Amos Makala Vs. Viongozi wa Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Amos Makala Vs. Viongozi wa Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paparazi Muwazi, Jan 16, 2009.

 1. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Amos Makala awashukia Mbowe na Dr Slaa kwa ufisadi

  Mweka hazina wa CCM Amos Makala ameendelea na mkakati wake mahiri wa kuisafisha CCM. Leo katika mkutano wake na wanachuo wa IFM ameisafisha CCM kuwa haihusiki na ufisadi na kwamba CHADEMA ndio chama chama cha kifisadi. Amesema Mbowe na Dr Slaa wametia mfukoni mwao shilingi milioni 78 zilizokuwa zinunuliwe pikipiki kwenye uchaguzi wa mwaka 2005. Amewaeleza wanavyuo kuwa CHADEMA ni chama kinachochea migomo katika vyuo vyao kwa lengo la kumondoa Kikwete madarakani. Ameyasema hayo akizindua tawi la CCM la wanachuo wa IFM katika Ukumbi wa Karimjee

  PM
   
  Last edited by a moderator: Jan 18, 2009
 2. Kaka K

  Kaka K Senior Member

  #2
  Jan 16, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi siasa za kuviziana....hazina faida hata kidogo kwa maendeleo ya nchi. Sio kila kitu kinahitaji siasa...matatizo yaliyopo Tanzania yanahitaji suluhu na si hizi maneno maneno.
   
  Last edited: Jan 16, 2009
 3. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CCM bwana yani hata muweka azina anakuwa na sauti doh! Makala na we ni fisadi tu kama usingekuwa fisadi usingefutuka namna hiyo bwanaaa usitafute kujikomba komba wakupe post kubwa zaidi......... kawadanganye kwenu singida
   
 4. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Je sheria yetu nchi inaruhusu kuanzisha matawi ya vyama vya siasa katika taasisi mbali mbali za elimu au mahala pa kazi???
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hivi msajiri wa vyama vya siasa yuko wapi hata CCm wanaingiza siasa vyuoni? toka Karimjee hadi ofisini kwa msajiri wa vyama ni mwendo kurusha jiwe tu,
  Au nayeye anasubiri aletewe maelezo na Polisi ambao wao watayapata maelezo toka kwa Chama kitakacholalamika?
   
 6. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Kama matawi ya CCM yanaanzishwa London na Jakarta..ijekuwa bongo-Lol
   
 7. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kazi bado ipo manake kama wengekuwa/vingekuwa vyama pinzani ya ccm nadhani wengezuiliwa lakini kwa kuwa wao wameshika mpini na ndio watawala kwa muda huu basi watafanya watakavyo.
  Yangu macho, itabidi msajili wa vyama awe na ulinganifuli unaolingana kwa vyama vyote na sio kuelemea upande mmoja.
   
 8. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF naona mjadala sasa unataka kuharibika kwa dataz za kudhania vile. Naomba ieleweke kuwa kuna makundi mawili hapa tunayoyaongelea: La kwanza ni kundi la akina Mzindakaya, JK, Karume, Rwakatare n.k. Hawa wana shahada za heshima tu (honoris causa) siyo za kusomea! Chuo chochote kinaweza mtunukia mtu shahada hiyo ya heshima kwa kutambua mchango wake katika jambo fulani. Siku za nyuma hata baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Spika Adam Sapi, Salim Ahmed Salim, Kaunda na Obote walipewa heshima hiyo na vyuo mbalimbali duniani.

  Kundi lenye matatizo ni lile lenye shahada feki na linadai kuzisomea shahada hizo! Kundi hili ni hatari sana maana linaharibu kabisa heshima, sifa na viwango vya elimu nchini. Wafuatao wana vyeti feki vinavyoitia aibu Serikali na nchi kwa ujumla:

  (1) Salmin Amour - Ph.D yake ni feki, ya kisiasa. Aliipata Ujerumani Mashariki enzi hizo kwa miezi mitatu tu huku akiwa na cheti cha form four tu!
  (2) Pius Ng'wandu - Ph.D yake ni feki. Chuo anachodai kusoma cha Stanford, Marekani hakina kumbukumbu zake. Aliosoma nao huko Marekani, akina Prof. Baregu, wanajua kuwa ana Masters tu!
  (3) Mary Nagu - Ph.D yaje ni ya kununua kwenye mtandao.
  (4) Emmanuel Nchimbi - Ph.D yake ya uchumi ni ya kununua. Hana uelewa wowote wa economics kichwani mwake.
  (5) Makongoro Mahanga - Ph.D yake ya ugavi ni ya kununua kama Nchimbi.
  (6) Didas Masaburi - Ph.D yake ilinunuliwa pamoja na ya kaka yake Makongoro.
  (7) Norman Sigallah - Ph.D yake ni ya kununua kwenye mtandao.
  (8) Mafwenga - Ph.D yake sawa na ya Sigallah
  (9) Nangale - Ph.D yake ni kutoka chuo kimoja bomu cha chini ya viwango, London.
  (10) Mathayo David - Ph.D ya kujipachika.
  (11) Mutamwega - Ph.D yake ni feki, ya kununua. Mhusika hawezi kuandika hata sentensi moja sahihi ya Kiingereza.
  (12) Lukuvi - Masters yake ni feki. Kaipata akiwa na sifa za elimu ya darasa la saba na cheti cha ualimu, class C.
  (13) Samuel Chitalilo - Vyeti vyake vya elimu ya juu toka Uganda vyote ni feki. Ana kesi ya kujibu mahakamani!
  Nimepata taarifa mbalimbali kuhusu vyeti vya Wabunge wafuatao: Sigonda, Capt.Komba, Omari Mzeru na Savelina Mwijage. Nazifanyia kazi. Nitazianika hapa muda muafaka!

  Ijabu

  Ijabu kanipa hamasa sana juu ya suala hili. Wote aliowaeleza kweli wana vyeti feki na hata ukiongea nao, ni vihiyo vihiyo wa kutupwa! Naomba niongeze majina mengine kwenye listi la Mhe. Diodorus Buberwa Kamala, Mbunge wa Mkenge na Waziri wa A. Mashariki. Huyu bwana kasoma Mzumbe kama Nchimbi ambako mtandao wa vyeti feki ulianzia na Mkuu wa Chuo hicho Bw. Warioba. Ph.D yake ni feki, ni ya kununua kama hizo za wenzake aliowataja Ijabu. Hata kwenye Bunge la A. Mashariki tunaambiwa anapwaya ile mbaya. Naibu wake, Mohamed Aboud, yeye ndo balaa maana ni form four failure na CV yake inasema uongo kuwa ana diploma ya Uingereza! Wote ni Ze Komedi mbele ya Wakenya, Waganda, Warwanda na Warundi!

  Yupo huyu mama wa Kibaha, Zaibab Gama. Anajiita Dk. wakati ana diploma ya radiology tu! Kuhusu Mbunge Savelina Mwijage (Viti Maalum, Kagera), huyu ana matatizo makubwa maana anatumia jina la marehemu. Taarifa zote zilitoka gazetini, lakini analindwa. Hawezi hata kuandika jina lake, lakini ni Mbunge. Anayebisha aje na ushahidi maana huyu mama namfahamu miaka mingi akiwa mfanyakazi wa ndani wa Mhindi Bukoba.

  Namfahamu sana Mbunge Sigonda. Ni mtu wa usalama wa Taifa aliyeishia darasa la nane. Leo naambiwa ni Dk.! Hebu tupe dataz Ijabu na wana JF wengine. Capt. Komba yeye ni msanii na mwizi asiyestahili kujadiliwa hapa maana anawaibia hata wasanii wenzake dani ya TOT. Mzeru wa Morogoro yeye ni mafix moja kwa moja. Hana udaktari wowote! Alijipachika udaktari kuombea ubunge na unaibu waziri kwa JK!

  Agustino Lyatonga Mrema - Pacific Western University, a diploma mill. Yeye alipoenda kuchukua hiyo "degree" alikwenda na matarumbeta kibao, vifijo na nderemo.

  Mustafa Mkullo - Almeda University, a diploma mill. Kule youngafrican.com nakumbuka ilisema eti chuo chake kiliwahi kutoa associate degree kwa mbwa anayeitwa "Wally" mali ya mwandishi mmoja wa habari huko Marekani (In 2004 the CBS affiliate in Albany, New York, ran a report on Almeda that featured Peter Brancato, who had filled out an application for an associate degree on behalf of his dog, Wally. Part of the "life experience" listed on the application was "Plays with the kids every day ... teaches them to interact better with each other ... Teaches them responsibilities like feeding the dog." Almeda granted Wally an associate's degree in childhood development with a course list including European culture, college algebra, American history, and public speaking.[13] In reply, Almeda claims Brancato perjured himself by creating a false identity using a fabricated name and date of birth. They write, "He completed an application that included a background of the following: Eight-years tutoring pre-K children, curriculum design and development, teaching coping skills, and volunteer coaching."" Almeda University - Wikipedia, the free encyclopedia

  Kama sijakosea waheshimiwa wengi sana wana degrees kutoka chuo cha Washington International - I think even Sofia Simba anayo ya huko (sasa Mwanakijiji asije akanishambulia kuwa namtendea vibaya interviewee wake!!!!)
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Mkuu kunani???,maana kila thread niliyoifungua nakutana na post hii!!!!,ama kuna ka 'kampeni maalum' nini
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kamanda usitualibie mabandiko hapa... Then kaa ukijua kuwa Komandoo ni msomi tosha na UDk wake ni halali kabisa, uta'adabu
   
 11. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mimi nampenda mama Diana Chilolo aka mkumbo wa Viti maalumu Singida,yeye anajua ni ngumbalu na huwa anajikalia kimya tu watu wakianza kuongelea elimu.Mwaka 2002 wakati akiwa mwl grade c pale Ipembe s/msingi ndo alikuwa anajifanyia masomo yake ili afanye mtihani wa form II bahati mbaya alipata alama (-) sijui baraza bado wanamdai maksi au vipi.

  Lakini uzuri wake yeye kimyaaaa
   
 12. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametakiwa kujiuzulu na kuwaomba radhi wanachama wake na Watanzania kwa ujumla, kutokana na kilichodaiwa ni kudanganya kwamba anapambana na ufisadi wakati naye ni fisadi.

  Tuhuma zimeelekezwa pia kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa, kwamba amekuwa akisaini nyaraka za kuchukua fedha na misaada kutoka nje kwa kigezo cha kuwasaidia wananchi tangu mwaka 2005 jambo ambalo halijafanyika hadi leo.

  Tuhuma hizo zilitolewa juzi na Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM, Amos Makala, wakati akifungua tawi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kupokea wanachama wapya 1,723 wa tawi hilo katika hafla iliyofanyika Karimjee, Dar es Salaam.

  Alisema anawashangaa viongozi wa upinzani hasa Mwenyekiti wa Chadema kwa kueneza alichodai uzushi kwamba CCM ni chama cha kifisadi wakati yeye (Mbowe) wakati akiomba ridhaa ya kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2005 aliahidi kuleta pikipiki za Sh milioni 78 na baiskeli 153 kwa kila wilaya, lakini mpaka leo hajafanya hivyo.

  Alimshutumu pia kuwa kwa kushirikiana na Slaa, alisaini nyaraka zilizoruhusu kujilipa akidai ni madeni aliyokuwa akikidai chama chake, jambo ambalo si kweli. Makala alidai pia kuwa Mbowe na Slaa walituma risiti bandia kupitia DHL kupeleka Uingereza katika shirika la kimataifa la kusaidia vyama vya siasa la Westminster, zikionyesha kuwa fedha zilitumika, jambo ambalo si kweli.

  “Kutokana na haya jamani nauliza nani fisadi? Namtaka Mbowe ajiuzulu uenyekiti wa Chadema na awaombe radhi Watanzania na wanachama wake hadharani, kwa udanganyifu alioufanya,” alisema Makala huku akishangiliwa na wanafunzi hao.

  Alisema ushahidi wa nyaraka hizo anao na endapo Mbowe na Slaa hawataridhika, wanaweza kwenda mahakamani kutafuta haki, badala ya kuwa mstari wa mbele kusema CCM mafisadi wakati wao wanaongoza kwa ufisadi wa chini kwa chini na wakiupaka matope uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

  Mwana CCM anaweza kuwa fisadi, lakini si CCM, Mbowe ana tuhuma nyingi za ufisadi, lakini yeye hazioni, anajinadi kuwa ana dhamira nzuri na nchi hii, huyo ni mwongo, mwenye dhamira ya kweli ni Kikwete ambaye baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi amewafikisha katika vyombo vya dola ili haki itendeke,” alisema Katibu huyo.

  Aliwataka vijana wa IFM na taasisi nyingine za elimu ya juu kutokubali kutumiwa na vyama hivyo, kwani vina lengo la kuwaharibia misingi ya uzalendo na uongozi wa siku zijazo na kuwataka wadumu ndani ya CCM ambako alidai kuna uzalendo, siasa za amani na utulivu.

  Akijibu juzi tuhuma hizo kwa njia ya simu, Slaa alisema Makala hana elimu na masuala ya utawala na fedha, hivyo anatapatapa hajui anachosema na kumtaka kuweka wazi nyaraka alizonazo, kama kweli ana uhakika nazo kama wanavyofanya wao kwa watu wanaowatuhumu.

  Alisema kama Makala ana ushahidi autoe hadharani, yeye na Mbowe watakuwa tayari kujiuzulu endapo itabainika walikula fedha yoyote, lakini alikiri chama chake kuwa na utaratibu wa kuomba wahisani kusaidia chama, ila si kwa ajili ya baiskeli wala pikipiki.

  Katika hilo la kukiri, alimtuhumu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema mwaka 2005, Swaibu Akwilombe aliyejiunga na CCM, kwamba ndiye aliyetoa nyaraka hizo, lakini alidai walichonacho CCM ni mapendekezo ya maombi kwa wahisani na si majibu ya kile kilichofanyika baadaye.

  “Kama ana ushahidi atoe hadharani, mbona sisi tulitoa wa Mkapa na wengine? Asizungumze tu, shida moja ni kwamba hana elimu na masuala hayo, unajua mtu anaweza kuwa na vyeti lakini hajaelimika, ndiye huyo sasa, aweke mambo hadharani na sisi tutajiuzulu ikibainika ni kweli,” alisema Slaa.

  Slaa aliongeza kusema, “walichonacho ni maandishi ya kuonyesha tunaomba hiki ili tufanye hiki na kile, lakini si kile tulichofanya tangu mwaka huo Julai 2005, mambo mengi tunafanya na mengine ni siri ya chama hatuwezi kusema kila kitu,” alisema Slaa. Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alisema tuhuma hizo ni propaganda za CCM kwani Sh milioni 78 si kitu kwa Mbowe aliyekisaidia chama mwaka 2005 Sh milioni 500 kwa ajili ya shughuli za chama.

  “Hatuna njaa ya Sh milioni 78 kama kuna tuhuma zielekezwe kwa sekretarieti na si Mwenyekiti wetu, hana hiyo njaa, tunamtaka Makala akome kutoa tuhuma hizo, maana ni za kipuuzi, kijinga na propaganda ambazo hazina kichwa wala mguu,” alisema Zitto na kuongeza: “Kama ana ushahidi autoe hadharani kama alivyosema Slaa, maana sisi tulitoa hadharani ushahidi wa Buzwagi, EPA na mingine mingi, anaficha nini, hatuna njaa hata kidogo na wala hana nafasi ya kujibiwa na Katibu Mkuu wetu maana ni mtu mdogo sana huyu.”

  Chanzo: Habari Leo
   
 13. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ORODHA YA MAFISADI
  (LIST OF SHAME)
  Info source: Dr. Wilbroad Slaa - MP (ChaDeMa).

  KANUNI/ VIGEZO VILIVYOTUMIKA

  A.USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
  Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

  B.USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI
  Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii ya Watanzania.

  MISINGI YA KISHERIA/KISIASA YA ORODHA YA MAFISADI

  A.KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka 'Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali' kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:
  (a)Kwamba "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi....";
  (b)Kwamba "lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi"; na
  (c)Kwamba "Serikali itawajibika kwa wananchi...."
  (d)...."
  Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, "... Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
  (a)...
  (b)Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
  (c)Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;
  (d)Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
  (e)...
  (f)...
  (g)...
  (h)Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
  (i)Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
  (j)Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
  (k)...."
  Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa "... Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii ..." ya Katiba. Katiba pia imewapa viongozi wa umma "... wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano." Aidha, viongozi wa umma wamepewa "... wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi...." Vile vile viongozi wote wa umma "watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi nay a pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao."
  Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, viongozi wa umma waliotajwa katika Orodha hii ya Mafisadi walikuwa wanabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:

  B.SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995
  Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili katika utumishi wa umma ambazo:
  (a)Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu wake kama kiongozi wa umma;
  (b)...
  (c)Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa;
  (d)Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.
  Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
  (a)kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali;
  (b)kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;
  (c)kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma;
  (d)kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;
  (e)kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma;
  (f)kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;
  (g)kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
  (h)...
  (i)Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;
  (j)Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi za ajira nje ya utumishi wa umma.

  VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO NA SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KAMA IFUATAVYO:

  A.WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

  1.DR. DAUDI T.S. BALALI
  Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania tangu mwaka 1997. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Gavana Balali amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

  (i)Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu;

  (ii)Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi ya Meremeta Ltd. iliyokuwa inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara. Kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikitoa taarifa za uongo kwamba Meremeta Ltd. ilikuwa ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006. Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005 inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi tarehe 3 Oktoba, 1997. Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd. zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Inajulikana vile vile kwamba Gavana Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005. Hata hivyo, kuna utata mkubwa juu ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba makampuni mawili ya Kiingereza - London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. - nayo yanamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd. Makampuni hayo yanatumia anwani moja iliyoko 84 Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London. Haijulikani ni kwanini Gavana Balali aliruhusu fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali ilikuwa inamiliki hisa 50 tu wakati makampuni mengine ya kigeni yalikuwa yanamiliki hisa 52. Na kama ilivyosema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, uhalali wa Serikali kulipa madeni ya Meremeta Ltd. kwa Nedbank Ltd. badala ya kuiacha benki hiyo kudai malipo hayo kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine haujulikani;

  (iii)Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake Bungeni ya tarehe 27 Juni 2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba "... mali na madeni ya MEREMETA yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja." Hata hivyo, barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007 inatamka wazi kwamba "Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni." Barua hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20 Februari 2006 na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha "majina ya wanahisa wa kampuni na mgawanyo wa hisa." Barua hiyo ya BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F inayohusu usajili wa kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana Balali tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea "Jamhuri ya Mauritius" na anwani yake iko Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na pia leseni ya biashara iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005. nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba, mama, watoto, wajukuu au wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe wa kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika barua yake ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa malipo ya dola za Marekani 13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;

  (iv)Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za Marekani 5,512,398.55 kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co. Ltd. kati ya mwaka 2004 na tarehe 30 Juni 2006. Kati ya fedha hizo, deni la dola 2,807,920 limedhaminiwa kwa dhahabu ghafi ambayo ingenunuliwa kutokana na fedha za mkopo zilizotolewa na Benki Kuu yenyewe! Kwa maana rahisi ni kwamba kampuni ya Mwananchi Gold haijatoa dhamana yoyote inayoeleweka kwa mabilioni ya shilingi ilizokopeshwa na Benki Kuu chini ya Gavana Balali. Kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, hadi kufikia mwezi Desemba 2006 Mwananchi Gold Co. Ltd. ilikuwa imeshindwa kulipa hata riba ya mkopo huo kwa kiasi cha dola za Marekani 62,847.91. "Katika mazingira haya", inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, "hatukuweza kujiridhisha kwamba deni la dola la Marekani 5512398.55 inalodaiwa (Mwananchi Gold Co. Ltd.) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006 linaweza kulipika." Je, ni kampuni gani hii iliyopewa mamilioni ya fedha za umma katika fedha za kigeni bila kudaiwa riba au kupewa kipindi maalumu cha kulipa mkopo huo? Kufuatana na taarifa za BRELA, Mwananchi Gold Co. Ltd. ni kampuni binafsi ambayo wanahisa wake ni Benki Kuu ya Tanzania yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (hisa 500), Mwananchi Trust Co. Ltd. (hisa 1,123) na Chimera Co. Ltd. (hisa 500). Kampuni hii ilisajiliwa kama kampuni binafsi tarehe 12 Desemba 2002. Mawakili wake ni kampuni ya mawakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Associates ikiwashirikisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo marehemu Francis L. Nyalali, Waziri Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa R. Mahalu. Wakurugenzi wa Mwananchi Gold ni Joseph Sinde Warioba, Gavana Daudi Balali, Col. J. Simbakalia, Vulfrida Grace Mahalu, Yusuf H. Mushi na raia wawili wa Italia, Paolo Cesari na Patrizio Magrini. Vulfrida Mahalu ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni binafsi ya VMB Holdings (1996) Ltd. na pia ni mke wa Profesa Mahalu ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Serikali wakati akiwa balozi wa Tanzania nchini Italia! Kanali Simbakalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa na Yusuf Mushi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni binafsi ya Business Machines Consultants (T) Ltd;

  (v) Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. Vile vile Gavana Balali anadaiwa kuidhinisha malipo ya shilingi bilioni 4,228,658,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. "Katika mazingira haya", inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, "hatukuridhika na uhalali wa hasara ya shillingi bilioni 131.9 zinazoonekana katika taarifa za fedha hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006...." Kwa mantiki hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu aliiasa Benki Kuu kuanzisha uchunguzi wa malipo yaliyosababisha hasara ya shilingi 131,950,750,000 na shilingi 4,228,658,000 zilizolipwa kama malipo ya madeni ya nje. Waziri wa Fedha Zakia Meghji mwenyewe amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika akaunti za malipo ya madeni ya nje katika barua yake kwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF). IMF yenyewe katika taarifa kwa vyombo vya habari ya tarehe 27 Juni 2007 imetamka kwamba "Serikali (ya Tanzania) imekwisha kusimamisha malipo kutoka akaunti hiyo hadi uchunguzi huo utakapokamilika." Wakati Serikali ikitoa taarifa hizi kwa IMF imekataa kata kata kutoa taarifa hizi kwa umma wa Watanzania wala wawakilishi wao Bungeni.

  2.ANDREW J. CHENGE
  Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka yote kumi ya utawala wa Rais Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo, Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa "mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria na ... aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria, na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria...." Katika kipindi hicho cha miaka kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

  (i)Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;

  (ii)Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;

  (iii)Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614 wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

  3.BASIL P. MRAMBA
  Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka kumi, Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

  (i)Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa "hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06"! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba "hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani."

  (ii)Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote kuthibitisha kwamba 'Bwana Basil' anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa yakifanyika nje ya nchi. Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na ambaye pia ni waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la 'Basil' ni Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba. Tumemtaka Waziri wa Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu hayo.

  (iii)Mheshimiwa Mramba amehusishwa pia na ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za umma na uuzaji holela wa rasilmali za taifa letu. Kashfa hizo ni pamoja ni ununuzi wa rada ya kijeshi, ununuzi wa ndege ya Rais, na ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB).

  4.GRAY S. MGONJA
  Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.

  5.PATRICK W.R. RUTABANZIBWA
  Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma.

  6.NIMROD ELIREHEMA MKONO
  Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa kampuni ya mawakili ya Mkono & Company Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.
  Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates' Remuneration and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.
  Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, 'Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme' iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: "Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)
  Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: "Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP."

  7.BENJAMIN WILLIAM MKAPA
  Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.

  8.RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
  Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

  Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

  C.SHERIA YA UDHIBITI WA MAKOSA YA KUHUJUMU UCHUMI, 1984
  D.SHERIA YA KUZUIA RUSHWA, 1971 na/au SHERIA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, 2007

  Info source: Dr. Wilbroad Slaa - MP (ChaDeMa).
   
 14. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Amos Makalla sasa amvaa Zitto  na Mwandishi Wetu
  MKURUGENZI wa Idara ya Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makala, amemtaka Naibu Katibu Mkuu na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, (CHADEMA) kuacha porojo na kuzua mambo kwa sababu za kisiasa.

  Makala alitoa kauli hiyo jana, kujibu kauli ya Zitto aliyotoa juzi ya kumtaka amruhusu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua mahesabu ya CCM ili kuthibitisha kama kweli chama hicho hakikuchota fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

  Makalla alisema Zitto aliyejipatia sifa kubwa nchini tangu awe mbunge, katika hoja hiyo, amekuwa polisi, mwendesha mashtaka na hakimu, jambo ambalo alidai si sahihi.

  “Zitto aache kuwadanganya wananchi, CCM haiijui Kagoda, wala haijawahi kuchota fedha za EPA, aache porojo za aina hiyo, hicho kihelehele cha kudai CCM imechota fedha za EPA, kinatoka wapi,?” alihoji Makala.

  Mwanasiasa huyo kijana wa CCM, alisisitiza kuwa hatua ya Zitto kuhusisha wizi wa EPA na chama hicho tawala, si sahihi kwani ni uongo na propaganda za kisiasa zinazofanywa na viongozi wa vyama vya upinzani kwa nia ya kujienga.

  “ Lakini sishangai sana hasa kwa vile Zitto ni kiongozi wa upinzani, hivyo anaweza kutumia nafasi hiyo kujijenga ila kwa kumsaidia, akitaka kujua ukweli, aende ofisi ya msajili, atapata hesabu zote za CCM za miaka hiyo anayosema ambazo zinaonyesha matumizi na mapato ya chama,” alisema Makalla.

  Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Stoo ukiwa ni mfululizo wa mikutano iliyopewa jina la operesheni Sangara katika kijiji la Lamadi juzi, Zitto alisisitiza kuwa CCM iliitumia Kagoda, kuchota fedha za EPA, katika Benki ya Tanzania (BoT).

  Zitto alisema njia pekee ambayo itaweza kuanika uozo ndani ya CCM ni kwa CAG kukagua vitabu vya hesabu za toka mwaka 2005-06 kwa vile miaka hiyo chama hicho kiliweza kuchukua fedha nyingi toka akaunti ya EPA.

  “Namshangaa mno Makalla anasema CCM haihusiki na uchotaji wa fedha nje ilihali kila mmoja anatambua jinsi chama hicho kilivyounda kampuni ya Kagoda Agriculture na kuchota kiasi cha sh bilioni 40 toka Benki Kuu ya Tanzania sasa nani mkweli asipende kudanganya umma” alisema Zitto.

  Katika hilo alisema vyama vya upinzani vinajiandaa kupeleka muswada wa kisheria bungeni ili msajili wa vyama vya siasa awe na nguvu ya kukagua mapato na matumizi ya kila chama.
   
 15. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yule kijana msomi mchakapakazi, Amosi Makala amefanikiwa mpaka sasa kumzidi kete mpinzani wake Suleman Sadiq "Murad". Bwana Makala ambaye amefanikiwa kujijengea jina Mvomero kutokana na uadilifu wake wa kupinga ufisadi katika viwanda miwa vya Mtibwa ambao unamuhusisha pia Rais Mstaafu Benjamini Mkapa. Tofauti na mwenzake Murad, Amos Makala amekuwa akisifiwa kote vijijini kutokana na kuwa upande wa wananchi, anaeleza mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

  Hadi sasa, vita ya wazi katika majimbo ya ubunge imeanza kujitokeza katika jimbo la Mvomero, Mkoani Morogoro ambalo linaongozwa na Suleiman Sadiq 'Murad'. Katika jimbo hilo, msuguano wa wazi, unaonekana kuwa umeanza baina ya Murad na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) Amos Makala(Kwa sasa ni Mweka hazina wa chama hicho) ambaye alibwagwa mwaka 2005 kwa kura 540. Ukweli wa hilo umejitokeza katika ziara ya hivi karibuni aliyoifanya Makala katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo jimbo la Mvomero. Hata hivyo, wakati Makala akieleza kufanya ziara kwa lengo la kuimarisha chama, Murad amekuwa akilalamika ziara hiyo kwa maelezo kuwa kiongozi huyo wa UV-CCM aliingia jimboni humo na kuitisha vikao vya vijana bila wenyeji kujua. Makala aliiambia Mwananchi Jumapili wiki hii kwamba, hakuvamia Mvomero kama anavyovumishiwa na wabaya wake, bali alikwenda kama sehemu ya kuimarisha chama na kusisitiza kuwa kamwe Mvomero haiwezi kuwa kisiwa. "Nilikwenda Mvomero, lakini Murad akasema nimevamia jimboni kwake, sikuvamia, nilitoa taarifa, Mvomero haiwezi kuwa kisiwa, Murad anaogopa kivuli cha uchaguzi," alisema Makala akifafanua kuhusu shutuma hizo. Hata hivyo, Murad naye kama ishara ya kujibu mapigo aliliambia Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, kwamba kwa sasa hahitaji malumbano na Makala kwani amekwisha kulifikisha suala kwa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC). Lakini Murad alithibitisha kauli yake kwamba Makala alifika katika jimbo hilo bila viongozi wengine kufahamu na kutamba kwamba yeye anatekeleza ilani ya chama kwa kaulimbiu ya nguvu, kasi na ari mpya na wala haogopi kivuli cha uchaguzi kwani hadi sasa ni mbunge na ana imani kuwa atashinda tena mwaka 2010. "Lakini labda nikueleze, sasa hivi sihitaji malumbano, hili suala nimesha likabidhi katika Halmashauri Kuu, sasa hivi natekeleza ilani kwa kasi," alisema Murad katika mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi Jumapili.

  .....ndiyohiyo
   
 16. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  MAFISADI wa sisiem utawajua tu. kila mahali wao hupenda kufanya ufisadi na kuchafua hali ya hewa. ....Acha kutupotezea mwelekeo
   
 17. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  MAFISADI wa sisiem utawajua tu. kila mahali wao hupenda kufanya ufisadi na kuchafua hali ya hewa. ....Acha kutupotezea mwelekeo
   
 18. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani wanaJF hii tabia ya kutuhumiana mara Mamluki wa CCM,mara fisadi wa CCM,mara kibaraka wa CCM,mara 'usituchafulie hewa',mara 'usitupotezee mwelekeo' itaisha lini???,maana ikishaonekana mtu anaklwenda kinyume na hoja fulani anaanza kuitwa majina ya ajabuajabu tu ama kupewa tuhuma zisizo na busara,kwa nini tusiheshimu mchango wake jamani???,ifkike kipindi tujikite katika kujibu hoja kwa hoja badala ya tuhuma kama hizi zisizo kuwa na mpango,hasa ukizingatia kwamba JF ni mahali 'where we dare to talk openly',,so tuheshimu mawazo na michango ya wenzetu jamani,tusiiruhusu jazba itutawale....Ni mtizamo tu...Mbarikiwe sana
   
 19. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Huyo Makala aje na uthibitisho wa ufisadi anaouongelea la sivyo ni blaaaa blaaaa za kudanganya jamii isiyojua kupembua pumba na mchele, Makala hata akienda huko kwao Iramba-Nduguti na akasema maneno hayo nadhani watanzania wa leo hawatamuelewa kama anavyodhani yeye achilia mbali wanafunzi hao ambao wanashida na mfumo jeuri wa serikali ya CCM inayoshindwa kuangalia na kuhakikisha watoto wa maskini wanasoma bila bugudha ya kulazimishwa kuchangia
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Makala anatakiwa kwanza aeleze ni kikao gani cha CCM kilipitisha azimio la kuanzisha CCM Trust yenye hisa katika Mwananchi Gold. Kama CCM ilipitisha kwa nini wanahisa wake (CCM Trust) si wadhamini wa CCM bali ni watu wengine wa nje? Akishaelza hayo na kueleweka, nitamuelewa anapoanza kuwavaa wengine kuhusu ufisadi
   
Loading...