Amri ya Makore mkuu wa wilaya ya Ubungo Sumaye akamatwe imeishia wapi?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,256
2,000
Wana JF

Huyu mkuu wa wilaya ya Ubungo Mkuu Kisare Makori alipotoa amri kwamba Sumaye akamatwe kwa kukiuka taratibu za kutembelea miradi, nilisema humu ndani kwamba Kisare hajitambui kwa kuwa huwezi kum-arrest mtu kwa kukiuka taratibu - kama hakuna uvunjaji amani. Taratibu sio sheria, na kutokana na mazingira fulani zinaweza kutofuatwa bila kuwa kosa kisheria.

Hata nilisema kwamba kitendo cha kumtia ndani Meya wa Ubungo "kwa kukiuka taratibu" ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria, kwa kuwa, kuhusiana na taratibu, Meya ana "discretionary power" za kutofuata taratibu za eneo lake, ili mradi havunji amani wala "sheria". Hata nilidokeza kwamba huyu Meya anaweza kumshitaki Makori kwa kumdharirisha. Sue the pants off him ili wakuu wengine wa wilaya wajifunze kuacha kukurupuka.

Nilisema mtu anaweza kukamatwa kwa kukiuka taratibu, pale tu ambapo ukiukaji huo wa taratibu unaondoa uwepo wa amani. Na kwa hiyo kitendo cha Sumaye kukiuka taratibu bila kuvunja amani, hakiwezi kuhalalisha yeye kuamriwa akamatwe baada ya kitendo cha kutembelea miradi kuwa kimefanyika. Utamshitaki kwa kosa gani, sheria ipi? Au utatumia tu ubabe-CCM kumweka ndani?

Kwa mfano, ni utaratibu uliopo kwamba raisi anapokwenda mahali anasindikizwa na polisi eskoti. Lakini kuna wakati Mkapa alichukua gari tinted na kuendesha mwenye mitaani. Je alivunja sheria? Kuna utaratibu wa kumuona mkuu wa wilaya kuwakilisha malalamiko. Lakini naweza nikakutana naye kwenye kilabu cha pombe za kienyeji nikaongea naye juu ya hayo matatizo. Nitastahili kuwa arrested kwa kutofuata taratibu za kumuona mkuu wa wilaya na kumweleza matatizo yangu?

Hata nilisema kinachotakiwa pale ambapo kuna uwezekano wa kutofuata taratibu, ni kushauri au kumzuia yule anayetarajia kutofuata taratibu asivunje taratibu. Huwezi kum-arrest kama ilivyokuwa kwa Meya - kabla hata hizo taratibu hazijavunjwa.

Kwa hiyo nikasema kitendo cha mkuu wa wilaya Makori kilikuwa kimejaa ukihiyo wa sheria, na ni ushahidi mwingine mkubwa kwamba CCM ipo kwa ajili ya kuhujumu na kunyanyasa vyama vya upinzani, huku watu kama wakuu wa wilaya wakifanya kazi kwa kujipendekeza kwa Magufuli.

Lakini je, Makore alimkamata Sumaye kama alivyotamba?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom