Amos Makalla, tekeleza matamko yako mkoa wa Dar es Salaam

Utawala wa Samia wote hauheshimika kama wakati wa JPM, enzi za JPM agizo lisipotimizwa kuna mtu ataliwa kichwa wakati saivi hata agizo la Rais mwenyewe halitimizwi na maisha yanaendelea kama kawaida.
 
nimemuona Mkuu wa wilaya ya Temeke tu pamoja na kamati yake ikifuatilia maelekezo hayo kwa vitendo, wasaidizi wengine wametulia kama vile hawapo.
sasa unadhani kweli RC anaweza kujigawa ktk wilaya zote.
 
matamko raia wameshayachoka sijui? yaani kipindi hiki cha uviko 19 watu wengi hawavai barakoa, wanasongamana no social distance, daladala ndio kabisa kujazana.. matamasha ya miziki kama kawaida,, nobody cares
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makala umetoa matamko sana tangia ule kiapo cha kuwa Mkuu wa Mkoa, cha ajabu hakuna linalotekelezwa hata moja

1) Ulianza na machinga ukachimba biti weeeh mwisho siku hakuna lililotekelezwa.

2) Ukaenda kukagua mradi wa mwendo kasi Mbagala ukachimba biti ukatoa siku 3 wananchi watoke kupisha ujenze ila wananchi wamekugomea huko Mbagala.

3) Umetoa tamko la kuvaa barakoa na kukaa level seat kwenye vyombo vya usafiri lakini hakuna lililotekelezwa.

Mkuu wa Mkoa Amos Makalla unafeli wapi? Jitathimini kwanza kabla ya kutoa matamko ama sivyo itaonekana Hayati alikupiga benchi sio kwa bahati mbaya.
Huyu benchi lilikuwa halali yake ,mswahili sana,itakuwa kapigiwa pande na waswahili wenziwe wa msoga tu,majungu mengi sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom