Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Tunakumbuka kuwa mwisho wa mwezi wa 5 mkuu wa mkoa Dar aliitisha vikao mbalimbali tena kwa mbwembwe nyingi mbele ya camera na kuja na mapendekezo ya kuisuka upya Dar na kuwapanga upya machinga kwa kuwa hafurahishwi na namna ilivyo sasa.
Akaenda mbali kwa kutoa maagizo kwa wakurugenzi kuanza mchakato huo.
Ila baada tu ya Rais mama Samia kuwatumbua mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa morogoro kwa kuwabugudhi machinga, hatimaye Amos Makalla akaamua kimya kimya kisitisha jambo hilo.
Hii yote ni kutokana na hofu ya kutumbuliwa, kwa kuwa anaweza asimfurahishe boss wake.
Wazo la Makalla huenda lilikuwa zuri lakini kwa hofu ya kutumbuliwa kama wenzake imebidi alisitishe.
Hapa ndio umuhimu wa Katiba mpya unapoonekana kwa maana itaenda kuondoa uMungu kwa Rais.
Rais amekuwa ndio kila kitu, ikitokea umefanya Jambo halijamfurahisha basi unatumbuliwa faster sana. Hivyo watendaji wanasubiri matamko ya Rais
Leo ikitokea Rais Samia akasema anaona machinga wanapaswa waondoke utaona kuanzia waziri, mkuu wa mkoa na watendaji wote watavyopigana vikumbo kufanya jambo hilo.
Hivyo Mh.Amos Makalla kama utaridhia basi tuungane kudai katiba mpya.
#katiba mpya ni sasa#
#hatuwezi kusubiri tena#