AN OPEN LETTER to BAE Systems: Do not return radar money to Tz Government

Nimemsoma mama Claire Short tena (as I did over four years ago) na nimejikuta nasikitika:

Anasema:

It is easy to say that we should cut off aid if there is corruption, but there are many poor and hungry people in Tanzania. The aid is for them. Someone else stole the money, but if we punish the poor for that we are punishing the wrong people. What should we do? That is the dilemma and that is why we need to tighten up our systems.

President Mkapa and I reached the agreement that if he promised that there would be no second half to the project, we would go ahead with increasing our aid. I saw him after he had ceased to be President, and he told me that he had kept the promise, so although that makes the system even more useless—because it covers only part of the country—at least no more money was wasted.

Say Whaaaaat?
 
ninachoona hapa tukijioganize vizuri kwa kupitia jf tunaweza hata kumg'oa jk pale..........naona ni possible kabisa

hii inawezekana kabisa maana kwa sasa viongozi hawana macho wala mapua ya kunusa kinacho endelea na kutusumbua wananchi
kwa mfano bunge live kabisa waziri mkuu anatete poshi
kuna mwingine anasema mtanzania awezi kushindwa kupata chai
hawa jamaa bwana sijui anaongelea chai ya maji matupu au niini?
 
Jamani nimevamia mjadala huu, yawezekana kuna mtu kisha andika.
Hivi kweli inawezekana kuwaomba BAE wasilipe fedha hizo serikali yetu against court order! Na kwa nini isiwe malalamishi haya yapelekwe ktk mahakama au kupitia vyombo vya sheria kuwakilisha malalamiko kama representative!
Nawasiliasha!
 
serikali ndio waende mahakamani kama wanaona wameonewa
lakini sijui huko watamwakilisha nani maana wananchi hawana imani na serikali hasa hii ya sasa
 
Nimemsoma mama Claire Short tena (as I did over four years ago) na nimejikuta nasikitika:

Anasema:

Say Whaaaaat?
Heee ndio westerners hao, hii ndio lugha yao lakini ajabu ni kwamba kwa maneno hayo hayo na sababu hizo hizo, hawakufikiria hivyo kwa kina Mugabe, Gadhaffi na Saadam.
 
serikali ndio waende mahakamani kama wanaona wameonewa
lakini sijui huko watamwakilisha nani maana wananchi hawana imani na serikali hasa hii ya sasa
Maana yangu ni kwamba sidhani kama BAE wanauwezo wa kutolipa ikiwa mahakama tayari imewaarisha waturudishie fedha zilizozidi. Sasa tunapowaomba BAE sijui wao watatumia kifungu gani cha sheria kutolipa unless haya malalamiko yapatiwe lawyer ambaye atawakilisha hoja hii mahakamani kisha pengine serikali au mahakama ya UK wanaweza kusimamisha maamuzi ya awali.
 
Iweje tunaacha mwizi wa ndani na kuanza na yule aliyeko nje tena mbali? Tuuwe nyoka aliyepo kitandani kisha tunahangaika na nge aliyeko nje tena mbali? Tutakuwa wageni wa nani pale tutakaporudi kwa furaha kutoka kuua nge na kukuta nyoka kajaa tele kitandani tena amezaa watoto hapo.
Serikali ya Wengereza imeona uchi wetu na inayo kila sababu ya kutupangia wapi pa kujisaidia hata kama mbele ya hadhara!! tumejitakia wenyewe kwa ujuha wetu hasa ulafi wa viongozi wetu.
Binafsi nitakuwa wa mwisho kuipongeza serikali kwa juhudi za kutaka kurejeshewa pesa hizo ilhali waliotufikisha hapo wangalipo wanadunda kifua mbele miongoni mwa hao wanaopiga kelele kutaka fedha zirudishwe. Japo si mweledi wa masuala ya kidiplomasia na kanuni zake nadhani huko mbele Waingereza watauliza maswali magumu kwa niaba yetu wengine japo nalo linahitaji subira kujua senema itaishia wapi. Senema ni nyingi nchi hii na tuangalie!!
 
Maana yangu ni kwamba sidhani kama BAE wanauwezo wa kutolipa ikiwa mahakama tayari imewaarisha waturudishie fedha zilizozidi. Sasa tunapowaomba BAE sijui wao watatumia kifungu gani cha sheria kutolipa unless haya malalamiko yapatiwe lawyer ambaye atawakilisha hoja hii mahakamani kisha pengine serikali au mahakama ya UK wanaweza kusimamisha maamuzi ya awali.

Serikali ya Tanzaia haiwezi kufanya kitu zaidi ya kutegema huruma tu . Wakijaribu kutumia sheria wataumbuliwa. K kuna ukweli mwingi hwananchi hawajaucjua bado. BAE wangeweza kuwalipa Tanzania kama serikali ingeonyesha nia ya kuwashugulikia wale waliohusika.
 
Nimemsoma mama Claire Short tena (as I did over four years ago) na nimejikuta nasikitika:

Anasema:

It is easy to say that we should cut off aid if there is corruption, but there are many poor and hungry people in Tanzania. The aid is for them. Someone else stole the money, but if we punish the poor for that we are punishing the wrong people. What should we do? That is the dilemma and that is why we need to tighten up our systems.

President Mkapa and I reached the agreement that if he promised that there would be no second half to the project, we would go ahead with increasing our aid. I saw him after he had ceased to be President, and he told me that he had kept the promise, so although that makes the system even more useless—because it covers only part of the country—at least no more money was wasted.

Say Whaaaaat?

Kumbe kulikuwa na 2nd phase kwenye hiyo project. Au ukanumba wangu sielewi
 
Mimi hata sielewi kwa nini hawa jamaa wanakuwa na uroho hivi . Membe anataka tuandamane tukatae pesa hiyo kupitia kwa mashirika hayo ? Kweli jamaa hajatuli huyu .
 
Jamani nimevamia mjadala huu, yawezekana kuna mtu kisha andika.
Hivi kweli inawezekana kuwaomba BAE wasilipe fedha hizo serikali yetu against court order! Na kwa nini isiwe malalamishi haya yapelekwe ktk mahakama au kupitia vyombo vya sheria kuwakilisha malalamiko kama representative!
Nawasiliasha!

Mkuu wangu, mahakama haikutoa amri ya kurudisha hizi fedha kwenda kwa serikali ya Tanzania. Uamuzi wa kurudisha fedha ulikuja kama sehemu ya makubaliano tu kati ya BAE na SFO. Kwamba, kama SFO itaacha kuchunguza BAE na kumshtaki mtu yeyote wa BAE kutokana kesi hiyo ya rada basi BAE itatoa (siyo kurudisha) fedha kiasi cha Paundi milioni 29.2 - 500,000 (ambayo ni fines). Sasa makubaliano yale yalisema wazi kuwa fedha itarudisha "ex gratia" ambayo imetafsiriwa katika kiingereza "as charitable" na ikamalizia "for the benefit of the people of Tanzania". Hayo ndio maneno ya makubaliano.

SFO hawakutaka fedha zirudishwe kwa serikali ya Tanzania; kiongozi mmoja wa US DoJ alisema wazi kabisa kuwa kurudisha fedha hizo kwa serikali ya TAnzania itakuwa ni sawa na kufanya kile kile kilichotokea mwanzo! Ni kutokana na hili ndio serikali yetu imekasirika - kwamba haiaminiwi. Tukumbuke kuwa serikali inachofanya sasa ni kubembeleza tu fedha ipewe yenyewe lakini haina msingi wa kudai hivyo. BAE na timu waliyoiweka ndio wanauamuzi wa mwisho wa fedha hiyo kama hisani iletwe vipi Tanzania.
 
