Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,743
NInashare nanyi ujumbe nilioukuta kwenye Whatsapp Group
Hizi picha zimesambaa sana mitandaoni these few days.
Mtanisamehe kama ninawakwaza kwa kuiweka hiyo. Lakini nina lengo la kuijadili kidogo.
Huyu Mch. Masanja anapitia wakati mgumu sana kipindi hiki kutokana na mtiririko wa matukio yaliyomtokea na hasa kadhia iliyojiri baada ya kifo cha Katibu wa Kanisa lake. Yamesemwa mengi na yeye ameongea mengi pia.
Kuna jambo ambalo naona jamii haijastukia nalo ni kutumika kwenye vita baina ya Masanja na wanaopambana naye.
Kuna jambo linalazimishwa ambapo ikifikia hatua watu kuitaka polisi ichukue hatua ya kumhoji Masanja na Mkewe kuhusu kifo kile. Hata baada ya ufafanuzi wa polisi kuhusiana na uchunguzi wa awali, lakini bado watu hao wenye malengo hasi wamehamia kwenye kuisambaratisha familia.
Inaonekana lengo kubwa ni kuhakikisha familia ya huyu mtumishi isiwe na utulivu hata wa kutafakari na kujirejeleza baada ya matukio haya waliyopitia.
PICHA
Hizi picha zinasambazwa kwa lengo mahsusi kumchafua ama kudhalilisha mwanamke na hata kumshambulia marehemu. Sisi leo tunajipa uhalali wa kuhukumu wakati tunajua kabisa kwa usahihi hatuna wema ama usafi wowote kiroho, kimawazo hata kitabia. Picha za mtoto zinasambazwa kama silaha ya kuhukumu na hata watetezi wa watoto wamekaa kimya.
Je lengo la wasambazaji ni kutaka mtoto adhuriwe? Inawezekana Masanja asifanye lolote kumdhuru mtoto. Je vipi kuhusu ndugu na washabiki wake? Je vipi ikiwa lengo la wanaosambaza hizi picha ni maandalizi ya kisaikolojia kwamba wamdhuru mtoto ili jumba bovu limuangukie Masanja?
Tujifunze kuwa na kiasi. Tuishi kwa kudumisha mila na desturi nzuri kwamba kumsema marehemu ni sasa na kumkaripia mtoto ambaye hajazaliwa bado. Tumsitiri huyu malaika wa Mungu kwani hapo baadaye akijakuwa mtu mzima na kukutana na stories zilizomchafua akiwa bado hajitambui anaweza kugeuka animal au akaathirika kisaikolojia.
Simtetei Masanja kwani hata mimi hapo mwanzo nilipeperushwa na upepo wa hawa wanaomchafua lakini nilipoona amezengumza neno la msamaha nikaanza kujenga picha namna jamii inavyoweza kujiponya kwa eneo la kusamehe na kuachilia. Msimkoseshe amani mke wake kwa sababu ya malengo maovu ya wanaomchafua.
Msimdhuru mtoto kwa kuharibu uwepo wake kupitia keyboards zetu.
Mungu wa Mbinguni awajaze hekima na awape kutafakari kisha kutenda yaliyo sahihi.
Atusamehe makosa yetu na kuponya magonjwa yetu
Atusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe waliotukosea