Kwa kweli mkuu wa mkoa wa Mbeya ana matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Taarifa zilizotufikia hivi sasa kutoka huko Moshi ni kuwa amewaalika waandishi wa habari ambao aliwateua wawe wakifanya kazi zake kwenda kumtembelea huko Mbeya alikohamishiwa na rais Magufuli.
Taarifa ni kuwa Makala amelipia gharama zote za waandishi hao ambao ni wengi lengo ni kuwapongeza kwa kumuandika vizuri mpaka rais akambakisha kazini.
Taarifa ni kuwa kila mmoja wa waandishi hao maarufu kama timu Makala Kilimanjaro, ambao idadi yao haijajulikana ni kuwa atapata shilingi milioni moja kwa kwenda kutalii tu huko jiji la Mbeya.
Ikumbukwe wakati akiwa Kilimanjaro, Makala alikuwa akilaumiwa kichinichini kwa kuwalazimisha wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo wawalipe waandishi aliokuwa akiandamana nao, leo anawalipa fadhila kwa kuwaalika waende kumtembelea huko Mbeya kwa gharama za serikali, hivi wakuu wote wa mikoa wangefanya hivyo hii nchi itakuwaje?
Hebu fikiria kuwasafirisha waandishi wote hao na taarifa ni kwamba kila mmoja atalipwa shilingi milioni 1 katika safari hiyo mbali na malazi na chakula gharama ambazo pengine halmashauri za huko Mbeya ndiyo zitawalipa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala.