Anacho fanya Rais Samia ni haki yetu wala si huruma yake

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Habari za kushinda wakuu,

Nazani tunajionea kasi anayo endanayo mama Samia. Kutokana na kazi anazo fanya amejizolea sifa kemukemu(Nakiri kuwa anastahili Sifa hizo).

Lakini wananzego wanasema mama anahuruma sana kutokana na anacho fanya. Ni kweli huruma pengine anayo.

Kitu cha kujua wakuu ni kwamba anacho fanya Rais ni haki yetu wala si huruma yake.

Kwa mfano habari ya kuvifungulia vyombo vya habari vilivyo fungiwa na kuweka bayana makosa na adhabu ni haki yetu.

Pia swala la kushusha kodi ili tupate wawekezaji kutoka nje ni haki yetu.

Pia swala la vifurushi kupanda bei hii ni haki yetu ili vishushwe nazani hili tulilipigania.

Najua mnafahamu mambo mengi ambayo ni haki yetu yanafanywa na kuonekana ni huruma yake.

Hongera Rais wetu mama Samia kwa kutupigania.
 
Kuna alichosema ambacho kimeshageuzwa kuwa vitendo na kuleta athari chanya kwa jamii au mtu mmoja mmoja?
 
Ameshusha kodi?
Tatizo lililopo Sheria na kanuni za kodi zikifuatwa kama zilivyo nikwamba Kodi hazilipiki ni nyingi mno na kubwa Sana.

Inapaswa kuanza na kubadili Sheria, kanuni na taratibu za ulipaji Kodi la sihivyo itabaki kuwa maneno matamu na baadae kipya kinyemi upya wa rais ukiisha tunarudi palepale.
 
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom