An Organization Should Be Designed to Live Longer Than Its Employee

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Nakumbuka katika mchakato wa kuelimika, kwenye topic ya Organization Design, Dkt. Ngirwa alieleza kwa ufasaha sana kuhusu umuhimu wa kuunda muundo wa taasisi ambao unauwezo wa kujiendesha wenyewe bila kujali nani yuko katika uongozi (An Organization Should Be Designed to Live Longer Than Its Employee). Lakini mara nyingi Watumishi na hasa wa Serikali tumekuwa tukijisahau sana wakati tunapokuwa kwenye nyadhifa zinazotuwezesha kufanya maamuzi ya kuweka miundo ya utumishi ambayo itakuwa na tija kwa mtu yeyote bila kujali anawadhifa au hadhi gani. Kwa mfano tuje kwenye suala la uborehsaji mishahara. Wapo watumishi wa serikali ambao hukwamisha ongezeko la mshahara kwa sababu tu yeye katika nafasi aliyopo kuna marupurupu mengi ambayo yanakuja kwa njia ya OC. Siku anapostaafu marupurupu hayo yanaondoka na kazi yake na yeye anabakia kuilaumu serikali kwa maslahi duni ya pesheni na kusahau kwamba wakati fulani yeye alikuwa ndo hiyohiyo serikali anayoilaumu.

Nimekutana na habari ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya akilalama kwamba alikwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukaa masaa kibao pasipo kupatiwa huduma. Nukuu ya sehemu ya kauli yake ni hii hapa;

Alisema katika kuhangaika alifika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini cha kushangaza alikaa kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni bila kuhudumiwa.

“Ndipo mtu mmoja anayenifahamu aliyekuwa akipita nilipoketi, akanisalimia kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina ninalihifadhi akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana siwezi kupata huduma hadi niwe mheshimiwa, nikaondoka kwa hasira," alisema.

Habari nzima unaweza kuipata kwenye kiunganishi hapa chini.

DC wa zamani hoi kitandani


Wakati huyu Mheshimiwa akishangaa hali hiyo leo, kwa mwananchi wa kawaida hiyo ni hali ambayo iko siku nyingi na naamini kuna uwezekano alishapelekewa malalamiko ya huduma mbovu wakati uheshimiwa wake ukiwa active.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom