Amos Makalla: Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa. Kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,228
2,000
Mkuu wa mkoa wa Dares salaam Amos Makalla amesema kwenye dawati la jinsia kuna wanaume aliowaita marioo wanakuja kulalamika kunyanyaswa na wanawake wenye fedha kwani huwapatia vitu alafu wakiachana wanawanyang'anya kila kitu hivyo hurudi nyuma kimaisha kwa kuwa mwanaume suruali.

========

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salama, Amos Makalla amesema pamoja na kupokea kero za wanawake wanaokutana na unyanyasaji wa kijinsia wapo wanaume wanaohitaji msaada kutokana na changamoto za aina hiyo.

Akizungumza leo Alhamisi Novemba 25, 2021 wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Makala amesema sasa hivi wanaume wamekuwa na malalamiko dhidi ya wanawake wenye fedha.

“Nilikuwa na ziara ya kusikiliza kero za wananchi, asilimia 30 ya kero 927 nilizopokea zinatokana na changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia."

“Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa. Kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa, hivyo anaweza kumpa kitu mwanaume na kumnyang’anya punde wakiachana,” amesema Makalla.

Mkuu huyo wa mkoa ameongeza, “Nimeyaona hayo wale wanaume marioo waliozoea kitonga wanakuja ofisini kulalamika kuwa walipewa mali na wanawake lakini wakanyang’anywa.

“Sasa swali linakuja hii sio ukatili? Naona kuna mjadala mpana katika hili suala la unyanyasaji wa kijinsia ndio mana mjadala mzuri wenye lengo la kuboresha sheria za ndoa,”.

Chanzo: Mwananchi
 
Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
777
1,000
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salama, Amos Makalla amesema pamoja na kupokea kero za wanawake wanaokutana na unyanyasaji wa kijinsia wapo wanaume wanaohitaji msaada kutokana na changamoto za aina hiyo.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Makala amesema sasa hivi wanaume wamekuwa na malalamiko dhidi ya wanawake wenye fedha.

“Kwenye kero nilizozikuta wapo wanaume wanaonyanyaswa. Kuna wanawake wana fedha wanahitaji tu wanaume wa kuwaoa, hivyo anaweza kumpa kitu mwanaume na kumnyang’anya punde wakiachana,” amesema Makalla.
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
12,748
2,000
Nikionaga mwanamke anayesapoti unyanyasaji huwa najiskia vibaya.
Kama umenyanyaswa na mwanaume utambue dio wote wenye roho hii.
Wanaume wengi tumekuwa walezi wema kwa wanawake lakini bado hamtambui.
Umenisikitisha sana
 
Jagarld

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
2,239
2,000
"Msinione hivi, nikiwa nyumbani huwa napigishwa hadi deki na Mama naniiii" mwisho wa kunukuu.
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
7,232
2,000
Kunyanyaswa ni matokeo yanayosababishwa na kitu au mambo fulani, je ni mambo gani hayo?

Mfano ikitokea mwanamke afanye majukumu ambayo yanapaswa kutimizwa na Mwanaume badala ya Mwanaume huyo kuwa mwaminifu unakuta tena anaharibu kwa kufanya usaliti hapo unategemea mwanamke ata-react vipi kwa mfano?!

Anangalieni mlipojikwaa kabla ya kuangalia mlipoangukia.
 
to yeye

JF-Expert Member
May 30, 2016
5,780
2,000
Nikionaga mwanamke anayesapoti unyanyasaji huwa najiskia vibaya.
Kama umenyanyaswa na mwanaume utambue dio wote wenye roho hii.
Wanaume wengi tumekuwa walezi wema kwa wanawake lakini bado hamtambui.
Umenisikitisha sana
I don't care...serious. Hata mnavyokufa hovyo ni sawa tu
 
to yeye

JF-Expert Member
May 30, 2016
5,780
2,000
Nikionaga mwanamke anayesapoti unyanyasaji huwa najiskia vibaya.
Kama umenyanyaswa na mwanaume utambue dio wote wenye roho hii.
Wanaume wengi tumekuwa walezi wema kwa wanawake lakini bado hamtambui.
Umenisikitisha sana
Huwajui vyema wanaume wewe! Kama upo vizuri hongera sana.But ogopa sana hawa watu
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
12,748
2,000
Nishageuzwa moyo hata sijali tena,,naangalia nipate VP pesa nilee wanangu na siyo kujali mwanaume.Niliyopitia yanatosha...HAPANAA
Unajua hata wapo wanaume wengi wamepitishwa magumu na wanawake.
Lawama zipo pande zote tu
 
to yeye

JF-Expert Member
May 30, 2016
5,780
2,000
Mimi ni mwanaume na nikimbilio la ke wengi tu kwa mambo ya kibinadamu
Ka ka hapana,hapana yaan HAPANAA! Sina huruma na mwanaume japo Mungu kanipa mtoto wa kiume naishia kumwombea asije kuumiza wala kuumizwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom