Amsterdam & Partners LLP Retained by Tanzanian Political Prisoner Freeman Mbowe

butron

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,500
2,000
E_zFnKeVUAETbEn
Huyu jamaa mbona anaonekana kama tapeli,ila ni wale ambao mpaka mcgunguze sana.Alafua anaonekana kashawazima.watu wengi ila anatumia kampuni kujiteteaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,520
2,000
Hivi kwa Tundu alishindaga au ndio tuendelee kuwasubiria di hegiπŸ™„
La msingi sio hasa "ushindi" wa kesi moja moja, bali ni kutimua vumbi la kutosha ndani na nje.

Kwa kuwa serikali ya ccm inatumia dola kuwabana wapinzani wasifanye siasa, kumbi za mahakama hazina budi kuwa ndio "viwanja" vya kufanyia siasa. Na katika hilo kuna mafanikio makubwa. Kitendo cha mabalozi wa nje pamoja na maafisa wao kufuatilia kwa karibu kesi ya Mbowe, ni mafanikio makubwa ya mapambano yanayoendelea mitandaoni, mahakamani, na katika nyanja nyingine.

Na kipimo kwamba dozi inafanya kazi, ni jitihada za serikali kuwatisha mabalozi wasihudhurie mahakamani.
Ushiriki wa Amsterdam katika kesi ya Mbowe, pamoja na mengine, ni kupanua uwanja wa mapambano. Nyie si mna mapolisi, majaji wenu? Nyie si mnatumia dola kuiba na kupora?
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,523
2,000
Mzungu ashaona fursa hapo, baada ya kuona Lisu kaishiwa sasa kahamia kwa Mbowe akapige kama alivyopiga za Lisu. Ukosefu wa elimu kwa baadhi ya viongozi wa vyama ndio umesababisha mtu kama Amsterdam apate mwanya wa kupiga hela za wasiokuwa na elimu kiulani.
Inavyoonekana porojo za aina hiyo zinakusaidiaga sana kupata japo lepe la usingizi.
 

MRI

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
258
500

Tunaambiwa kuwa na subra maana.....

"Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi. Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu."


Tuwe na subra, kesi ikishaisha ndio tuseme

Mhubiri 7: 8 - 9​

Hata shetani alitumia Neno la Mungu kumjaribu Yesu.Shetani akasema Ikiwa wewe ni mwana Mungu Jitupe chini maana Imeandikwa ataakuagizia Malaika zake"

Imeandikwa usilitaje bure Jina la Mungu wako .

Amelaaniwa MTU yule anaye mtegemea binadamu kuwa kinga yake Na akimuacha Mungu.
mama D
 

Kwameh

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,547
2,000
Hivi Kibatala anaweza kuruhusiwa kuingia na kutoka Mmarekani kumtetea Marekani ndani ya Mahakama ya Marekani ?

Waafrika sisi ni masokwe tusiojithamini.
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,612
2,000
Jenga hoja, acha matusi ya bei rahisi. Tumia kichwa kufikiri
Mkuu wewe, mimi na wengine tupo humu kwa lengo la kuhabarishana, kufundishana na hata kubishana kwa staha ili mradi hatuvunjiani heshima wala kuaibishana kwa namna yoyote hapa jamii forum. Kutofautiana vyama au itikadi ya vyama au kupishana mawazo isiwe sababu ya mtu kutengeneza chuki dhidi ya mungine, isiwe sababu ya mtu kuanza kumshambulia mungine kwa matusi au kwa maneno yasiofaa ambayo yataleta malumbano ndani ya uzi ulioanzishwa na matokeo yake mada iliyoletwa ionekane haina maana. Ukitaka kujua ni kwann nimeandika hayo matusi unayoita ya reja reja, na ni nani alieanza matusi basi soma post namba #40 kuja chini utaelewa. Pia kuna dada mungine kaanzisha huko juu na mimi nikamjibu kwa style ile ile aliyoanza nayo. Mbona ww umeandika kiustarabu na mimi nimekujibu kistarabu! Ni nani anaeweza kudhalilishwa na akakubali kudhalilika bila sababu?
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
18,806
2,000
Hahhahaha.. Chadema hawajifunzi tu?

Huyu alichangia sana anguko la Lisu kwenye uchaguzi mkuu 2020 leo tena atakuja kumpoteza kabisa Mbowe
 

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
2,420
2,000
Hivi Kibatala anaweza kuruhusiwa kuingia na kutoka Mmarekani kumtetea Marekani ndani ya Mahakama ya Marekani ?

Waafrika sisi ni masokwe tusiojithamini.
Kwanini asiruhusiwe kama kakidhi vigezo vya kua wakimataifa.?.Wako wanasheria wengi tu wakiafrika wamefanya hizo kazi uko nchi za wazungu.ata watanzania wapo.mfano wa karibu ni Nimrod mkono.Jielimishe.
 

MRI

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
258
500
Huyo Amsterdam atapata mimba huku bongo, na ndicho anatafuta mbegu ya kikurya.
Mkuu hata kusoma Kwenye hujui!Hiyo kesi haiko Bongo(Tanzania) Imefunguliwa na MBOWE Kwenye mahakama za kimataifa .Acha kukurupuka muwe mnasoma na kutafakari
 

MRI

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
258
500
Hahhahaha.. Chadema hawajifunzi tu?

Huyu alichangia sana anguko la Lisu kwenye uchaguzi mkuu 2020 leo tena atakuja kumpoteza kabisa Mbowe
Mshitakiwa alikuwa ni Magufuli ,Kabla ya kesi ya Mungu aliamua kutoa hukumu yake ya moja Kwa moja kutokana na matendo yake MAGU
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,746
2,000
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚β­•β­•β­•

Div 0 ya Mwenyekiti, ndio matokeo yake hayo..


Ha haaa haaaaa..!! Hata aje masiha, hii case Mbowe hachomoi, ha haaa
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
18,806
2,000
Mshitakiwa alikuwa ni Magufuli ,Kabla ya kesi ya Mungu aliamua kutoa hukumu yake ya moja Kwa moja kutokana na matendo yake MAGU


Ndio maana watu wanawaona hamna akili!

Baada ya Magu kufariki mambo yenu yamekuwa safi ee?
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
14,512
2,000
Kwa wapambanaji wanaopigania Demokrasia, uhuru na haki kwa kila mtu, pamoja na haki zako, habari ya "kungojea" haipo. Ni ALUTA CONTINUA. Kama ni Neno la Mungu, hata makaburu walitumia, kimakosa, Biblia kuhalalisha ubaradhuli wao
Huwezi linganisha wanaonunuliwa na lowasa na wapigania haki
Chadema waliwauza watanzania na kuwanajisi wapinzani wote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom