Amuua baba mzazi, amzika chapchap | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amuua baba mzazi, amzika chapchap

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 1, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jeshi la Polisi mkoani Kagera, linamsaka Kaiza Richard (22), kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi na kumzika chapchap baada ya kumkataza kuuza shamba la urithi alilomrithisha.

  Polisi walisema inasadikiwa katika mauaji hayo, Richard alikuwa na mwenzake ambaye jina lake halijafahamika.
  Aliyeuawa ni Richard Raphael (55), mkazi wa kitongoji cha Kigusha kijiji cha Buguruka, Kata ya Maruku tarafa Kyamutwara, Wilaya ya Bukoba Vijijini.

  Habari kutoka kwa majirani zilisema mtoto huyo alikasirishwa na kitendo cha baba yake kumzuia kuuza shamba alilomrithisha huko Izimbya.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Hennry Salewi, alisema uchunguzi wa mauaji hayo ya kikatili ulibainisha kuwa chanzo cha ugomvi ni baba kumzuia mwanae asiuze shamba hilo ambalo alimpa.

  Alisema kijana huyo alitaka kuuza shamba hilo alilorithishwa na mzazi wake ili akanunue pikipiki, jambo ambalo marehemu hakuliafiki.
  Kamanda Salewi alisema kuwa mauaji hayo yalitokea Mei 23, na mtoto Alinda Joachim (10) aliyekuwa anamuita marehemu mjomba aliwakuta watuhumiwa nyumbani hapo wakichimba shimo.

  Mtoto huyo alisema alikuwa amerudi majira ya saa tatu kudai fedha ya uji shuleni, ndipo alipomkuta Kaiza pamoja na mwenzake ambaye hakuweza kumtambua, wakiwa wanachimba shimo kando ya nyumba ya marehemu.

  Ilielezwa kuwa mtoto huyo Alinda aliwafuata na kuwauliza wanachimba nini na walimjibu kuwa wanachimba choo na Kaiza alimtuma Alinda aende kwa Mohammed Seleman mkazi wa kijiji hicho ili akamchukulie redio yake.

  Alinda kabla ya kutekeleza maelekezo hayo alipita ndani ya nyumba na kuanza kumuita mjomba wake.
  Alinda alishtuka baada ya kumuona mjomba wake akiwa amelazwa chumbani kwake bila kuitika, ndipo alipokimbilia kule alikotumwa na kutoa taarifa ya mambo aliyoyaona.

  Baada ya taarifa hiyo, Mohammed pamoja na majirani zake walifika haraka na kuwakuta wauaji wakitaka kutokomea huku wakiwa na baiskeli ya marehemu na begi la nguo zao.

  Salewi alisema baada ya wauaji hao kuona Alinda anafika na wanakijiji walishtuka na kufanikiwa kukimbilia kusikojulikana na ndipo majirani walianza kuchunguza alipo marehemu na kubaini kuwa kafukiwa katika shimo.

  Alisema baada ya kumfukia, walitandaza majani ya migomba juu ya shimo hilo.
  Alisema wananchi walitoa taarifa katika kituo cha polisi Bukoba na Jeshi la Polisi lilianza utaratibu wa kuomba kibali cha mahakama ili kufukua shimo lililokuwa likidaiwa kuwemo mwili wa marehemu, Mei 25, mwaka huu shimo hilo lilifukuliwa na kutoa mwili wa marehemu na kubaini marehemu aliuawa kwa kuchinjwa.

  Mwili wa marehemu ulizikwa baada ya kufanyiwa uchunguzi na Jeshi la Polisi, watuhumiwa hao wanaendelea kusakwa na polisi.
   
 2. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pikipiki aliyoitaka ataikosa,
  Baba atamkosa!
  Maisha uraiani atayakosa!
  Kila kitu kitaishia pasipotarajiwa!.
   
 3. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,576
  Likes Received: 12,860
  Trophy Points: 280
  Doomsday is realy near now munguwangu watu wanachinjana km kuku,why sasa huyo hilo shamba ataliuzaje tena .ishakula kwake
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Unamchinja baba?kweli huyo dogo kichwani kutakua kuna matatizo
   
 5. okonkwo jr

  okonkwo jr JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2016
  Joined: Jun 14, 2015
  Messages: 2,427
  Likes Received: 1,466
  Trophy Points: 280
  Dah better to have no kids
   
Loading...