Ampiga mama yake mzazi kisa maneno ya mke wake

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,397
"
Inavyosemekana haijathibitika.

Huyo kijana katika video anamchapa mama yake mzazi. Sina hakika kama ni kweli vyovyote iwavyo sijapendezwa kabisa nimechukizwa kweli.

Naomba anaejua ukweli wapi hii imetokea?Ni mkoani Kagera au popote na ikiwezekana huyo kijana na huyo anaeongea kurekodi sheria iwashukie.

Ni Unyama wa hali ya juu na seems huyo mama huwa anapigwa mara kwa mara.Na hii video wamerekodi kama sehemu ya kumdhalilisha mama huyu.

Waziri wetu, mama yetu Ummymwalim naomba uweke mkono wako tumsake. Jeshi la polisi policetanzania tunaomba sana Plss yoyote anaeweza kupaza sauti tupaze mpaka wapatikane.

Imeniuma nami nimeamua ku share nanyi Naimani sector zoote Serikalini Zipo Humu na watachukuwa Hatua Katika hili Kama kweli limetokea kwetu Nchini.

Chanzo #dinamarius
1583386934338.png



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bikira Maria umejaa neema Bwana yu nawe umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa, Maria mtakatifu Mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu na milele amina.
 
Dini inatuzuia kuwatendea Wazazi Wetu ukatili Hatakama watatuuzi vp wawe wachawi wachonganishi nk

Kuzuia Yote Hayo Inahitajika Hekima Sababu Mzazi ni njia na Moja Ya Sababu ya kuona flame wa Mungu

Lkn Vijana wasasa sijui ni kiburi madawa bange Wanawake au Nini Kinacho tufanya Kuchukuwa Maamuzi Makali yakuchukiza Jamii na mungu kiujumla
Waheshimu baba na mama upate miaka mingi dunia

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Innalilah waina ilaih rajiuna haya ni matatizo ya watoto kutomjua Mungu na thamani ya wazaz matokeo ndio haya mtu hajui hata nafasi ya mzaz ni ipi.

Watoto wa siku hizi wanashinda nursery school ni shule kila siku ndio matokeo haya watoto wanakuwa km misekule wanapiga na wazazi fimbo kabisa
 
Kwa waganda?
Moja ya magroup yangu INASEMAKANA ni Tanzania lakini ukanda huo huo wa mpakan na Uganda. Anayempiga ni mtoto wa anayepigwa na anayerekodi ni mkwe wa anayepigwa.

Sababu ya kupigwa huyu mama Inasemekana hao wawili, mke na mume walikuwa nje(ughaibuni) walikuwa wanazichanga pesa na kuzituma kwa mama na kumpa maelezo ya jinsi ya kuzitumia hizo pesa lakini bahati mbaya mama akawa anatumia tofauti kabisa na maelezo hivyo walivyorudi na kukuta ni tofauti na walichotarajia kukikuta hiyo ndio adhabu waliyoona inafaa eti kumpa mama yao.

Mungu awalaani hawa kunguni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom