John Heche: Tarime haiwezi kuwa ya Kijani, itabaki kuwa Nyekundu.....

pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,213
1,228
Leo kumefanyika mkutano mkubwa sana wa siasa mkoan Mara -Tarime

Mh John Heche mbunge wa Tarime amechukua muda wake kupost picha za mkutano huo katika mtandao wa twitter

Picha ikionesha mamia ya watu waliohudhuria, na kwa kweli inavutia sana kuonesha ukuaji wa Demokrasia nchini, (Mwenye picha anaweza nisaidia kuweka hapa Tafadhali)

Kilichonivutia zaid ni caption au maneno yaliyo sindikiza picha hyo

Mheshimiwa Heche ameandika "Tarime haiwezi kuwa ya kijani, itabaki kuwa nyekundu"

Caption hiyo imenifanya nitafakari hasa, maana ya rangi za vyama vyetu vya siasa

Dunia nzima ina pigana kuwa ya kijani, pale ambapo tunahamasishana kupanda miti, kufanya recycle, kutumia bidhaa zenye kutunza mazingira ili kuwa na dunia ya "kijani" hapa Tanzania tuna wakina Heche ambao wanajiapiza kuwa Tarime haiwez kuwa ya kijani

Huku wakisisitiza kuwa Tarime itabaki kuwa " nyekundu "

Pengine ndugu msomaji,hii dhana isikuingie kichwani had nikukumbushe Tarime Nyekundu anayoitaka iendelee kubaki Bwana Heche ni ipi?

Ni Tarime Nyekundu ya Bwana Heche ambayo imejaa mauaji ya wazee vikongwe, umwagaji damu Nyekundu za wazee wasio na hatia

Ni Tarime Nyekundu ambayo raia wake wanaona fahari kutoleana mapanga hadharani, na kesi za kuchinjana zimejaa kila kituo cha polis

Ni Tarime Nyekundu ambayo mara baada ya matukio ya umwagaji damu kuzidi, yalifanya ipewe hadhi ya kanda maalumu kipolisi

Hii ndo tarime Nyekundu ambayo kiongoz anaapa kuwa haitakuja kuwa kijani

Nyekundu -Blood, Killings, Death
Kijani- Uoto asili, life, ukuaji

Alie buni rangi za CHADEMA alikuwa na lengo gani? Je kutupeleka kwenye umwagaji damu au?
 
Halafu mnasema Magu kabana democracy?
Magu kazuia mikutano?

Ila ukweli ni kwamba hilo jimbo Heche ajiandae tu sababu 2020 linarudi kwa wenye jimbo lao πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Halafu mnasema Magu kabana democracy?
Magu kazuia mikutano?

Ila ukweli ni kwamba hilo jimbo Heche ajiandae tu sababu 2020 linarudi kwa wenye jimbo lao πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Bado twasafiri, bado kitambo kidogo!
 
Swali tata kwani TLP au Nccr mageuzi na Cuf zimekufa si bado watu wanasubiri sana zife
 
Halafu mnasema Magu kabana democracy?
Magu kazuia mikutano?

Ila ukweli ni kwamba hilo jimbo Heche ajiandae tu sababu 2020 linarudi kwa wenye jimbo lao πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Acha upumbavu dogo, kwa hiyo watu ni vichaa wakisema demokrasia imebanwa na mikutano ulizuiwa? Wenye jimbo lao Ni kina nani?
 
Kweli! Bado miezi michache jimbo lirudi home, action itaonekana kwenye hizi chaguzi ndogo! πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ni kweli, kwakuwa rais kashaagiza jimbo liende ccm maana sasa hivi box la kura sio linalotoa kura, bali rais ndio anapanga.
 
Acha upumbavu dogo, kwa hiyo watu ni vichaa wakisema demokrasia imebanwa na mikutano ulizuiwa? Wenye jimbo lao Ni kina nani?
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Democracy ipi imebanwa wakati mnaachiwa mikutano hivyo mumtukane Rais mtakavyo? Huo mkutano Heche alikua anamwaga matusi tu kama choo cha stendi
 
Ni kweli, kwakuwa rais kashaagiza jimbo liende ccm maana sasa hivi box la kura sio linalotoa kura, bali rais ndio anapanga.
Kwa hiyo huyo Heche alipitishwa na CCM 2015? πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Mnachekeshaga sana kusema CCM inashinda kwa kuiba kura wakati huyo anaesema ni mbunge wa upinzani yupo bungeni anakula posho za bure kama Nassari
 
Halafu mnasema Magu kabana democracy?
Magu kazuia mikutano?

Ila ukweli ni kwamba hilo jimbo Heche ajiandae tu sababu 2020 linarudi kwa wenye jimbo lao πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
Uzur hata yeye anajua halambi Jimbo...
 
Back
Top Bottom