Amri ya Rais yapuuzwa waziwazi bila aibu

Stanboy

JF-Expert Member
Jul 4, 2013
1,115
1,300
Habari watanzania wenzangu?
Kwa wale wa Dar es salaam,poleni na hali ya hewa hii ya baridi na mvua za mara kwa mara.

Ni takribani wiki mbili kama sikosei toka Rais wa Jamhuri ya Muungano alipotoa agizo kuwa gharama za vifurushi zishuke na zirudi kama ilivyokuwa awali,cha ajabu mitandao ya simu imefanya mabadiliko kidogo sana ambayo haijafika kile kiwango cha awali.Hivi mitandao ya simu ndo imepuuza kauli ya Rais ya kuwa ishushe gharama zake za vifurushi?Hivi ni kweli wasaidizi wa Rais hawajaona hili ili kumsaidia Rais kufanya maamuzi mengine kwa haya makampuni ambayo yanampuuza Rais wazi wazi bila aibu...

Ikumbukwe kuwa kila mtu anatumia kujiungq vifurushi hivi...na kila mtu alisikia kauli ya Rais..sasa mnatuaminisha nini watanzania wanyonge sisi?

Chonde chonde makampuni ya simu msitake kumchokoza Rais wetu mpendwa akawafanyia maamuzi magumu..turudishieni vifurushi vya awali ama lah mseme kuwa hakutakuwa na mabadiliko ili tuzoee tu kuwa wanyonge tunaendelea kunyongwa na mabeberu.

Nawasilisha,
Au mnasemeaje watanzania wenzangu?
 
Angekua anko magu vingeshuka


Kuna watu walisema ni mtaalam wa kutengeneza tatizi na kulitatua fasta
 
Labda hawajapata notice, kwani vifurushi kupandishwa ilikuwa kisheria?
 
Back
Top Bottom