Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,785
Huyu jamaa mimi nampinga pamoja na kupigiwa debe sana na baadhi ya watu hapa jamvini kwamba ni mtendaji mzuri na anafaa kuwa Rais 2015. Kauli yake hii kuhusu kuwalipa mafao yao wale ambao nyumba zao zitabomolewa kwa kweli ilinishangaza sana, "Kama nyumba yako imeingia nusu ndani ya eneo la barabara, itabomolewa hiyo nusu na wewe utalipwa kulingana na ulivyobomolewa, hatuwezi kulipa gharama ya nyumba nzima wakati umebomolewa nusu," alisisitiza.
Hivi nyumba ikishabomolewa nusu kuna nyumba tena hapo wandugu? au ndiyo kuwaacha walala hoi katika hali ngumu zaidi kimaisha baada ya kulipwa mafao ambayo hawawezi kufanya nayo chochote katika kujipatia makazi mapya hasa tukitilia gharama kubwa za ujenzi wa nyumba nchini.
Kaka kumbuka hata kulipwa hiyo nusu ni favour!! hawakutakiwa kulipwa kabisa!!