Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Ameomba aulizwe maswali ajibu, sasa ninyi mmekomaa na 'misuto'. Wakati mwingine tumuulize kwa staha, huenda kuna mamho anataka kuyatolea ufafanuzi. Sidhani kwa staili hii ya mashambulizi anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri kujibu.
Lakini pia tutambue kuwa siasa ni mabadiliko. Hakuna aliyedhani leo Simbachawene atakuwa hapo alipo. Haitoshangaza kuona Mwigulu, Nape na wengine wa aina yao wakirejea kwenye Baraza.

Hoja yako ni nini hapa Manyerere? Kuna misuto ya hapa na pale hilo ni kweli, lakini kuna maswali ya msingi anayakwepa wazi wazi.

Sasa unapotaka kuleta utetezi wako lazima ujue pia kuna maswali ya msingi anayakwepa. Kuna mdau amemwambia kama baadhi ya maswali anaona atapoteza ulaji, atumie ile id yake fake kutoa mwanga.
 
Kaka bwana Blaza, naomba kama utaguswa na roho utoleee ufafanuzi ile video clip uliyokuwa uko porini na jeshi la CCM....

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Mauwaji mengi yalitokea chini yako, hili unalizungumziaje??

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Kwanini hujawahi kwenda kumjulia hali ndugu yako/yetu Tundu Lissu? Wewe kama kweli ni Mkristo safi utakumbuka maandiko haya, DINI SAFI NI HII KUTAZAMA WAGONJWA NA KUSAIDIA YATIMA.....Wewe ulishindwa kwenda, au hata kumpa pole tu! Bado unajiita mkristo??

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Je, umewahi kujutia like tukio la zile maiti za kwenye viroba wakati ule wa kupotea kwa ben saanane , ulipo kataa zisifanyiwe uchunguzi kwakuwa uliamini ni zakigeni?

Je, nini manufaa ya kuwa waziri tofauti na kuwa mbunge katika swala maslahi binafsi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwigulu Mchemba,

..wewe ulikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati Mh.Tundu Lissu anashambuliwa.

..Je, ni nani aliondoa walinzi wa area D kuanzia lango kuu mpaka wanaolinda nyumba moja moja za viongozi mfano kwa Naibu Spika?

..Kwanini uliruhusu jeshi la Polisi na wasemaji wake kupotosha kwamba upelelezi hauwezi kufanyika bila kumhusisha dereva au Tundu Lissu mwenyewe?

..Kwanini wizara yako na jeshi la Polisi ulillokuwa ukilisimamia halikuomba ushirikiano na serikali na Polisi wa Kenya na Ubelgiji ili dereva na Tundu Lissu wahojiwe na kuchukuliwa maelezo?

..Suala la kushirikisha vyombo vya nje linahitaji ushirikiano wa AG, na Wizara ya Mambo ya Nje, lakini wewe kama Waziri wa Mambo ya Ndani ndiye uliyetakiwa u-initiate maombi hayo.

..Ni miaka zaidi ya miwili tangu Tundu Lissu ashambuliwe. Looking back unadhani ni jambo gani ungelifanya tofauti in response kwa shambulizi lile?
 
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ukiwa kama msomi wa uchumi na mtanzania uliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali Tanzania,unazungumziaje uchumi wa nchi yetu katika awamu hii ya tano,kitaifa na kwa mtu mmoja mmoja(kwa maoni yako)?
 
Hivi mshahara wa mbunge ni kiasi gani?
Mshahara wa waziri ni kiasi gani?
Mtu akihamia CCM analipwa kiasi gani?
(Unaweza kunijibu kwa Ile ID yako feki)


Hahahaha ...mkuu unanikumbusha kwenye ile nyimbo ya prof Jay ya kikao cha dharura
Babu Ayoub alivyomuuliza prof kuhusu mabomba kutoa maziwa nchi nzima
Prof alivyomjibu naomba muulize maswali ya kiutu uzima...Watanzania mmekuja kuuliza maswali au mmekuja kunikomoa.

Ila huyu bwana MADELU alijisahau sana wakati alivyokuwa kwenye nyadhifa za juu za kiuongozi.
 
Halafu mods wamefuta maswali yangu yote.

Jamii forum mkoje Nyie? Jukwaa la hovyo kabisa kwa Sasa.

Narudia Tena Wewe mwigulu siku nikiwa na mamlaka nakubuluza ICC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bavarian8

Hatujawahi kukataa uwepo wa tume huru ya uchaguzi. Hata kwenye katiba mpya ilikuwa agenda. Wenezetu walikataa. Agenda ya tume huru ni pana

Hapo haukuwa mkweli. Unaosema wenzenu walikataa ni akina nani hasa?? Mliokubali mlifanya nini kuhusu jambo hili ukizingatia mlikuwa wengi zaidi??

Au unaowaita wenzenu ni wale waliosema katiba mpya sio kipaumbele cha sasa na hakikuwa kwenye manifesto??

Hata sijui kwanini kuna utamaduni wa kulaumu mwingine!! Wakati mwingine ni taabu kuamini anaye-reason ni PhD holder. Iko wapi “philosophy” katika majibu unayotoa katika post zako leo? Shame!! Brother “content” katika majibu yako ni za chini sana.
 
Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
Mkuu member mwenzetu wa JF, Mhe. Mwigulu Nchemba
  1. Kwanza nikupongeze kujitokeza tena humu na kukubali kuulizwa maswali, maana mtu wa calbre yako kurejea humu in person na kukubali kujibu maswali, you really have guts!, na labda ujio wako utawarudisha baadhi ya members wetu humu wa calibre yako ambao humu hawachangii tena akiwemo Nape, Ngeleja, Dr. Kigwa, Makonda, na wengine
  2. Pili nikupongeze jinsi unavyojibu karibu kila swali, na pia kwa yale maswali ambayo majibu yake sio for public consuption, umewakaribisha waulizaji at personal level.
  3. Pia nakupongeza kwa uvumilivu wako na ustahimilifu wa kuyavumilia baadhi ya maswali kiukweli ni ya kijinga!. Hapa nawaomba members wenzangu wa jf, kumpata mtu kama huyu kujibu maswali yetu humu ni heshima kubwa kwa mtandao wetu huu wa jf, tumuulize maswali ya maana, kiheshima na kistaarabu ili kuonyesha jf ni mtandao wa watu mature, responsible na wenye objectivity, hiki sio kijiwe, hivyo tuache maswali ya vijiweni.
  4. Mimi nakiri kukukubali sana tangu ulipotaka kugombea urais ile 2015 Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa!
Na baada ya maelezo hayo, mimi ni mwandishi wa habari za uchunguzi, IJ, nina maswali madogo 5 yanayohusu utata wa majina yako, ambayo yanahitaji majibu mafupi mafupi tuu ili yasikuchukulie muda mrefu
  1. Ulizaliwa lini, wapi, na ulipozaliwa ulipewa majina matatu yapi?
  2. Ulianza shule lini, shule gani, iko wapi, na uliandikishwa kwa majina matatu yapi?
  3. Ulipokatisha shule kwa ajili ya kuchunga mbuzi, ulikatizia lini, ukiwa darasa la ngapi na ulikatizia shule kwa majina gani?.
  4. Ulichunga mbuzi kwa muda gani, na uliporejea tena shule, ulirejea lini, shule gani, na ulirejea darasa la ngapi na kwa majina gani?.
  5. Ulimaliza shule darasa la saba lini, shule gani, mwaka gani na ulimaliza kwa majina matatu yapi?.
NB. kama jina la shule ni hiyo hiyo, kwenye jina la shule jibu only once.
Natanguliza shukrani na hongera kwa uteuzi tena.
P.
 
Mh. Nchemba umefanya vyema kuja mwenyewe katka jukwaa hili, ili upate kujumuika na hata kuchangia na wanajukwaa mambo mbalimbali, hasa yale yanalolihusu jimbo lako la uchaguzi la huko Iramba. Lakini kwa kuwa lengo la uzi wako ni kutaka watu wapate ufafanuzi kutoka kwako kuhusu masuala mbalimbali, basi ni lazima yajitokeze mambo ambayo yaliumiza sana watu ktk kipindi ambacho wewe ulikuwa ni kiongozi mwenye dhamana ktk wizara nyeti ya mambo ya ndani.

Kwa hiyo basi, ni vyema ukawa "specific" ktk uzi wako, ili kama ulikuwa na maana ya kujadiliana kwa hoja mambo yale tu yenye kulihusu jimbo lako na wala si vinginevyo. La hasha, sehemu kubwa ya mjadala itahusu watu kutishwa, kushambuliwa na kuumizwa, kutekwa na hata kuuwawa huku wewe ukiwa ni kiongozi mwenye dhamana umekaa kimya kana kwamba hakuna jambo lolote lile baya limetokea.

Kama hiyo haitoshi, huwezi kukwepa baadhi ya maswali kwa kisingizio cha kiapo, labda pengine ungekuja na hoja ya uchaguzi bado unaendelea ama athari ya kauli zako zingeweza kuwa za kisheria zaidi. Unaweza kutoa hoja ya jumla tu hata watu wakakuelewa hukuwa sehemu ya genge la wahalifu ama pengine unajutia yale yote yaliyokuwa yakitokea hali wewe ukiwa ndiye waziri mwenye dhamana.

Tumewaona viongozi wengi watokapo katika dhamana za uongozi wao, huwa "remorseful" na hata hujitokeza mbele ya jamii na kutoa neno lenye kufariji wahanga wa yale yote mabaya yaliyofanyika ktk utawala wao. Kuwa muungwana na kufanana nao, na utoe neno moja hata wengi wetu tukapate kujua unayajutia mambo hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu M.N,
(a)Mbali na uvaaji wa skafu, tunawezaje kuhamasisha, kujenga na kuimarisha hisia za uzalendo nchini, hususani miongoni mwa vijana?Tofauti za kiitikadi na kifalsafa zinaweza kukwaza mchakato huo?
(b) Nini imani yako juu ya hali ya elimu katika jimbo la Iramba Magharibi na nchini kwa ujumla?Elimu imeimarika au imedhoofu, kulinganisha na mwaka 2015?

(c) Baadhi ya wanaharakati wa haki za kiraia na binadamu wanaamini ujauzito haupaswi kuwa sababu ya kuua ndoto za kielimu za watoto wa kike. Kuipa nguvu hoja yao, wanaharakati hao, wanatumia ilani ya uchaguzi ya CCM, ya mwaka 2015, uk.95 kipengele I (i,), (ii) & (iii).Tunaweza kupata mtazamo wako juu ya hili?

(d) Katika nafasi yako kama mjumbe wa Kamati ya Ushauri mkoa wa Singida, unafikiri kulikuwa na haja ya kweli ya kuwa na Wilaya na Halmashauri ya Mkalama?Kwa nini, badala yake, isingeimarishwa wilaya na Halmashauri ya Iramba ili kuokoa fedha? Kama ilikuwepo haja ya wilaya na Halmashauri mpya, Mkalama ilikuwa ni chaguo sahihi kijiografia?

Baada ya maswali hayo, nikutakie kila la heri katika harakati zako za kuwakilisha wananchi wa Iramba Magharibi.
 
Ndio maana nawambia tafuteni TAARIFA kabla ya kuandika. Mtafute Nondo umuulize nimemfanyia kitu kibaya au kitu chema. Abdul Nondo SI NI MEMBER HAPA, NA AJE ASEME NIMEMFANYIA KITU CHEMA AU KIBAYA
Uliwaaminisha Watanzania kwamba Nondo ali jiteka. Na siku mna mpata alikuwa kajipaka Perfume
Mwigulu ukiwa mwongo uwe na kumbu kumbu maana hii uliongelea bungeni.. Mungu ana kuona. Na nita washangaa sana Wana Iramba wakikupa kura zaidi ya za familia yako. Kama CCM ita kupitisha anyway!! Yaani ndugu yako ana pigwa risasi kama nyumbu hata pole ya uongo kwa sms???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameomba aulizwe maswali ajibu, sasa ninyi mmekomaa na 'misuto'. Wakati mwingine tumuulize kwa staha, huenda kuna mamho anataka kuyatolea ufafanuzi. Sidhani kwa staili hii ya mashambulizi anaweza kuwa kwenye nafasi nzuri kujibu.

Lakini pia tutambue kuwa siasa ni mabadiliko. Hakuna aliyedhani leo Simbachawene atakuwa hapo alipo. Haitoshangaza kuona Mwigulu, Nape na wengine wa aina yao wakirejea kwenye Baraza.
Manyerere
Hashambuliwi anaulizwa facts..
Halafu nimekumbuka
Hebu tupe uelewa wako kuhusu yale mabomu ya Soweto Arusha. Nakumbuka wewe ulikuwa jirani sana na mkutano wa Chadema pale Soweto wewe ulikuwa njia ya Ilboru ukiwa una hutubia kikao cha familia wakati Chadema walikuwa na umati wa kutisha. Ina semekana wewe ndie ulikuwa nyuma ya lile tukio...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom