mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 324
- 347
Jana na leo taarifa ya mkuu mpya wa mkoa wa Dar esSalaam, Amos Makala kukutana na wazee wa CCM wa mkoa huo zimeenea katika mitandao mbali mbali ya kijamii.
Katika taarifa hiyo Makala amenukuliwa akisema atakuwa anakutana na wazee hao wa chama kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kujadili changamoto za mkoa huo.
Suala la kukutana na wazee si jambo baya kwa kiongozi yeyote wa umma hususan wale waliopewa dhamana ya kumuwakilisha Rais katika maeneo yao.
Ubaya unakuja pale kiongozi huyo anapoamini nafasi yake ni kwa ajili ya kundi fulani pekee kama amabvyo amefanya Makala
Kuamini kuwa wazee wenye mlengo wa CCM tu ndiyo wenye kubeba changamoto za wazee wote wa Dar esSalaam, ni kutowatendea haki wazee na wakazi wa Dar kwa ujumla tena kwa kutumia ofisi ya serikali ambayo inatakiwa kuwa wazi wakati wote kupokea na kusikiliza ushauri wa wananchi wote bila kujali kada zao.
Leo hii Makala anatumia ofisi na bajeti ya serikali kukutana na wazee wa chama pekee,ilihali nafasi hiyo ya kichama wazee hao wangetumia kujadili mustakabali wao kwa viongozi wa chama kabla ya kufika serikalini.
Uamuzi huo wa Kibaguzi wa Makala ni tofauti na dhamira nzuri ya Rais Wetu Samia Suluhu Hassan ya kutobagua watanzania kwa itikadi zao.
Rais amewateua wasaidizi wake akiamini watakuwa wamejua dhamira yake lakini kwa haraka sana Amos Makala ameshindwa ama kwa kutojua au kwa kujua kuwa falsafa yake ya kutumia ofisi ya umma kibaguzi, hailingani na matamanio ya Rais