Amtia mimba mdogo wa mkewe na kumsababishia umauti

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
10,230
10,798
Nishemeji yake, toka nitoke na mkewe, lakini jamaa alipata ujasiri wa kumtongoza nakutoka nae kinyumba.

Tena chakusikitisha ni mtoto wa miaka 14 tu.

Ilipokuja kugundulika kua mtoto anaujauzito jamaa ikabidi amlazimishe mkewe wamrudishe kwa wazazi wake, kwakua mkewe hakuna anajua kinacho endelea akakubali wazo la mumewe na ukizingatia binti hakua anasoma. Alipofika kwao ndipo ikagundulika kua binti ni mjamzito.

Wazazi walijitahidi kumbana amtaje nani aliemtia ujauzito ule, binti alikataa lakini mwisho wa picha mtoto akamtaja kua ni shemeji yake.

Alipoambiwa dada mtu, ugomvi ukawa mkubwa bainayake na mumuwe jambo lililo sababisha kuvunjika kwa ndoa yao na mwanamke kurudi kwa wazazi wake.

Mimba ilipo kua tayari imetia mudawake tayari wazazi walimpeleka Hospital, ndipo binti wawatu alipo poteza maisha, sababu hakuwa na uwezo wa kuzaa inasemekana njia yake ya uzazi ilikua ndogo sana. Mungu amuweke mahala pema binti yule na amlaani jamaa yule.

Naiwe fundisho kwa sisi mababa tunaopenda kuwafanya watoto wadogo tena bila kuzingatia ni nani ktk família zetu.

Nanyinyi akina mama munaopenda kuchukua wadogo / watoto wenu waliokua tayari washaiva kuwapeleka mulipo olewa.

Mwisho kabisa, DUNIA NI TAMU ILA TUOIHARIBU NISISI WENYEWE WANADAMU.
 
Niogope kuchukua ndugu zangu waliopevuka,mabint zangu wakipevuka nao nikawafiche wapi?
 
wanaume wanakula popote haijalishi ni hotel ama mgahawani hat nyumbani huwa hawachagui
 
Niogope kuchukua ndugu zangu waliopevuka,mabint zangu wakipevuka nao nikawafiche wapi?

ndo hapo sasa...huyu jamaa kaja kututisha hapa, husimsikilize we leta ndugu zako wote wa kike nyumban
 
Miaka kumi na nne yumkini Jamaa lilikuwa linambaka huyo mtoto...
 
Imefika hali ya wanaume kuwa kama mamba anatafuna hadi watoto wa nyumbani mwake hali inatisha sana
 
maskini mwanamke kaharibiwa ndoa yake na kumpoteza mdogo wake Inasikitisha sana,sisi wanaume bhana.

Angeitafakari adhabu aliyomchagulia mumewe angegundua kuwa inamuumiza na yeye pia, angeangalia namna nyingine ya kumuadhibu au kumsamehe bure na kupanga kumchukua mtoto wa mdogo wake na kumlea kwenye familia kwa haki na upendo apatao mtoto wa familia.
Au kwa kesi hii mdogo mtu anakua adui? kama anakuwa adui mbona amemfuata huko huko kwa wazazi.
 
Wanaume wengine siui watukanwe kwa tusi gani?? Sasa uadui hautakaa uishe kwa kuwa alisababisha kifo kwa wakwe na mke hawezi kurudi tena!!! Yaani ni laana na walaaniwe wanaume wote wanaotembea na ndugu za mke na wasichana wa kazi maumbani. This is the highest degree of humiliation!!
 
ndo hapo sasa...huyu jamaa kaja kututisha hapa, husimsikilize we leta ndugu zako wote wa kike nyumban
Bahti mbaya Sina mdogo wa kike,ila ningewaruhusu waje kila wanavyojisikia!
Halafu nimuone huyo asiyejua kufunga zipu ya suruali yake!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom