Ana hali mbaya baada ya kujitahiri mwenyewe kwa wembe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Jamaa mwenye umri wa miaka 40 amelazwa katika hospitali ya Tharaka- Nithi nchini Kenya akiwa katika hali mbaya baada ya kujitahiri kwa wembe.

Katheya Riungu alijitahiri usiku wa Ijumaa, Januari 11 nyumbani kwake katika kijiji cha Mutunguni.

Habari kutoka kwa polisi zinaeleza kuwa wenyeji waliripoti kisa hicho kituoni jioni ya Jumapili Januari 13,2019 baada ya jamaa huyo kuvuja damu usiku kucha.

Riungu alichukua hatua hiyo baada ya kupata fununu kuwa rafiki zake walikuwa wamepanga kuthibitisha kama kweli ametahiriwa.

Kulingana na taarifa iliyondikishwa katika kituo cha polisi cha Chogoria, Riungu alipata fununu kuwa rafiki zake walikuwa wamepanga kuthibitisha kama kweli ametahiriwa.

Kwa kuogopa fedheha, aliamua kujitahiri kabla ya njama hiyo kutekelezwa.

"Walikuwa wamepanga tarahe ya kuthibitisha lakini Jumapili Januari 13, alikuwa amejitahiri kwa wembe na alikuwa akivuja damu,’’ ripoti hiyo.

Riungu alikimbizwa hadi katika hospitali ya ya rufaa ya Chuka anakoendelea na matibabu.


Malunde 1 blog
 
How sad.

Hao sio marafiki. Friends don't do that to each other.
 
Dah jamaa ndani ya miaka 40 alikuwa bado actor wa kihindi,i mean Govindah?sema kama ni jaluo mikono ya sweta ndiyo zao.
 
Back
Top Bottom