Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,583
Nimewapata... Nyani na Zomba... tuna uwezo gani wa kuichunguza kampuni ya Kimarekani kwa kutumia sheria zetu? Tunaweza kumleta Balali bila ya msaada wa Marekani? Fedha zetu zilizokwapuliwa kama zimewekezwa Marekani tutazipata vipi bila kuwahusisha Marekani? Nakubaliana na nyinyi kuwa kuna mambo ambayo tunaweza kuyafanya sisi wenyewe, lakini ni hiki kiburi chetu ndicho kimetufikisha hapa tukidhania kuwa watawala wetu wataamua kufanya mambo kwa maslahi ya Taifa letu. Kama wangetaka hivyo wangefanya hivyo siku nyingi zilizopita.
Hiyo Richmond ni wabongo wenyewe ndio walioingia mkataba nayo huku wakijua fika kuwa ina exist kwenye briefcase tu/ au haidili na mambo iliyodaiwa inadili nayo. Hapo tatizo ni la nani?
Balali: hivi status yake ktk serikali ya Tanzania ni ipi? Fugitive from justice or..? Has he even been indicted? If not, who's fault is it and what is the TZ Govt. waiting for?
Fedha zilizokwapuliwa: zimekwapuliwa na nani na yuko/ wako wapi hao waliozikwapua? Kama wako Tanzania, je ni nini kinachoendelea? Sisi kama taifa tumefanya nini kuwashughulikia?
Mwisho: hatuna kiburi na si kiburi chetu kilichotufikisha hapa tulipo!! Ujinga wetu ndio uliotufikisha hapa tulipo. Tunaachia mifisadi iendelee kufuja mali zetu na kutanua halafu tunaendelea kuiweka madarakani miaka nenda rudi. We have way too much tolerance for nonsense. Watanzania tuko wengi mno kuwa "pimped" na mifisadi michache. Hivi tunashindwa nini sisi kuwafanyia kweli hawa mafisadi? Mi nadhani tuna uoga wa asili that we need to overcome first in order to earnestly deal with our problems. Marekani na nchi zingine zitaweza kusaidia kwa dhati pale tu tutakapoanza kujisaidia wenyewe.