Amri ya kutotoka nje yatangazwa mjini Beni mashariki mwa Dr. Congo

Wakujilipua

JF-Expert Member
May 5, 2018
1,591
1,391
Mamlaka nchini jamhuli ya kidemokrasia ya congo imetangaza hali ya hatari na msako wa nyumba hadi nyumba kila siku kati ya saa kumi na mbili jioni hadi saa mbili asubuhi maeneo ya Beni.

Gavana wa mkoa wa kivu kaskazini charly nzazu kasivita, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kikao cha usalama kilichojumuisha wajumbe wa jeshi ,polisi pamoja na vikosi vya kulinda amani vya umoja wamataifa kutikana na msururu wa maandamano ya kulalamikia mauaji ya raia .

Licha ya serikali kusema kuwa hatua hiyo ni moja ya njia mbadala ya kubaini maficho ya maadui na pia kulinda usalama wa raia, pia baadhi ya watu hawajaridhishwa na hatua hiyo.

Hatua hiyo imepokelewaje? wanasema kuwa hatua hiyo inawanyima uhuru wa kutembea hasa wafanyabiashara wa usiku kama vile boda boda,migahawa pamoja na hoteli.

"serikali ni bora ichukue mbinu nyingine na wala sio hii ya msako kwani itakuwa vigumu kudhibiti vilabu na pia raia wana jificha vichakani " anasema wakili omari kavota kutoka shirika la kutetea haki la CEPADHO

Pia waandamanaji wanavilalamikia vikosi vya jeshi la congo pamoja na vile vya kulinda amani nchini DRC monusco kushindwa kuwapa usalama sasa basi tiririsha maoni yako juu ya hatua hii ya jeshi la Congo

MUNGU IBARIKI TANZANIA TUENDELEE KUWA NA AMANI HII HII TULIYONAYO .
 
baadhi ya picha huko beni
 

Attachments

  • Screenshot_2019-11-27 Amri ya kutotoka nje yatolewa DR Congo - Kunani (1).png
    Screenshot_2019-11-27 Amri ya kutotoka nje yatolewa DR Congo - Kunani (1).png
    639.1 KB · Views: 1
  • Screenshot_2019-11-27 Amri ya kutotoka nje yatolewa DR Congo - Kunani .png
    Screenshot_2019-11-27 Amri ya kutotoka nje yatolewa DR Congo - Kunani .png
    741 KB · Views: 1
  • Screenshot_2019-11-27 Amri ya kutotoka nje yatolewa DR Congo - Kunani (2).png
    Screenshot_2019-11-27 Amri ya kutotoka nje yatolewa DR Congo - Kunani (2).png
    543 KB · Views: 1
Back
Top Bottom