Ana siku ya 75 tangu ajifungue ila haoni siku zake; je ni kawaida?

Hehe nacheka kama mazuri.

Mkuu, kutokuona sikubwakayi ananyonyesha ni kawaida.

Ila usipokua makini mkeo atabeba mimba wakati mtoto wa sasa ana miezi sita au mitatu tu.

Sio mtabiri ila tunaongelea mambo yapo kwenye jamii haitakuwa case ya kwanza.

Anza sasa mkakati wa kuavoid mimba hata kama jaoni siku zake.
Sawa chifu!

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Ujue mimi ni mtupu sana kwenye haya mambo... maswala ya uzazi nilikuwa sielewi kabisa maana shuleni enzi hizo points za kukariri nakumbuka KUNYONYESHA MUDA MREFU ilikuwa ni moja ya NJIA ZA ASILI ZA UZAZI WA MPANGO

Hapohapo nikawa naendelea kusikia tena ishu za kubemenda watoto, kuzaa bila mpangilio na nikashuhudia kabisa mtu amepata mimba huku bado ananyonyesha

Lakini leo nashukuru akina mzizi mkavu na the like wamenichambulia vizuri maswala haya kwamba kumbe siyo kunyonyesha muda mrefu tu bali na kwa utaratibu unaofaa pia kikamilifu

Kuhusu hilo la kutokuingia kwenye siku zake kwakweli sikuwa nikijua lolote ndo nimejifunza humu, asanteni.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom