Anaandika,ZITTO KABWE,katika ukurasa wake dhidi ya maamuzi ya kenya .

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,054
23,505
Ameandika Mhe Zitto Zuberi Kabwe

Kenya Kuzuia Gesi ya Tanzania: Tanzania ichukue hatua dhidi ya Kenya

Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo. Tamko la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya linasema ' ndani ya siku 7 kuanzia juzi tarehe 24 Aprili 2017, itakuwa ni marufuku Kwa Kenya kuagiza Gesi ya kupikia kutoka Tanzania '. Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.
Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa. Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.
Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.

Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania. Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.

Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo Kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma mjini
26/4/2017
 
sasa gesi ni Mali ya mwekezaji tanzania hatuna kitu hapo tusubirie robo ya faida ndo tupewe kama kodi huku mwekezaji akibeba mabilioni ya shilingi

ata neno LA mungu linasema na kila MTU afanye alivyokusudia moyoni make
 
Sioni ubaya wa Wakenya, wanalinda vya kwao kama sisi tumekubali kuwa dampo na source ya malighafi wacha tuendelee hivyo hivyo
USA japo UK ni mama yake lakini kasema buy american hire american.

Hatuko tena kwenye ujamaa tuko kwenye ubepari hakuna tena yale mambo ya huyu mkenya sijui msumbiji sijui msouth ndugu yangu as long as mna-meet kwenye kwenye viwango vya kibiashara sawa otherwise kila mtu akapambane kwa jeuri na nguvu zake
 
sasa gesi ni Mali ya mwekezaji tanzania hatuna kitu hapo tusubirie robo ya faida ndo tupewe kama kodi huku mwekezaji akibeba mabilioni ya shilingi

ata neno LA mungu linasema na kila MTU afanye alivyokusudia moyoni make
Nadhani nimemuelewa anazungumzia gas ile ya kupikia toka Iran and the likes inakuja Tz inajazwa then inapelekwa kenya
 
Wazuie tu kwani hayo mapato yanatusaidia nini? Wauze wasiuze ni saww tu.
 
Wazuie tu kwani hayo mapato yanatusaidia nini? Wauze wasiuze ni sawa tu.
 
Wakati wanachagua wabunge wa EALA chama butu waliangalia kujaza tu viti badala ya kupima aggressiveness ya wawakilishi, huu ndio mtihani kwa walioamua kujitoa ufahamu na kura zao za 'hapana'.
 
  • Thanks
Reactions: cai
Unajua nchi inavyoendeshwa wewe? Au unaandika tu kwa sababu umo kwenye mtandao na kuandika ni rahisi kwako
 
Sasa huko EALA ndo wamepeleka wale wasioweza kutetea hata utu wao ndo wataweza kutetea inji?
 
Back
Top Bottom