Kidamva
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,578
- 1,984
Kumekuwa na malumbano kuhusu hatua ya Rais Magufuli kukomalia mchanga wa dhahabu (makinikia).
Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu amekosoa hatua hiyo akisema kinachotakiwa ni kufunga mikataba kwanza vibginevyo tutashitakiwa na tutashindwa.
Hali hiyo ndio inayojitokeza kwenye mkataba wa IPTL na Serikali ulioingiwa mwaka 1994.
Kila mwezi Tanesco inailipa IPTL zaidi ya sh3 billion kama service charge. Ni mkataba uliozua Maneno mengi kwa miaka mingi.
Lakini juzi Ewura wameitisha maoni ikiwa ni mchakato wa kuongeza leseni ya IPTL. Kelele zimeanza, wanaharakati na wanasiasa wanahoji kwanini IPTL ipewe leseni wakati mkataba wake una harufu ya ufisadi.
Lakini Ewura wanasema IPTL ina mkataba wa kuzalisha umeme hadi mwaka 2022, hivyo wanatakiwa waongezewe leseni.
Issue hapa ni sheria. Kosa tulilofanya ni kuingia mikataba mibovu na waliohusika wapo wanadunda tu.
Ndicho anachokisema Lissu, sheria sheria sheria.