa kilio cha kukosa matumaini wakati wananchi wanalia pia...

...kiongozi hatakiwi kutoonekana wakati wakati wa changamoto.

Watu wanataka kuisikia sauti yako, watu wanataka kukuona.

Nyakati hizi lazima utumie 3R’s za mawasiliano:

Review, Repeat, Reinforce

a. Hakikisha kila wakati unapitia maoni ya watu, rudia tena na tena kueleza mwelekeo unaouchukua bila kuchoka.

b. Husisha watu wote muhimu kupata suluhisho la haraka.
(Strategic Engagement)

Mara nyingi, kunapokuwa na Crisis, viongozi wengi hupenda kujifungia wenyewe na kutafuta suluhisho wenyewe.

Hata hivyo, imeonesha kuwa, kwa sababu ya msongo wa mawazo ambao viongozi wengi wanakuwa nao...

...aidha huchelewa kufanya maamuzi ama huishia kufanya maamuzi yasiyo na tija.

Wakati wa “Crisis” ni wakati wa kusikiliza wadau wote muhimu kadiri unavyoweza.

Chukua michango yao na kisha “issumarise” kisha ka ana wataalamu wako kufanya maamuzi ya mwisho.

Mara niyngine, suluhisho halitatoka ofisi kwako, wako watu nje ambao wanaweza kuwa msaada wa kukupa jawabu la changamoto unayopambana nayo.

Viongozi wengi huogopa kuruhusu watu kusema mawazo yao kwa hofu ya kukosolewa.

Usisahau maneno ya aliyekuwa Secretary of State nchini marekani aliposema...

...“Leadership is solving problems.

The day soldiers stop bringing you their problems is the day you have stopped leading them.

They have either lost confidence that you can help or concluded you do not care.

Either case is a failure of leadership”.

(Uongozi ni kutatua matatizo ya watu.

Siku ambayo wanajeshi wanaacha kukuletea matatizo ndio siku umeacha kuwa kiongozi wao.

Hii ni kwa sababu watakuwa hawakuamini tena au wameona haujali.

Kwa vyovyote vile inamaanisha umefeli kwenye uongozi wako).

NB: Nakupatia zawadi ya kitabu changu cha “Surviving The Crisis” ili ujisomee zaidi kuona kile ambacho viongozi wanafanya nyakati za changamoto kubwa.
 
N:B Nakupatia zawadi ya kitabu changu cha “Surviving The Crisis” ili ujisomee zaidi kuona kile ambacho viongozi wanafanya nyakati za changamoto kubwa.
Kupanda bei ya mafuta is not a crisis - Acha ushamba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom