Amri ya Magufuli yatekelezwa, jengo la TANROADS labomolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amri ya Magufuli yatekelezwa, jengo la TANROADS labomolewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nickname, Feb 5, 2011.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Tumejionea kwenye taarifa ya habari ya ITV kuwa serikali imeamua kubomoa jengo la meneja wa TANROADS mkoa wa dsm lililopo ubungo kwa kuwa liko kwenye hifadhi ya barabara.

  Sasa jengo la TANESCO nalo litabomolewa;amri ya Waziri Magufuli itailetea hasara kubwa serikali kwa kuwa majengo mengi yatabomolewa.
  Je, sheria itekelezwe au isitekelezwe ili tuepuke hasara?
   
 2. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sheria ni msumeno,itekelezwe. Wananchi wengi walio pembezoni mwa hifadhi za barabara wameathirika na sheria hii. Vivyo hivyo inatakiwa kwa majengo ya serikali na mashirika mbalimbali.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,065
  Likes Received: 3,993
  Trophy Points: 280
  hilo jengo la tanesco haliwezi kuwa na gharama na umuhimu mkubwa zaidi ya barabara inayopita! kwa hiyo kama kula nyundo na liliwe nyundo!
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  hii yote ni kutengeneza 'news' ili kuondoa attention ya watu kwenye mauaji na ukatili wa polisi, rushwa, dowans, nk.
   
 5. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Need we say more....
   
 6. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Huwa wapo kipindi haya majengo yanaanza kujengwa from foundation mpka mwisho!! ajabu ya hii serikali likikamilika wanakuja kubomoa!! jengo kama la Tanesco likibomolewa ni mimi na wewe tunabeba mzigo!!

  SIPINGI kubomoa ila naona wakati tunabomoa afisa wa mipango miji alieto kibali cha ujenzi waoote wawe magereza wanajutia maamuzi yao yasiyo ya kitaalamu lakini kwa hili li nchi SIONI HILO!!
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sheria ni msumeno mkubwa!!!
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kwani TANESCO ilijengwa before or after the expansion of Morogoro road (1990s).

  Wao tanroads ndiyo wanaosimamia hii sheria halafu wao ndiyo wavunjaji nambari moja! serves them right.
   
 9. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  sheria lazima iheshimiwe, hao walioruhusu hilo jengo lijengwe ndio waliovunja sheria.
   
 10. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Pale wanajenga kituo cha mabasi yaendayo kasi na siyo hifadhi ya brbr.
   
 11. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Pamoja na sheria lakini pi busara inatakiwa itumike,hela iliyotumika kujenga hiyo ofisi na kuibomoa si ya magufuli bali yetu sote ,huko ni kufuja fedha ,na kuhusu jengo la Tanesco hilo pia limejengwa kwa pesa zetu wote,kama kubomoa basi wabome afisi za wakala wa uchimbaji visima na mabwawa kwani majengo yao ni ya kizamani na yana thamani ndogo kulinganisha na jengo la Tanesco,na kwa kuwa huyo wakala wa uchimbaji visima atakuwa hana ofisi iwapo atavunjiwa ili kunusuru jengo la Tanesco basi itabidi Tanesco iwape hawa wakala ofisi kwenye jengo lao
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,161
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mbona hiyo ni ndogo, Mbona Tanesco ina hasara kubwa zaidi ya hiyo ukianza na Dowans, IPTL na mengine, Acha wabomoe tu
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,094
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa mimi nampinga pamoja na kupigiwa debe sana na baadhi ya watu hapa jamvini kwamba ni mtendaji mzuri na anafaa kuwa Rais 2015. Kauli yake hii kuhusu kuwalipa mafao yao wale ambao nyumba zao zitabomolewa kwa kweli ilinishangaza sana, "Kama nyumba yako imeingia nusu ndani ya eneo la barabara, itabomolewa hiyo nusu na wewe utalipwa kulingana na ulivyobomolewa, hatuwezi kulipa gharama ya nyumba nzima wakati umebomolewa nusu,” alisisitiza.

  Hivi nyumba ikishabomolewa nusu kuna nyumba tena hapo wandugu? au ndiyo kuwaacha walala hoi katika hali ngumu zaidi kimaisha baada ya kulipwa mafao ambayo hawawezi kufanya nayo chochote katika kujipatia makazi mapya hasa tukitilia gharama kubwa za ujenzi wa nyumba nchini.
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #14
  Feb 5, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Siku zote sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma. Ukiibiwa sheria inakulinda na ukiiba sheria ina kuhukumu. Anachofanya magufuli ndio hasa kinachotumika duniani kote. Jengo kama halikufuata taratibu Bomoa, kama mama Tibaijuka alivyofanya. Hakuna cha jengo la serikali, jengo la mhindi n.k. Kama sheria imevunjwa itumike sheria kuhukumu.Period.

  Hii nchi bado ina watu wa maana!
   
 15. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama wanavyotuonyesha kwa mbwembwe jinsi wanavyobomoa majengo hayo, wahakikishe wanatuonyesha wote waliosababisha uzembe huo wanavyochukuliwa hatua.. Gharama iliyotumika kujenga, itakayotumika kubomoa na kujenga tena ni ya watanzania. Tuna haki ya kuona wazembe hao wakiwajibika.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tuone kama kweli jengo la TANESCO nalo litabomolewa. Ofisi za TANROADS zilikuwa kwenye kiwanja cha TANESCO na walitakiwa kuhama. Ni usanii mtupu huo. Magufuli arudishe nyumba za serikali walizopora ndio tutamuelewa. :msela:
   
 17. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Mda si mrefu JK atabadili mawaziri ili kumdhibiti, CCM hawataki wachapa kazi.
   
 18. lynxeffect22

  lynxeffect22 JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 625
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mimi naunga mkono wabomoe kila jengo lililoingia kwenye hifadhi ya barabara. bila watanzania kubadilika hatuitafika popote. wenzetu wa marekani na ulaya si kwamba wametuzidi sana ila ni kwamba mfumo waliojijengea wa uwajibikani na sheria unafuatwa. mtu akichemsha anawajibika hata ikibidi kuingia jela. kwa hiyo waliohusika wote kuruhusu hayo majengo, mabadiliko wa matumizi ya ardhi wakusanywe na wawekwe keko uone kama kuna mtu atapindisha sheria au ethics za kazi yake
   
 19. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mbona wakati wa kubomoa nyumba za wananchi swali hilo haliulizwi??? Serikali lazima ionyeshe mfano, kwa kuanza kubomoa nyumba zake kwanza. Namuunga mkono Dr. Magufuli (PhD) kwa asilimia mia.
   
 20. m

  mshaurimkuu Member

  #20
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi huwa nashindwa kuelewa watendaji na wasomi wa nchi hii. Jengo kubwa (angalau kwa viwango vya Tz) kama la TANESCO siyo kibanda - siamini kama lilijengwa kwa kukurupuka au kwa siku moja.

  Kuna "wataalam" walikaa mahali wakaandaa andiko (proposal), vikao vikakaa mara nyingi, michakato ikafanyika kwa muda mrefu, wakatafutwa wataalamu washauri wa kila fani - architectural engineers, civil engineers, urban planners, surveyers, electrical engineers, n.k. n.k.

  Taasisi mbalimbali za kiserikali (pengine na binafsi) zikahusishwa - wizara yenyewe (ya nishati), jiji, wizara ya ujenzi (inayohusika na barabara), TRA, n.k. Baada ya mchakato huo mrefu ndipo hatimaye kandarasi (tender) ikatangazwa na michjo kadhaa ikafanyika hatimaye kumpata/kuwapata MAIN CONTRUCTOR, several SUB-CONTRUCTORS katika maeneo mbalimbali - civil, electrical, n.k hawa wakisimamiwa na mtu anayeitwa CONSULTANT ambaye kazi yake kuu ni kuhakikisha kazi inafanyika kwa ubora unaotakiwakwa.

  At the end, tunaambiwa so simply - JENGO LIKO BARABARANI. Hivi wataalamu wote hao hakuna aliyeweza kung'amua hilo mapema? Na kama hawakung'amua, nini kifanyike? Si wamesajiliwa na Bodi ya Wahandisi (and other professional bodies)? Kama waling'amua na kushauri ila serikali (TANESCO) wakawa vichwa ngumu pengine kwa utashi wa kisiasa, hakuna wa kuwajibika? SHAME ON THEM!

  Haiwezekani jengo kama la Tanesco ambalo halina hata miaka nadhani 12 leo tunaambiwa linatakiwa kubomolewa - liko barabarani. Magufuli angekuwa kweli mchapakazi angehoji hayo yote kabla ya kufikia hitimisho la kuvunja. Vinginevyo ni kulea uzembe unaoendelea kuligharimu taifa hili. Lakini inawezekana hii ni (ya kujenga na kuvunja) ni miradi yao - you never know.
   
Loading...