Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,787
4,424
SERIKALI YARUHUSU WAFANYABIASHARA KUREJEA KARUME KWA MPANGO MZURI.

- Umati walipuka kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan.

- RC Makalla apokea taarifa ya ripoti ya Kamati iliyoundwa kuchunguza Chanzo Cha Moto.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameruhusu Wafanyabiashara wa Soko la Karume kurejea na kuendelea na Biashara kwa kuwekewa Mpango mzuri ambapo Wafanyabiashara wa Soko hilo wamepongeza uamuzi huo na kuishukuru Serikali.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na Wafanyabiashara hao Mara Baada ya kupokea Taarifa ya ripoti iliyoundwa kuchunguza chanzo Cha Moto, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Rais Samia ameelekeza pia uwepo utaratibu mzuri wa kuzuia Moto, kuhakikisha hakuna atakaedhulumiwa eneo lake na kutoa ruhusa kwa Wafanyabiashara kujenga Vibanda kwa gharama zao.

Kuhusu Ripoti ya chanzo Cha Moto, RC Makalla amesema Kamati imebaini Moto huo ulitokana na Mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za kulevya "Mateja".

Aidha RC Makalla amesema Baada ya kupokea ripoti hiyo ataikabidhi kwenye Mamlaka za juu kwaajili ya utekelezaji wa maoni na Mapendekezo yote ya Kamati.

Miongoni mwa Maoni na Mapendekezo ya Kamati hiyo Ni pamoja Ujenzi wa Soko jipya linaloendana na Hali ya Sasa na vizimba kutolewa kwa kipaombele kwa wazawa, uwepo wa mfumo mzuri wa kuzuia Moto, Barabara za kuingia na kutoka, Ujenzi wa Majengo ya Muda mfupi, Kila mfanyabiashara kuwa na bima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na Kuungua Hilo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 7.2 ambapo idadi ya Wafanyabiashara waliokumbwa na janga Hilo Ni 3,090.

Pia soma:

- Shuhuda: Chanzo cha moto soko la Karume ni mateja, waliangusha mshumaa wakati wanatengeneza mihadarati (18/01/2022)

 
Tumesikia taarifa ya Tume iliyoundwa kwa ajili ya uchunguzi wa chqnzo cha moto Soko la Karume Dsm.....almaarufu mchikichini.
Kwa Taarifa hii

(1) Ninamuomba Madame President ikimpendeza YAANI IKIMPENDEZA WAJUMBE WA HII TUME WASILIPWE KWA KWELI SABABU WAMETUMIA MUDA MWINGI KU PROVE MANENO YA MLINZI

(2) MLINZI AHOJIWE TENA VIZURI KUHUSU UPATIKANAJI WA MISHUMAA KWA AJILI YA KUCHOMA SOKO/ MASOKO USIKU
NI HAYO TU....ILA MBONA BWANA ZUNGU HAFUNGUI MDOMO WAKATI HILI LIMETOKEA JIMBONI MWAKE ? AU ANA JADILI KUUPATA UNDUNGAI ?
 
Back
Top Bottom