Amuua Mke na mwanaye kisa wivu wa mapenzi

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,206
4,698
Muleba. Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Joachim Rwegasira mkazi wa kijiji cha Bushanga Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera kwa tuhuma za kumuua mkewe, Rosemary na mwanaye, Joiness na kisha kujijeruhi.

Rwegasira anapatiwa matibabu hospitali ya Wilaya ya Muleba Rubya akiwa chini ya ulinzi wa polisi ikielezwa kuwa wivu wa mapenzi ndio chanzo cha mauaji hayo.

Akizungumza leo Jumamosi Aprili 17, 2021 Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Maketi Msangi amesema tukio hilo limetokea jana Ijumaa Aprili 16, 2021 baada ya Rwegasira kumtuhumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na jirani yao

Amesema siku ya tukio mtuhumiwa alianza kumshambulia mkewe akimtuhumu kuwa na uhusiano na jirani yao na walibarikiwa mtoto ambaye ni Joiness.

Amedai kuwa baada ya kufanya kitendo hicho, mtuhumiwa huyo alijijeruhi na kitu chenye ncha kali tumboni na shingoni na sasa anapatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Rushonge, Vedasto Mpaka amesema hakuwahi kupokea malalamiko yoyote ya wawili hao na siku ya tukio alikwenda kwa mtuhumiwa na kumkuta akiwa na majeraha huku kando yake kukiwa na miili miwili.

MCL
 
Mtoto asiye na hatia yoyote ile, amekua mhanga namba moja wa makosa ya wazazi wake!

So sad. 😡
 
Back
Top Bottom