Anaandika Dr. Levy kuhusu mabadiliko ya vifurushi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
Ushakuwa legend Naseeb... Usiishi maisha ya kisiasa ambayo yanafanya issues za kitaifa uside upande mmoja zinapojitokeza. Issue ambazo kimsingi zinaumiza watu wengi. Nigga simama, ongea, kemea, shauri, lalamika... Acha utoto wa kukaa kimya.

Sehemu kubwa ya mawe unayoingiza ni kwa njia ya mtandao. Internet ndo kila kitu. Bila mtandao wa internet dogo ungekuwa nothing dunia hii. Serikali imevagaa na kuingiza watu chaka la simba kwenye issue za Bando. Wewe kama haupo vile.

Suala la bei za bando limewagusa watu wote nchi hii. Don't take it easy bro.... Ongea. Sema. Onesha kukatika stimu. Mamilioni ya watu wako wote huko mitandaoni ni kwa sababu ya bando la internet. Hushituki kama wanataka kukufilisi kwa kukutenganisha na watazamaji wa ngoma zako huko you tube?

Unasubiri wengine tuseme, kisha tukose ushikaji na VIONGOZI wa taifa hili. Halafu wewe ukae kimya ili uonekane uko nao vizuri. Wakupende. Wakati UKWELI ni kwamba sisi tunalalamika kwa NIABA yako? Maana sisi tunalilia bando la kuchat whatsApp na kuitia pisi kali viwanjani na chatting za groups. Ila wewe internet kwako ni utajiri wa kutisha.

Ajabu @faustine_ndugulile kazingua wewe umekaa kimya. Na pengine umempongeza kimya kimya kabisa. Next time hao hao wakiona walalamikaji tuna hoja na wakabadilisha hayo maamuzi yao ya kijinga, wewe ndo utakuwa wa kwanza kuwapongeza na kuwasifu kama watu wanaojali watu wenyonge.

Vinega wa Ant Virus, walichangia sana bei za malipo ya shoo Bongo zipande. Wenye akili wanajua. Ila ninyi hamtaki kukiri wala kutoa salute. But siyo kesi hata hiki kinachowagusa watu wako wa Tandale huko. Ambao kimsingi ndo waathirika zaidi kwa kutoona swaga zako insta. Wewe umekausha kama vile haya makitu hayakuhusu.

Kukaa kimya ni usnitch kinoma. Ufala pia. Maana kesho mtakuja mitandao kuwaambia watu wazame kwenye #biozenu watazame video mpya. Watatazama kwa makalio?

Ongea dogo, washua wanazingua issues za bando. Kwa sababu internet ndo maisha ya sanaa na wasanii kwa sasa. Wapo wengi. Lakini wewe una nguvu ya mashabiki na unasikilizwa na viongozi. Do that!



Dr. Levy


168503714_10223179636217060_2142476281559819443_n.jpg
 
Nadhani kila mtu ajisemee mwenyewe kuliko kumsubiri mtu aseme kwa niaba yako
Hujui unachokisema, kuna watu maarufu kama hao akina Mondi wana mawasiliano ya karibu sana na hao wakubwa. Wewe mnyonge na hohehahe huna hata namba ya Waziri... Unaanzia wapi?
 
Nadhani kila mtu ajisemee mwenyewe kuliko kumsubiri mtu aseme kwa niaba yako
Ni kweli kabisa kwa nini awe naseeb pekee na sio mwakilishi wake bungeni inakuwa kama personal wakati mwingine yaani mibaba mizima ya kila sector inayotegemea internet tutegemee Nasaeeb kwani nternet ni kwa ajili ya social media pekee vyuoni makampuni ya kibiashara je wao kimya tu mawazo ya kufikiri internet ni kwa ajili ya social media yawafanya viongozi wasiojua umuhimu wa hii sector kuibuka na mambo ya hovyo huku nchi nyingine internet imekuwa sehemu ya haki za binadamu .. ni kweli kila mtu aseme
 
Hujui unachokisema, kuna watu maarufu kama hao akina Mondi wana mawasiliano ya karibu sana na hao wakubwa. Wewe mnyonge na hohehahe huna hata namba ya Waziri... Unaanzia wapi?
Mondi hana ubavu wa kupambana na hizo kampuni ambazo hata wanasiasa wanaziogopa isitoshe ndo wanamuweka mjini au umesahau makampuni hayo ya mawasiliano ndo wadhamini wakubwa wa matamasha ya mengi ya wanamuziki vipi kuhusu matangazo redioni ? kwa mwenye akili za kibiashara huchagua wapi aseme hakuna anayenyea sehemu anayo kula chakula labda kichaaa
 
Bahati nzuri huko insta misipajui hata kunafananaje, kuna jamaa yangu nae analalakika sana kua insta inammalizia sana Mb cha ajabu muda wote hakauki huko...
insta na jamii forums kwangu ndo zinanimalizia bundle hata wasanii wengi kwasasa wapo active zaidi na Insta, kwakweli facebook siielewi hata kidogo yaani kwangu huo muda wa kuingia Facebook ni bora nizame Kupatana.com niangalie bidhaa zinazouzwa naweza pata cha kununua.
 
Back
Top Bottom