Amuua Mtoto Wake Kwa Hasira za Marekani Kufungwa na Ghana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amuua Mtoto Wake Kwa Hasira za Marekani Kufungwa na Ghana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 1, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Hector Castro Wednesday, June 30, 2010 12:52 AM
  Mwanaume mmoja nchini Marekani anashikiliwa na polisi baada ya kumpiga mpaka kumuua mtoto wake aliyekuwa akilia sana wakati yeye akiangalia mechi ya kombe la dunia kati ya Marekani na Ghana ambayo Marekani ilifungwa 2-1 na kuliaga kombe la dunia. Hector Castro mwenye umri wa miaka 28 alimpiga sana na kisha kumuua kwa kumziba pumzi mtoto wake wa kambo wa kike mwenye umri wa miaka miwili.

  Baada ya kumuua mtoto huyo ili kuficha ukweli, Castro aliididimiza bisibisi kwenye shingo ya mtoto huyo ili kufanya kifo cha mtoto huyo kionekane kuwa ni cha ajali.

  Castro aliita ambulansi akidai mtoto wake amepata ajali wakati akicheza na bisibisi imezama kwenye shingo yake.

  Hata hivyo mchezo wake uligundulika muda mfupi baada ya madaktari waliokuja na ambulansi kugundua kuwa mtoto huyo alifariki kutokana kupigwa na kuvunjwa mbavu kadhaa na wala si bisibisi.

  Castro alitiwa mbaroni kwa tukio hilo lililotokea jumamosi wakati wa mechi ya kuwania kuingia robo fainali kati ya Marekani na Ghana.

  Castro alijitetea kuwa alishikwa na hasira kutokana na mtoto huyo kulia sana bila kunyamaza wakati yeye akiangalia mechi hiyo ya Marekani na Ghana ambayo iliisha kwa Marekani kufungwa mabao 2-1.

  Kutokana na umri mdogo wa mtoto aliyeuliwa, Castro huenda akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.

  Chanzo NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  ama kweli wazungu Bwana ni Mashetani kweli kweli kazi ipo hapo.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  oooh nimekosa hata la kuongea ..mmh hatari
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160

  I wish ningekuwa jaji wa kuhukumu kesi hiyo, ningemcharaza viboko 36 kabla ya state punishment. What a stupid man
   
Loading...