Amos Makalla: Uhalifu utabaki Historia Dar. Amwambia Rais Samia kama shughuli imepata Mwenyeji

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
626
1,000
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla amempongeza Rais Samia kwa kazi Nzuri anayoifanya ikiwemo tukio alilofanya leo kuendelea kuboresha huduma za Afya.

Makalla amemuhakikishia Rais Samia, yeye kama mkuu wa Moka wa Dar na mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama kwamba Mkoa uko Salama na kazi aliyompa, wamejipanga na kazi waliyoianza kuhakikisha wananchi wako salama Uhalifu utabaki Historia.

Pia, Makalla amemshukuru Rais Samia kwa kumpa heshma, kumkumbuka na kumpa ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema hatomuangusha na ameanza kwa kukimbia badala ya kutembea.

Makalla amesema Rais amemrudisha nyumbani kwani yeye ni mtoto wa Dar, amezaliwa na kukulia hivyo kama shughuli imepata mwenyeji.

kaka km

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
1,335
2,000
Aendelee kuwamaliza wezi wa magari, wezi wa vifaa vya magari, majambazi ya kutumia silaha.

Hao wanatakiwa kupotea ama wakinusurika wawe na kesi za miaka jela.

Wambula alisifika kumaliza ujambazi hapa Dar, wambura atupatie kijana wake anarmuamini aendeleze legacy yake.
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,571
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla amempongeza Rais Samia kwa kazi Nzuri anayoifanya ikiwemo tukio alilofanya leo kuendelea kuboresha huduma za Afya.

Makalla amemuhakikishia Rais Samia, yeye kama mkuu wa Moka wa Dar na mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama kwamba Mkoa uko Salama na kazi aliyompa, wamejipanga na kazi waliyoianza kuhakikisha wananchi wako salama Uhalifu utabaki Historia.

Pia, Makalla amemshukuru Rais Samia kwa kumpa heshma, kumkumbuka na kumpa ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema hatomuangusha na ameanza kwa kukimbia badala ya kutembea.

Makalla amesema Rais amemrudisha nyumbani kwani yeye ni mtoto wa Dar, amezaliwa na kukulia hivyo kama shughuli imepata mwenyeji.

Mhu; tusubiri kuona.
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,689
2,000
Vibaka ni wengi sana yaani polisi wajipange hasa. Ikiwezekana arudishe hata sungusungu kwa operation maalum. Vibaka wanatunyanyasa sanaa
 
fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,748
2,000
Mkuu wetu Huyu mbona naye anataka kujifanya mtoto pendwa kama makondaa,muda wote tu anajizungumziya yeye
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom