Amon Mpenja, sio dhambi kwa asasi za kiraia kutoa elimu kwa mpiga kura wa Tanzania

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,013
Kumekucha mapambano yanaendelea . mapambano kati ya wapenda haki na usawa na wasiopenda haki.

Nimekusikia bwana Amoni Mpenja, Naibu katibu mkuu wizara ya sharia kupitia ITV ukisema ni marufuku kwa asasi za kiraia na NGO kutoa elimu kwa mpigakura wa Tanzania. Tena ukasema utazifuta milele na umezitaja taasisi zitoazo msaada wa kisheria.

Tunajua kwamba mashirika makini kama Kituo cha sharia na haki za binaadamu mumeyanyima vibali makusudi kama mlivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019. Kiroja ni pale tume ya uchaguzi inapochagua MAREFA yaani waangalizi na watoa elimu kwa wapigakura. mkawambia wachague vishirika laini visivyohata na watumishi wala pesa za kufika maeneo yote ya nchi, lengo lenu muibe KURA Vizuri ili mseme CCM inakubalika labda kwa mazuzu.

Katika katazo lako hujasema mpigakura akiwa na elimu ya kutosha juu ya zoezi lenyewe serikali inapata hasara gani? wewe umeishia kwenye kutoa vitisho vya Kuchafuka kwa Amani na nchi kusambaratika kwa lipi hasa? kwa watu kuwa na elimu ya mpigakura?

Wananchi wanajua nguvu ya CCM unayoitumikia wewe ni ujinga wa watanzania.kwamba Eti unanunua mindege iso na Tija kwa kodi zao kisha unajisifu kana kwamba pesa umetoa mfukoni pako, kwamba tunakatwa pesa kuchangia umemme wa REA kisha jitu linajisifu kwamba linapeleka umeme vijijini, kwamba zahanati zinajengwa kwa pesa zetu lenyewe linasema ni hisani toka moyoni mwake, watoto wanakaa chini ati kuna elimu bure nk.

Ndugu MPENJA nitasema na kusema tena kwamba kuzikataza asasi hizi kutoa elimu kwa wapiga kura ni ubinafsi na uwoga wa bure kama kukataza bunge live huku nyie mkimulikwa na Makamera hata mkienda kusali nk, ni sawa na kukataza mikutano ya vyama huku nyie mnafanya ati mwakagua miradi, sawa na kuzuia wenzenu kutangaza nia wakati nyie mlitangaza tangu siku ya kwanza hapo ikulu.

Haitoshi tu kuzikataza asasi tuelezwe zikitoa elimu kwa mpiga kura wa Mahenge au Liwale Amani inavurugika vipi? na kwanini NEC ndiyo wapewe idhini ya kuteua asasi za kutoa elimu wakati wao ndiyo wanaangaliwa? yaani ni sawa na ile kauli ya yule msemaji/MROPOKAJI wa klabu moja kubwa ya mpira hapa nchini ati kwamba timu yake isingecheza na timu fulani pinzani mpaka refa atoke nje ya nchi. unachaguaje refa wa kuchezesha mechi yako mwenyewe?

Kiroja ni kwamba chama kinachojisifu kupendwa na kuleta maendeleo kwa wanaoitwa WANYONGE ndicho kinachoogopa hao WANYONGE wenyewe wasiamke? siku wanyonge wakiamka hamtaweza kutoa kauli za vitisho na kifedhuli kama hizi au kama zile za IGP kwamba wananchi wasichague vyama vya hovyohovyo. sijui ni nani wa hovyohovyo kati ya SIRRO na wananchi?
wasalaam.

Ndimi mwanadarasa mwenzio (UDSM)-2000s
 
Back
Top Bottom