Uchaguzi 2020 Anachokifanya Tundu Lissu kwa sasa ni kutafuta umaarufu kwa ajili ya 2025

rose mzalendo

Member
Mar 5, 2019
71
114
Tundu Lissu ni mwanasheria maarufu ambaye ameeendesha kesi nyingi nchini kwa mafanikio.

Aidha, kwa kipindi sasa amekuwa akijihusisha na masuala ya siasa, na kwa mwaka 2020 ameteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya CHADEMA.

Kufuatia mchakato wa uchaguzi unaoendelea tarehe 26.08.2020 alipeleka pingamizi dhidi ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Mh. JOHN POMBE MAGUFULI.

NIA YA TUNDU LISSU
Kwa kifupi Tundu Lissu alichokifanya dhidi ya Mgombea wa CCM kinatoa tafsiri kuwa:
1. Anatafuta umaarufu wa Kisiasa na hasa ukizingatia alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu.
2. Katika hatua ya kujionesha kuwa anauwezo wa kumpinga Rais JPM waziwazi (kifupi ni mashindao ya kitoto)
3. Anajuwa wazi kuwa uwezo wa kushinda katika uchaguzi huu Octoba 2020 hana hivyo anachokifanya ni maandalizi ya uchaguzi wa 2025.
 
Lisu kwa Sasa haelewi hata aanzie wapi chama pesa hakina na yeye pesa Hana

Sasa hivi watonyaji wanasema anaelekea Kwao kwa mganga wa kienyeji sijui kwa ajili ya nini
Mnahaha, subirini kidume kinarudi tena
 
Mkuu Rose Mzalendo, nadhani wewe ni kada mwenzangu wa chama chetu, uzalendo wa kweli sio kujiita mzalendo bali kuwa ni mzalendo wa ukweli. Mzalendo wa ukweli kwanza yeye mwenyewe atakuwa ni mkweli, na ataibua hoja za ukweli anaoujua.

Japo mimi ni kada lakini nakiri Lissu ni maarufu na zile pingamizi zake ni valid kisheria ila ni voidable na sio void. Ili kujua kuwa kweli ni voidable subiria picha za mgombea urais kwenye karatasi ya kura if it's the same.

Ombi kwa Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi, naomba makosa mengine yote madogo madogo kwenye ujazaji fomu ambayo sio void bali ni voidable kwa wagombea wote, yawe tolerated na waruhusiwe kurekebisha wapitishwe!

P
 
Hivi nyie mashabiki ndakindaki wa ccm lini mtakuwa waelewa? Lissu alimwekea pingamizi rais au mgombea mwenzake?

Sasa kama tu tafsiri ya rais na mgombea hamwelewi lini mtakuja kumwelewa Lissu ambaye ana IQ kubwa?
Wanaitwa incumbents kwa kimombo.
 
Si kweli. Tl anasumbua kweli na dawa take bado haijapatikana, Kama usemalo ni kweli basi taifa zima na taasisi zake linacheza na akili ya mtoto michezo ya kitoto.
 
Tundu Lissu ni mwanasheria maarufu ambaye ameeendesha kesi nyingi nchini kwa mafanikio.

Aidha, kwa kipindi sasa amekuwa akijihusisha na masuala ya siasa, na kwa mwaka 2020 ameteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya CHADEMA.

Kufuatia mchakato wa uchaguzi unaoendelea tarehe 26.08.2020 alipeleka pingamizi dhidi ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Mh. JOHN POMBE MAGUFULI.

NIA YA TUNDU LISSU
Kwa kifupi Tundu Lissu alichokifanya dhidi ya Mgombea wa CCM kinatoa tafsiri kuwa:
1. Anatafuta umaarufu wa Kisiasa na hasa ukizingatia alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu.
2. Katika hatua ya kujionesha kuwa anauwezo wa kumpinga Rais JPM waziwazi (kifupi ni mashindao ya kitoto)
3. Anajuwa wazi kuwa uwezo wa kushinda katika uchaguzi huu Octoba 2020 hana hivyo anachokifanya ni maandalizi ya uchaguzi wa 2025.
Pingamizi ni kwa mujibu wa sheria
 
Back
Top Bottom