Amri kuu ya chama chetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amri kuu ya chama chetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mundali, Sep 23, 2010.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  UPENDE UFISADI, KWA MOYO WAKO WOTE, KWA NGUVU ZAKO ZOTE NA KWA AKILI ZAKO ZOTE. HII NDIO AMRI ILIYO KUU TENA NI YA KWANZA, NA YA PILI YAFANANA NAYO NAYO NI HII, MPENDE FISADI KAMA NAFSI YAKO. AMRI HIZI ZIMETOKANA NA MFUMO TULIOJIWEKEA.

  MASHARTI YA KUJIUNGA NA CHAMA CHETU.
  1. Ubishi. Bishana mpaka ufe hata kama unachobisha unaujua ukweli wake.
  2. Kutetea chama kwa nguvu zako zote hata kama familia yako inateketea.
  3. Kuwapenda mafisadi wenzako kuliko mama yako mzazi.
  4. Kuvaa mavazi rasmi ya chama chetu kila wakati. Mavazi yetu yatakuwa na mchanganyiko wa rangi za mimea, mkaa na embe.
  5. Lazima ujue kuimba nyimbo za chama chetu mahali popote, hata kwenye misiba.
  6. Jifunze kuufanya uongo uonekane ni ukweli (mfano, Jua linachomoza magharibi na kuzama kusini).
  7. Ahadi ndio msingi wetu mkuu. Toa, tetea na himiza ahadi hata kama ni kuahidi watu kuwafanyia shooping kwenye sayari ya mars.
  8. Kujua mbinu zote bora za kuchakachua kura na matokeo ya uchaguzi.
  9. Hakikisha ushindi unapatikana hata kwa mapanga na virungu, nunua kura, vyombo vya habari kisha zingatia kuwa fujo tutaanzisha sisi kokote wanapotupinga. Polisi wataenda washindani wetu.
  10. tutabaki nambari wani hata kwenye chama akibaki mwenyekiti pekeyake.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ndio umekosa kazi ukatumwa uje uaandike huo upuuzi humu ndani
   
 3. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii kiboko, no wonder chama chenu migongano ya wenyewe kwa wenyewe ni moja kati ya misingi bora ya chama.
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Basi jueni kuwa amri hizi zinavunjwa sana na wanchama wenu mwaka huu mchana wanavaa hayo mavazi usiku wako chadema kwa bure, wanadai pesa za mafisadi haziwafikii zinaishia kwa wachache. Na wanadai kuna mafisadi wao mumewanyima uongozi wanasema wanayo mbiu yao ya kampeni inasema ''BORA TUKOSE WOTE:" Mtajijuuu
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kwani kataja ni chama gani mbona hizi sifa kama ni za chadema hivi!
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hii kali mkuu!!! the the eeee....:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:
   
 7. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Umepatia unaakili kweli kweli wewe...nani kakufundisha kujibu kinyume chake hivi ?
   
 8. m

  muafaka Senior Member

  #8
  Sep 23, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sema una sera gani, zinatekelezwaje na zinauhalisia gani otherwise hapo hakuna hoja bali ni kutaka kuwachanganya watu wenye akili zao.
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Ccm
   
 10. p

  pierre JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii imeniacha hoi.Mwenye macho haambiwi tazama.
   
 11. p

  pierre JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je watanijalije mimi mlalahoi kama nikishikamana na hizi amri za hiki chama au nitaachwa watoto wangu wakisoma shule za kata na wao wakipeleka wa kwao ulaya?Nihakikishie kwanza
   
 12. p

  pierre JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waw.Hii bab kubwaaaaaa
   
 13. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Sio kukosa kazi mkuu, hiki chama kipo na kina sera nzuri kwelikweli. Na uzuri wa chama chetu sera tunaziandaa wenyewe tunampatia mgombea wetu apite kuzinadi. Akishindwa kuzitekeleza atawaambia waliomchagua "sikushiriki kuziandaa hizi sera ni ngumu mno kutekelezeka. Laiti ningeshiriki kuziandaa nisingekubali vitu kadhaa kuingizwa".
  Chama chetu kinashiriki chaguzi zote kubwa na ndogo. Wagombea wetu wana mbinu kali za kuombea kura. Mosi wanajifunza kusahau hoja mbalimbali, hata kama ni za nusu saa iliyopita. Halafu wanazinadi sera zetu, mkiwachagua tu, utekelezaji wa sera mbadala unaanza (ufisadi), mkiwauliza mbona sera zenu zinasema kupambana na rushwa nyie mwaenda kinyume, Jibu ni lilelile, hatukushiriki kuziandaa.
  Chama chetu ni miongoni mwa vyama maarufu sana, kama ukipenda ntakuelekeza kwa mifano unayoishi nayo.
   
 14. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,728
  Likes Received: 3,145
  Trophy Points: 280
  Mbavu zinauma kwa kucheka.. Asante sana mkuu kwa sala ya iliyotoka kwa aliyetuumbia ccm
   
 15. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  nahisi ofisi za chama hiki zipo lumumba.
   
 16. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #16
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimekubali PhD yako sio feki
   
Loading...