Amua sasa, acha tabia ya kustarehe na vijana na kuolewa unaenda kuolewa na wazee

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
UJUMBE MAKINI KABISA KWA WANAWAKE USIKOSE KUSOMA TAFADHALI ASEE

ACHA KULALAMIKA DADA MAHESABU UMEKOSEA MWENYEWE.

Msichana ana miaka 22, anafuatwa na mvulana na kuambiwa kwamba anataka kuolewa, mvulana yupo kamili kajiandaa na anamaanisha, msichana anakataa kwa visingizio vya kipumbavu mvulana anaachana nae.

Anachokifanya ni kumfuata mvulana ambaye hana mpango wa kumuoa kisa gari kisa fedha anataka kuitwa mpenzi na mambo kuishia kitandani anavuliwa pichu.Haiishii hapo anapofika miaka 23, 24, 25, 26 hali inakuwa hivyo hivyo kwake anajiona hana haja ya kuolewa anaamua kuwa na mpenzi tu, leo huyu kesho huyu na keshokutwa yule.

Siku hazimsubiri miaka 27, 28, 29 na 30 inaingia hapo ndipo anashtuka kwamba kapoteza muda na anatakiwa kuolewa.Hahaha! Mungu sio chizi aliyajua maisha yako ya mbele ndio akakuletea wanaume mbalimbali wa kutaka kukuoa lakini ukakataa kwasababu zisizo na mantiki.

Mwenyewe unaona muda wa wewe kuolewa umefika lakini hauolewi unaanza kuangaika huku na kule kila mwanaume kwako anaonekana kuwa muhimu. Yaani wakati ambao haukuuhitaji ndoa, ndoa ilikuhitaji na wakati ambao unaihitaji ndoa wanaume wana-HIT & ku-RUN.

Kwa mahesabu kama una miaka 30 inakupasa kuolewa na mwanaume mwenye angalau miaka 33 au 35. Je kuna mwanaume mwenye umri huo ambaye yupo tayari kuoa? Mwanaume hataki kuitwa babu na mtoto wake anataka kuitwa baba. Mwanaume anapofikisha umri wa miaka 30 anaweka jiko ndani lenye miaka chini ya 25.

Sasa kama kipindi alichokuwa na miaka 30 ukamkataa, wewe ukiwa na miaka 30 mwenzako ana 35 kashaoa kitambo na kama MUNGU kamjalia ana watoto wawili.Sikulazimishi uolewe ila unapopata mwanaume aliye tayari kukuoa kubali tu, ndoa ni bahati kuna wanawake wanafikisha miaka 40 na bado hawajaolewa na kila siku wanatamani kuolewa.

Unapoipata bahati fanya mambo.Siku zote mwanaume anapokwambia kwamba anataka kukuoa ukaleta pozi weeeeee, akija kwa mara ya pili huyo si muoaji, atakuja akuchezee na kukuacha kwani anajua pia we haupo tayari kwa kuwa alishakupa nafasi ukailetea pozi.

WANAWAKE WAPO MILIONI 29 TANZANIA NA WANAUME MILIONI 25. HALAFU WEWE UNALETA POZI.HAYA, TUTAONA MWISHO WAKE.

#Nimemaliza
 
Ujumbe Murua kwa wanawake/mabinti wanaohitaji kuolewa, ila kuna wengine ndoa sio muhimu kwao.

Inapendeza kila mtu mwenye akili timamu aishi maisha yake anayoyaona ni sahihi ilimradi hayana kero kwa wengine.
 
Wanawake wenye akili ya maisha na wengi wao wanajielewa wapo Uganda tu hapo jirani na wanapenda sana wanaume wa kibongo,wa bongo wengi omba omba tu
 
Hivi neno nataka kukuoa bado lina nguvu kweli? Matapeli wa mapendi neno nataka kukuoa ni kawaida Sana! Wanawake wengi ni wahanga wa utapeli wa wanaume kwani wanaume wakweli wako wachache sana na uchumi nao ni jambo muhimu katika ndoa usikubali kuolewa ili kupata sifa tu kuwa umeolewa .Hivi mwanamke asipoolewa ndo kufeli maisha? Kuoa au kutoolewa ni sio jambo geni!
 
Na life halina formula kabisa wako walioolewa wakiwa na 30s na wakawapata wanaume Agemate wao na wana-Enjoy kabisa....So kila mtu ana maisha aliyooandikiwa na lazima ayapitie tu hata akiforce kuolewa akiwa 18yrs hiyo ndoa haitadumu..
 
Back
Top Bottom