Ana Mke lakini nina Mtoto wake, Naomba ufafanuzi juu ya jambo hili kisheria

Jkosewe

Member
Feb 22, 2020
32
125
Habari wanaJF,

Naomba ufafanuzi juu ya sheria hii

Mimi ni binti ambaye nipo kwenye mahusiano na mwanaume ambaye alishaoa toka mwaka 2015 kwa ndoa ya kikristo na toka nipo naye kwenye mahusiano tuna mwaka 1 na miezi 2
Na kipindi chote hicho tulikuwa tunaishi kama wapenzi na wanajamii walimfahamu kuwa ni mume wangu pamoja na baadhi ya ndugu. Mwaka jana nikafanikiwa kupata ujauzito japo mke wake hana uwezo wa kupata ujauzito kwa muda huo wote.

- Je kisheria mimi nitajulikana kama nani?

- Je nitakuwa na uwezo wa kudai haki yangu pamoja na mtoto?

- Pia naomba ushauri juu ya hili swala maana mke wake hafahamu hili swala?


Sent using Jamii Forums mobile app
 

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,606
2,000
Kwa nini wanawake huwa wanajipa asilimia kubwa kwamba mwanaume atawahi kufa kabla yake?
 

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
12,390
2,000
Huna haki yoyote,sana sana kuendelea naye ni wewe kujizibia riziki za kuja kupata mume wako,cha kufanya ni umuombe tu awe anatoa huduma kwa mtoto;

Kwa mazoea mnaweza kuendelea kuchapana tu lakini haina uhalali wowote wa wewe kuja kudai ndoa au fidia.
 

Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,764
2,000
Jkosewe, 1. Wewe ni kimada.

2. Huna haki yoyote katika mali za jamaa.

3. Mtoto pia hana haki kama ulivyo wewe (isipokuwa kama baba atatamka).

4. Swali, je kuna uthibitisho wa daktari kuwa mke wa jamaa hatazaa milele?

5. Ushauri: Tafuta vyako na mwanao, mwombe jamaa akusaidie kwa namna atakavyoweza.

Kumbuka: haki ya mke katika ndoa haiondolewi kwasababu ya 'kimada' kuzaa mtoto. Mtoto ni matokeo ya ndoa, na ndoa ni hiari ya wanandoa. Wanaweza kuendelea kuishi pamoja hata kama hawana mtoto.

Naamini kwa kifupi umeeelewa. Kwa ziada onana na mwanasheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

John Mwalingo

Member
Apr 29, 2020
11
45
Kwa lugha nyepesi unatambulika Kama marafiki tu wa kimapenzi, ila haki za mtoto lazima uzipate kama Chakula, Malazi, Elimu na haki zingine nyingi anazo stahili mtoto kuzipata.

Pili tukirudi kwa Ndoa ya rafiki yako wa kiume na mke wake kwake yeye atakuwa na haki zote anazo stahili katika ndoa yake ikiwa ni pamoja na haki ya mgao wa mali zilizo tokana na chumo la pamoja, na haki zingine zote atazipata Kama ambavyo Sheria ya ndoa ya mwama 1971 inavyo eleza kuhusu haki za wanandoa.

Note....!!!

Katika ndoa mtoto si kigezo cha kukwamisha mwanandoa asipate haki zake katika mali zilizo tokana na chumo la pamoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
3,294
2,000
Kwa jinsi unavyosema eti mwaka jana ukafanikiwa kupata ujauzito maana yake ni kitu ulikuwa unakitafuta kwa jamaa, umejilengesha. Hii ni mbaya sana, wewe unajijua ni mchepuko na jamaa ana mke we unajibebesha limimba. Na hakika ndani ya akili yako ukawaza kwa kuwa mkewe hajazaa basi tayari kwa wewe kuzaa na jamaa umejihalalisha na bila haya unauliza eti haki zako.

Dada pole sana, cha kukushauri ongea na jamaa na ushuke chini aamue tu kumtunza mtoto ila si wewe. Siku jamaa akiamka vibaya anarudi kwa mkewe anakuacha kama hakujui. UMEKOSEA SANA KUZAA NA MUME WA MTU!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Concomitant

Member
Sep 17, 2018
12
45
Kisheria huna haki yoyote kwa kuwa wewe si mke wa ndoa. Kijamii tunakuona kuwa mwizi wa waume za watu.

But you need to celebrate kwa kuwa umepata mtoto mlee na mtunze mwanao huyo ndiye ndugu yako.

Kama umri wako bado nakushauri achana na huyo mwanamme haraka sana kabla mkewe hajafahamu tafuta na naamini utampata mme wako wako. Muombe huyo mzazi mwenzio msaidiane kulea mwanenu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom