Elections 2010 Amos Makalla "Maji ya Shingo" Mvomero

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
Wana JF,

Hivi karibuni nilikuwa Morogoro kwenye shughui zangu binafsi. Katika mizunguko yangu wilayani Mvomero nikajikuta nimevutiwa kutaka kujua hali ya kisiasa ikoje. Maeneo/vijiji nilivyobahatika kufika ni pamoja na Turiani, madizini, manyinga, Kidudwe, Magole, Mvomero na maeneo mengine ambayo majina yake yamenitoka.

Nilifanikiwa kuzungumza na wakazi wa maeneo hayo kuhusiana na uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Nilichoshuhudia huko ni kwamba wananchi wana mwamko mkubwa sana juu ya uchaguzi wa mwaka huu, na zaidi ni kwamba wanataka mabadiliko ya kweli.

Na pasipo kuumauma maneno wanasema mwaka huu Amos Makala imekula kwake, kuna kijana wa Chadema anaitwa Matokeo Owden Manyeta almaarufu "Mau" ndio chaguo lao. Kutokana na hali hiyo nikaambiwa kuwa bw. Makala ameamua kuwatumia hadi viongozi wa kanisa analosali pale turiani kumsaidia kampeni kwa waumini wenzake, hususani wanakwaya kwakuwa aliwahi kuisaidia kwaya hiyo kwa kuinunulia vyombo vya muziki na ufadhili mwingine mwingi tu.

Bahati mbaya kwake ni kuwa bw. Mau naye ni muumini wa kanisa hilo, kwahiyo hata wanakwaya wamegawanyika wengine wanamuunga mkono bw. Makala na wengine bw. Mau. Pia nikaambiwa bw. Makala amekuwa "mkarimu sana" kama anavyofanya mama wa arusha mjini na takukuru ya mvomero wanaimba nyimbo zile zile wanazoimba wenzao wa arusha mjini.

Haya wapiga kura wa Mvomero kazi kwenu.

Nawasilisha.
 

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,152
1,250
Ni vyema mgombea huyo akapatiwa mbinu za kisasa za kulinda kura, natumai viongozi wa chadema ambao hawako kwenye kampeni watashughulikia hilo.
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
13,398
2,000
Mkuu habari njema lakini Manyeta anatakiwa kuwa makini CCM ni wazuri sana wa kuchakachua matokeo.Ajizatiti kulinda / kuzuia wizi wa kura.
 

Nyuki

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
367
0
ni vyema mgombea huyo akapatiwa mbinu za kisasa za kulinda kura, natumai viongozi wa chadema ambao hawako kwenye kampeni watashughulikia hilo.

hata akishindwa mkullu atampa waku teuliwa then atakuwa waziri wa fedha maana ameshata uzoefu mkubwa alipokuwa mweka hazina wa cham cha mapinduzi taifa
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
ni vyema mgombea huyo akapatiwa mbinu za kisasa za kulinda kura, natumai viongozi wa chadema ambao hawako kwenye kampeni watashughulikia hilo.
Sawa kabisa mkuu, nadhani viogozi wa chadema wafike sehemu wajiandae kwa dhati kulinda kura zao, vinginevyo ccm itawafanyia kitu mbaya kabisa. Nadhani kuna wanachama wa chadema hapa jf na viongozi wao pia wako humu, nadhani ushauri wako wataufanyia kazi.
 

Anna Gilbert

Member
Sep 27, 2010
8
20
CCM wanamuhitaji sana makala awe mbunge ili apewe uwaziri, so CHADEMA wanatakiwa wawe makani sana kwenye kura maana ccm ni wataalam wa kuchakachua
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
hata akishindwa mkullu atampa waku teuliwa then atakuwa waziri wa fedha maana ameshata uzoefu mkubwa alipokuwa mweka hazina wa cham cha mapinduzi taifa
Angekuwa na uhakika wa kupata nafasi ya ubunge wa kuteuliwa kama angekuwa na uhakika wa JK kushinda.
Kwakuwa yuko jikoni ccm huenda anaujua ukweli ndio maana anapigana kufa na kupona ili apate nafasi ya kuigia mjengoni.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
182,467
2,000
CCM waitishe kikao cha dharura na kumshauri JK ajitoe ili aweze kuwanusuru wabunge wake vinginevyo Ikulu na Bunge litabebwa na Chadema.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
45,045
2,000
ndugu wamec hemsha huyo ndio mbunge wao mtarajiwa cya baada ya uchaguzi
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
CCM waitishe kikao cha dharura na kumshauri JK ajitoe ili aweze kuwanusuru wabunge wake vinginevyo Ikulu na Bunge litabebwa na Chadema.
Hawana sababu ya kuitisha kikao cha dharura, tayari wanajua kwamba safari hii hawauziki, na wananchi hawadanganyiki tena.
Haya makelele unayoyasikia toka kwa Lt. Gen. Shimbo ni dalili kwamba JK anajua yuko kwenye wakati mgumu ndiposa anatafuta namna ya kutisha watu ii waweze kuchakachua matokeo.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
45,045
2,000
Mao santiago wish na nakutakia heri uchaguzi mwema sin uhakika na hawa mabwana wanavyojipanga ndio maana na kuwa na wasi wasi nduguyo udboy
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,476
2,000
Mweka hazina wa chama tena nae hoi,atatumia mihera tuuuuuuuuuuuu
 

Pengo

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
579
0
Kweli humu ndani kuna watu kazi yao ni kudanganya wenzao tuu,hongera sana kwa kumpa mfupa autafune kibogoyo!
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
Mao santiago wish na nakutakia heri uchaguzi mwema sin uhakika na hawa mabwana wanavyojipanga ndio maana na kuwa na wasi wasi nduguyo udboy
mkuu unaweza kuwa mtu wa msaada sana kwa udboy mwenzako kwa kumfikishia salam na tahadhar ya wanamapinduzi wa kweli na wazalendo waliko jf. Kuna mawazo mengi sana mazuri yanatolewa hapa, kubwa kabisa la kulinda kura, ni vizuri akajipanga manake wao wanasema "ushindi ni lazima"!!
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
Mweka hazina wa chama tena nae hoi,atatumia mihera tuuuuuuuuuuuu
mkuu hilo ndio zoezi linaloendelea huko tena kwa kasi ya ajabu.

hizi kampeni za shuka kwa shuka usizipimie kabisa, wananchi wanasema takukuru Mvomero wakipigiwa simu, na wao wanampigia makala au wapambe wake, imefika sehemu wanahamasishana kwamba bora wale mihela yake tu hakuna jinsi.

Nikaambiwa kuwa wamekuja na mbinu nyingine ya kuunda timu za kampeni za watu 200-400 na kila baada ya mkutano wanagawa mpunga kwa kisingizio cha kuihudumia timu ya kampeni.
 

Vakwavwe

JF-Expert Member
May 16, 2009
505
195
i know the guy....ni mhandisi wa mitambo na uwezo wa uongozi anao......nilisoma naye kuanzia sec mpaka chuo......
wachakachuaji wa matokeo watashindwa tu....maombi tunayoyafanya sasa hivi ni Mungu mwenyewe atalinda kura.......
Tahadhari: CHICHIEMU wanatumia uzushi huu kukatisha tamaa watu wasipige kura....jamani pigeni kura tutashinda hata wakiiba ,mbona karatu wamekuwa wakiiba lakini hawakuweza kumshinda rais mtarajiwa...
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,567
1,250
i know the guy....ni mhandisi wa mitambo na uwezo wa uongozi anao......nilisoma naye kuanzia sec mpaka chuo......
wachakachuaji wa matokeo watashindwa tu....maombi tunayoyafanya sasa hivi ni Mungu mwenyewe atalinda kura.......
Tahadhari: CHICHIEMU wanatumia uzushi huu kukatisha tamaa watu wasipige kura....jamani pigeni kura tutashinda hata wakiiba ,mbona karatu wamekuwa wakiiba lakini hawakuweza kumshinda rais mtarajiwa...
Ahsante sana mkuu, niliambiwa kwamba kijana ni mhandisi kitaaluma lakini sikufanikiwa kujua fani yake. Mi nadhani watu wa mvomero hawatakosea wala kujutia uamuzi wao kumchagua mhandisi Mau.
 

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
195
Wakuu am following this report and will come with unbiased report.. stay tuned
nitafanya ziara kuanzia Mvomero,Msufini,Hembeti,Dihombo,Mkindo,Kigugu,Chazi,Turiani na mtibwa then i will share my findings with you
 
Top Bottom