Ana viungo vya uzazi vinne, na sehemu mbili za haja kubwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,806
Mtoto wa ajabu amezaliwa akiwa na viungo
vinne vya uzazi vya kiume, sehemu za
kutolea haja kubwa mbili moja ikiwa
mgongoni pamoja na mguu mkubwa wenye
vidole sita ambao nao umeota kati kati ya
mgongo.
Mtoto huyo ambaye mzazi wake Naishooki
(23), anatoka kijiji cha Injok, Wilayani
Arumeru, mkoani Arusha, alizaliwa juzi usiku
kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya
Olturumet.
Akizungumza huku akilia kwa uchungu,
mama mzazi wa binti aliyejifungua mtoto,
Naishiye Logolie, alisema hawajawahi kuona
kitu cha ajabu na kutisha kama yaliyotokea
kwa mtoto wao.
“Mwanangu alipokuwa mjamzito hajawahi
kuonyesha dalili za tatizo lolote.
Tumechachanganyikiwa kuona kitu kama
hiki. Tunaomba madaktari watusaidie kujua
ni nini hiki. Ni huzuni kwa jamii yangu,”
alisema Mama Logolie katika wodi namba
mbili alikolazwa mama wa kichanga hicho.
Alisema mtoto wake alianza kupata
uchungu juzi na walipompeleka katika kituo
cha afya karibu na nyumbani kwao,
walishangaa kupewa rufaa kwenda
Olturumet, ambapo walipofika mdaktari
walimwambia ni lazima afanyiwe upasuaji
haraka kumwokoa mtoto na mama pia.
Aidha, alisema baada ya mwanaye
kupelekwa chumba cha upasuaji, walianza
kusali kuombea upasuaji huo uwe salama,
lakini baada ya upasuaji waliitwa na daktari
na kuambiwa kuwa mzazi yuko salama
isipokuwa kuna tatizo kwa mtoto.
“Kwa haraka hatukudhani ni kile ambacho
kimetokea tulifikiri labda mtoto amechoka
sana au ana tatizo la kiafya ambalo
lingekuwa la kawaida, baada ya kuona
maumbile yake nilizimia, sikuamini na hata
sasa siamini mwanangu kazaa mtoto wa
aina hii,” alisema Naishiye.
Mganga wa Halmashauri ya Arusha, Dk.
Thobias Mkina, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa wanajaribu
kufanya linalowezekana kuokoa maisha ya
mtoto huyo ambaye hajaweza kunyonya
maziwa ya mama yake tangu azaliwe juzi
usiku.
“Matukio ya kuzaliwa watoto wakiwa na
matatizo yanatokea, lakini hili kidogo
linaonekana kuwa la kipekee sana kutokana
na maumbile ya mtoto,” alisema Dk. Mkina.
Alisema sababu za kitaalamu zinazoweza
kusababisha matukio ya aina hii ni matumizi
ya dawa zenye kemikali na wakati mwingine
kuna matukio ya kurithi kutoka kwa kizazi
cha muhusika.
Hata hivyo, alisema uchunguzi unaendelea
na wakimaliza watampatia rufaa kwenda
katika hospitali kubwa zaidi.
Baada ya taarifa za kuzaliwa kwa mtoto
huyo, watu wamekuwa wakifurika katika
familia ya mwanamke huyo kujua
kilichotokea huku wengine wakisafiri kwa
mwendo wa kilomita zaidi ya 20 kufika
katika hospitali hiyo kumwona mtoto huyo.
Kuzaliwa kwa mtoto huyo mwenye uzito wa
kilo nne, kunatokea siku chache baada ya
tukio la ajabu kutokea katika siku za
karibuni mkoani Arusha la kondoo aliyezaa
kondoo mwenye kichwa cha binadamu
katika eneo la Kiserian, Wilayani Arumeru.
CHANZO: NIPASHE
 
Tanzania bado tuko nyuma sana. Pamoja na majigambo kila kukicha ya madaktari 'BINGWA' bado tunaona mtoto kuzaliwa na viungo kama hivi ni 'ajabu'? Nilitegemea mmoja wa hao madaktari 'bingwa' aeleze (in medical terms) nini kilitokea hadi mtoto huyo akawa na viungo vya ziada.

Gazeti la Nipashe nalo ni mazezeta kabisa, wameshindwa kupata maelezo ya kitaalam ili waandike vitu vinavyosaidia jamii? Huu uandishi wa ki-jima utaendelea mpaka lini? Kwa nini wasimpigie specialist wa 'reproductive health' awaeleze kabla ya kuandika huu upuuzi? Yes, ni mara chache kwa mtoto kuzaliwa na viungo vya ziada lakini haya mambo yanaelezeka, na kama magezeti yanajidai kuwa wanaelimisha jamii basi Nipashe wanaeneza ujinga.
 
kila kukicha tunasikia jambo jipya.........inasikitisha kweli...........ukiona unajifungua salama na mtoto mzima jambo la kumshukuru Muumba wako
 
Mungu wangu. Tumezidi kumkosea mungu, hiyo ni miujiza ya mungu.
 
Umemaliza! Muacheni mungu aitwe mungu. Ni vitu vya kisayansi na vinaelezeka ila unajiuliza 'why me???'
kila kukicha tunasikia jambo jipya.........inasikitisha kweli...........ukiona unajifungua salama na mtoto mzima jambo la kumshukuru Muumba wako
 
Huwa sinunui magazeti ya Nipashe au IPP kwa ujumla yamekaa kiudaku sana, wakati wote huwa wanabase na unilateral information. Utakumbuka hata habari ya kupasua kichwa na mguu ilivumishwa wanachukua info kutoka kwa relative pekee bila kuhusisha wataalam husika waliofanya hilo kosa. Media za bongo zimekaa kishabiki zaidi yaani kishakunaku. Hata juzi kati walizusha ooh madaktari wamesahau mkasi tumboni mwa mgonjwa kumbe uongo kisa walichukua taarifa kwa ndugu pekee, kumbe mgonjwa mwenyewe alikuwa na uvimbe mkubwa ambao haukuweza kutolewa. Pia alikuwa HIV positive . Waandishi wa habari wajitahidi kuanzia habari zinazohusisha pande zote mbili hasa mahali penye utata. Nawatakia kazi njema wanaJF
 
Tanzania bado tuko nyuma sana. Pamoja na majigambo kila kukicha ya madaktari 'BINGWA' bado tunaona mtoto kuzaliwa na viungo kama hivi ni 'ajabu'? Nilitegemea mmoja wa hao madaktari 'bingwa' aeleze (in medical terms) nini kilitokea hadi mtoto huyo akawa na viungo vya ziada.

Gazeti la Nipashe nalo ni mazezeta kabisa, wameshindwa kupata maelezo ya kitaalam ili waandike vitu vinavyosaidia jamii? Huu uandishi wa ki-jima utaendelea mpaka lini? Kwa nini wasimpigie specialist wa 'reproductive health' awaeleze kabla ya kuandika huu upuuzi? Yes, ni mara chache kwa mtoto kuzaliwa na viungo vya ziada lakini haya mambo yanaelezeka, na kama magezeti yanajidai kuwa wanaelimisha jamii basi Nipashe wanaeneza ujinga.

Kama nipashe ni mazezete hizi habari tungezipataje?
 
Back
Top Bottom