Amos Makalla bado hujaiona faida ya Katiba Mpya?

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Tunakumbuka kuwa mwisho wa mwezi wa 5 mkuu wa mkoa Dar aliitisha vikao mbalimbali tena kwa mbwembwe nyingi mbele ya camera na kuja na mapendekezo ya kuisuka upya Dar na kuwapanga upya machinga kwa kuwa hafurahishwi na namna ilivyo sasa.

Akaenda mbali kwa kutoa maagizo kwa wakurugenzi kuanza mchakato huo.

Ila baada tu ya Rais mama Samia kuwatumbua mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa morogoro kwa kuwabugudhi machinga, hatimaye Amos Makalla akaamua kimya kimya kisitisha jambo hilo.

Hii yote ni kutokana na hofu ya kutumbuliwa, kwa kuwa anaweza asimfurahishe boss wake.

Wazo la Makalla huenda lilikuwa zuri lakini kwa hofu ya kutumbuliwa kama wenzake imebidi alisitishe.

Hapa ndio umuhimu wa Katiba mpya unapoonekana kwa maana itaenda kuondoa uMungu kwa Rais.

Rais amekuwa ndio kila kitu, ikitokea umefanya Jambo halijamfurahisha basi unatumbuliwa faster sana. Hivyo watendaji wanasubiri matamko ya Rais

Leo ikitokea Rais Samia akasema anaona machinga wanapaswa waondoke utaona kuanzia waziri, mkuu wa mkoa na watendaji wote watavyopigana vikumbo kufanya jambo hilo.

Hivyo Mh.Amos Makalla kama utaridhia basi tuungane kudai katiba mpya.

#katiba mpya ni sasa#
#hatuwezi kusubiri tena#
Screenshot_20210712-131056_1.jpg
 
Jana Katibu mkuu CCM ameagiza matuta yabarabara Rukwa hadi Tunduma yaondolewe.

Meneja Tanroad amesema lipo juu ya uwezo wake.

Serikali ileile ya chama inabishana kwa matamko.
 
Jana Katibu mkuu CCM ameagiza matuta yabarabara Rukwa hadi Tunduma yaondolewe.

Meneja Tanroad amesema lipo juu ya uwezo wake.

Serikali ileile ya chama inabishana kwa matamko.
Aisee huu ni ujinga.
 
Jana Katibu mkuu CCM ameagiza matuta yabarabara Rukwa hadi Tunduma yaondolewe.

Meneja Tanroad amesema lipo juu ya uwezo wake.

Serikali ileile ya chama inabishana kwa matamko.
Mkuu,

Hatua za kuweka tuta barabarani lina mlolongo mrefu uschukulie kama unavyofikiria.

Hata kuliondoa tuta baada ya kuwekwa huwezi kuamka na kuliondoa kisa liesababisha ajali kwa kupunguza mwendo ghafla.

Meneja Tanroads yuko sahihi, na katibu mkuu hayuko sahihi kutoa maagizo tu wakati anajua ni mpaka agizo hilo liende wizarani na watalaamau kutumwa kwenda eneo husika kutathimini.

Siasa mbaya sana eti mtui anajitokeza na kudai matuta yana tuchelewesha safari wakati waliowekwa kulikuwa na sababu za msingi kufanya hivyo.
 
Jana Katibu mkuu CCM ameagiza matuta yabarabara Rukwa hadi Tunduma yaondolewe.

Meneja Tanroad amesema lipo juu ya uwezo wake.

Serikali ileile ya chama inabishana kwa matamko.
Hapo kuna siasa na utaalam. So mtaalam ni mshindi. Wewe ndo unahangaika na matamko ya kisiasa kwenye ishu za kitaalam.

Fuatilia,maagizo yote ya kisiasa kwenye ishu za kitaalam huwa yanaishia jukwaani,au mbele ya kamera.

Na huwa wakikutana kwenye vikao vya majumuisho,wanamalizana hukohuko.
 
Back
Top Bottom