Ana GPA ya 2.6 Degree anataka kusoma Masters. Je, inawezekana?

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,926
Mwenye kujua kama inawezekana kusoma Degree ya pili (Masters) kwa mwenye GPA ya 2.6.

Na kama inawezekana utaratibu upoje? Na je huyu mtu mwenye GPA ya 2.6 anaweza kupata Scholarship?

Karibuni wajuzi wa mambo
 
Alafu unaweza kukuta mwenye hii GPA ni mwanaume kabisa
 
Atatakiwa asome Postgraduate Diploma kwanza kwa muda wa miezi 12, akishafaulu ndipo atakua na sifa stahiki ya kujiunga na Masters Degree. Kila la kheri.
 
Mbona unambeza? Wewe ulipata first class? Ulisoma kozi gani? Au ndio uko semester 1?
Nilimaliza kitambo mkuu.
BSc. Sio education.

Kwenye kile chuo kisichopendwa na wengi alafu sikupata Gentleman degree.

Kwenye taaluma nashukuru Mungu niko njema tatizo sijapata hela tu
 
Nilimaliza kitambo mkuu.
BSc. Sio education.

Kwenye kile chuo kisichopendwa na wengi alafu sikupata Gentleman degree.

Kwenye taaluma nashukuru Mungu niko njema tatizo sijapata hela tu
Utakuaje njema kwenye taaluma kisha ushindwe kupata hela? Uliielewa vyema hiyo taaluma yako? Au ulisoma kitu usichokipenda kwa kufuata mkumbo na umaarufu wa hicho kitu? Unakwama wapi na taaluma yako njema?
 
Alafu unaweza kukuta mwenye hii GPA ni mwanaume kabisa
Kwani GPA unaipata kwa kuwa na nguvu/msuri. Iyo kitu inapatikana kutokana na uwezo wa kukumbuka na nidhamu ya shule. Kuna Watu wengi wameingia chuo na matokeo ya A level mwaka wa kwanza semista ya Kwanzaa tuuu, mtu kafukuzwa
 
Kutoka UDSM

Entry Qualifications
An honours degree or its equivalent from a recognized institution of higher learning. Candidates who hold an unclassified degree (e.g., M.D.) should have at least a B grade average in the subject of the intended Masters study.

Kipengele kinachokuhusu

Candidates with pass degrees may also be considered for admission if:
(i) Their undergraduate performance in the proposed subject of study was a B grade or higher.

(ii) They have satisfied the relevant College/School/Institute with their academic potential through subsequent research experience and/or additional training.
Candidates with a coursework average of B+ (GPA 4.0) or higher in specified Postgraduate Diplomas may upgrade to registration for a dissertation leading to a Masters Degree. Candidate with Professional qualifications such as, ACCA, CPA, CIM, CSP, CMA, etc. may also be considered.
Only candidates with GPA 3.5 or above in their first degrees are considered for masters by thesis.
 
Utakuaje njema kwenye taaluma kisha ushindwe kupata hela? Uliielewa vyema hiyo taaluma yako? Au ulisoma kitu usichokipenda kwa kufuata mkumbo na umaarufu wa hicho kitu? Unakwama wapi na taaluma yako njema?
Acha kuongea mashudu.
Hela na taaluma ni mambo mawili tofauti labda kama mwalimu wako wa chekechea hukumuelewa vizuri.

Bakhresa ana taaluma gani?
Nikisema taaluma namaanisha makaratasi yangu ya vyeti na hela nilizonazo haviendani, sasa kuna ajabu gani hapo?
 
Kwani GPA unaipata kwa kuwa na nguvu/msuri. Iyo kitu inapatikana kutokana na uwezo wa kukumbuka na nidhamu ya shule. Kuna Watu wengi wameingia chuo na matokeo ya A level mwaka wa kwanza semista ya Kwanzaa tuuu, mtu kafukuzwa
Mwanaume lazima ukomae upate matokeo mazuri hiyo nido kawaida.
After all don't take it too serious nilikua natania tu ndio maana nikaweka emoji mwishoni
 
Back
Top Bottom