Mimi nimetuma. Jamani tuungane saa ya ukombozi imewadia - we have nothing to lose except our chains
 
nimesoma comment nying na nimeona niseme haya. Barua hi n nzur na n vema 2kaisapoti kwa ku2ma hzo email, kuhusu court order uksoma barua h vzur utagundua kuwa mahakama imeoda BAE kurudsha pesa lakn sio kuilpa serikal so by interpretation BAE Bado wanaoptn ya kuchoose jns gan warudshe hyo fedha na dat y nasema 2isapot.
 
Mie naona hawa BAE na viongozi wa Serikali ya Bongo wote walikwiba pesa ya walipakodi wa Tanzania, sasa tunapompelekea kesi yetu huyu BAE tutegemee kupata nini? au labda mwizi akiwa mzungu anaweza kuaminiwa kuliko mswahili?
 
Hansard 30 January 2007
Sale of Radar System (Tanzania) [30 Jan 2007]
30 Jan 2007 : I made the decision to cut back our promised a
id by £10 million and went to see
President Mkapa-a man I greatly respect and who did a good job by his country. He
told me that the contract had been signed
before he came to office, a deposit had been
paid and there was a penalty clause if Tanzania did not go ahead.

ina maana hii kitu ni dhambi ya mwinyi pia au hapo kwenye bold sijaelewa
namba ufafanuzi kabla sijapiga mishale kwa kukurupuka
mimi siku zote najua ili kitu katuletea chinga hapa naona kama napata nuru mpya vile
nani alikuwa jeshi na wamasiliano wakati huo wa mwinyi?
 
M. Mwanakijiji,
Shukran nimeelewa, kwa hiyo unafikiri BAE wanaweza kupindua?.

tatizo la BAE ni kuwa hawataki kuonekana wanawapa fedha serikali. Jaji aliyesikiliiza kesi hii alisema kuwa "the real victims in this case are the Tanzanian people" hakusema "the Tanzanian government". Hata kina Lamb na Short hawakusimama kutetea kuwa serikali imeumizwa. Na ndio sababu ya kutaka kutoa hizi fedha kuwafaa Watanzania. Ndio maana kwa mfano serikali ikitaka inaweza kuchagua miradi ya kufadhiliwa na BAE wakaamua kufadhili miradi hiyo moja kwa moja bila kuzipeleka fedha hizo kwa serikali ya Tanzania. Tatizo ni kuwa serikali inataka ijifanye ndio "victim"..
 
wewe unaona ni sawa nchi yetu kupangiwa matumizi ya hela na serikali ya nje?????
Huna habari kwamba NGO zimekuwa vichaka vya kuiba hela zinazotolewa na wafadhili?
Mimi pia naunga mkono fedha hizo zisirejeshwe kwenye mikono ya serikali fisadi hii ambapo kila kiongozi ana bei yake ya kununuliwa kwa njia ya rushwa. Hebu tukumbushane, tulitambiwa kwamba eti ile pesa ya EPA iliyokwapuliwa BOT ilirejeshwa, lakini mkaguzi mkuu waserikali ameapa kutoziona hata harufu yake kote serikalini; wanaotetea vibaka hawa wakabidhiwe pesa hiyo wanaweza kusema ile ya EPA waliiweka wapi?
Fedha hii ya rada iliibiwa na vibaka wa kimataifa wakisaidiwa na vibaka hawahawa wa CCM wanaosemekana kutumana kwenda Uingereza kuidai irejeshwe mikononi mwao! Kuna mtu anayeweza kuwaamini wezi hawa ambao muda aote walikuwa bize kufunikafunika ushahidi ili kesi hii isifanikiwe?
NGO ni vichaka vya wizi wa fedha za wahisani? sina uhakika lakini ni heri ziibiwe na NGO's hizo maana tunaweza tukapambana nazo Mahakamani kuliko ziliwe na vibaka hawa waliojiwekea wigo wasihojiwe wala kushtakiwa milele hata kama kwa vitendo vyao watakuwa wamesababisha mateso na vifo kwa miongo kadhaa ijayo!!
 
Back
Top Bottom