#COVID19 Amnesty International wanajaribu kuishinikiza Tanzania kununua chanjo ya Covid-19

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,661
18,035
Ukitembelea tovuti ya Amnesty International ukurasa wa Tanzania utakuta wamebandika andiko wakitaka kamati iliyoundwa ya corona itumike kuhakikisha kuwa Watanzania wanachanjwa chanjo ya corona.

Kinachonishangaza ni kuwa mataifa ya nje yanaongeza sana shinikizo kwa mama kuhusu corona. Wanaingia na gia ya kumsifu na kumponda Hayati Magufuli kuhusu alivyoshughulika na corona. Wanamtaka afuate sayansi na kuachana na kuamini hadithi wao wanaita "myths"!!!

Hawa inabidi tuwaambie wazi kuwa kumtanguliza Mungu siyo kuamini hadithi. Tanzania haikudharau sayansi Bali ilimtanguliza Mungu mbele ya sayansi. Chonde chonde huu utaratibu usivurugwe. Mungu amejibu maombi yetu kwa sababu tulimheshimu kwa wazi na dunia yote ikasikia. Akaamua kutuponya kwa rehema zake na kwa kulitetea Jina lake mbele ya mataifa!

Si kwamba watanzania ndio tumekuwa wema sana mbele za Mungu! Tukibatilisha hii heshima tuliyompa na kuamua kutanguliza mawazo ya mabeberu wanaotanguliza "sayansi" na kumweka Mungu pembeni, tutakutana na yanayowakuta waliofuata mwelekeo huo!! India ni Taifa LA kwanza duniani kwa kuzalizasha chanjo kwa wingi zaidi lakini hilo halijawasaidia!! Marekani wana chanjo za ziada kwa mamilioni, lakini ndilo linaloongoza kwa kufa na corona!

Tanzania tuko salama hadi sasa mpaka wanashangaa!! Wao wameamua kuabudu sayansi sisi tumeamua kumtanguliza na kumwamini Mungu kuwa atatuokoa ma korona.

Mabeberu wamekuwa wakimsimgizia marehemu Magufuli kuwa alikataa uwepo wa corona. Siyo kweli! Alitambua uwepo wa corona lakini alitumia mbinu tofauti ya kukabiliana nayo. Yeye alikataa kuiga mbinu za mabeberu na akaamua kumtamguliza Mungu kwa kuitisha maombi! Dunia nzima japo wanakataa kukiri lakini wameshuhudia Tanzania tumekuwa salama dhidi ya corona ukilinganisha na mataifa mengine ikiwa ni yale yanayotaka kuiba utukufu wa Mungu kwa kushinikiza tufuate mbinu zao ili waseme ndizo zilizotuokoa vinginevyo tungeisha!

Naomba niwakumbushe: walisema Tanzania tumekataa lockdown tutaokota miili barabarani!! Hilo halijatokea! Mataifa mengi wimbi la pili na la tatu la corona limekuwa la hatari zaidi na wengi wamekufa na mpaka sasa wanakufa! Sisi Tanzania wimbi la pili halikuwa na nguvu Kabisa ndio maana hata shule hatukufunga! Wakati wa maombolezo ya Rais Magufuli watanzania kwa mamilioni walijitokeza kumuaga kwa mamilioni na kusongamana bila barakoa!!

Wakasema baada ya wiki mbili tutaanza kuokota miili barabarani maana tutakuwa tumeambukizana sana!! Haikutokea!! Watuache! Wasitupangie wala wasimshinikize mama kwa habari ya chanjo ya corona.

Yamewashinda kwao wasiwe wataalamu wa kutusaidia sisi.

RAI yangu: Kama wanataka kutusaidia basi watupe pesa za kumalizia SGR na Stigler's George! Nawasilisha!
 
Mnataka wangapi wafe ndiyo msikilize tumepoteza mpaka viongozi wa juu kabisa!!! mnashindia kusema mebeberu tulete chanjo na kupata iwe hiari tatizo liko wapi? wengine tuna wazazi wanataka chanjo.

Hatuwezi kuwanyima watanzania wote chanjo kwa mawazo ya wachache! na haziuzwi madukani au hospitalini! Mimi binafsi nimepigwa chanjo March 5, 2021 sina tatizo lolote mpala leo!
 
Tatizo hamueleweki, chagueni moja. Hamtaki modern medicines, acheni kila kitu sio chanjo ya polio mnataka, nyingine hamtaki.

Ubishi ndio jadi yetu, hata UKIMWI ulivyoingia tulikuwa wabishi, mpaka tulivyoanza kuzika watu wana kilo 5 ndio akili zikakubali.

Tujipe muda tutaona
 
Je ipi ni busara ,kufunga mlango wa nyumba yako kabla majambazi hayajakuingilia ndani au baada ya majambazi kukingilia?

Tumia akili kuchunga Afya yako!
Hakuna anayesema hivyo. Ila kuhusu corona hiyo chanjo tayari ilishapitwa na wakati! Hiyo chanjo ilitengenezwa ili kudhibiti kirusi cha corona kama kilovyokuwa make 2019.

Leo kimeshabadilika mara nyingi! Kinachotafutwa kwa sasa ni pesa basi. Lakini pia imedhihirika hiyo chanjo ina madhara maana imetengenezwa kwa mwendo kama wala hakuna ajuaye athari zake za muda mrefu!
 
Mnataka wangapi wafe ndiyo msikilize tumepoteza mpaka viongozi wa juu kabisa!!! mnashindia kusema mebeberu tulete chanjo na kupata iwe hiari tatizo liko wapi? wengine tuna wazazi wanataka chanjo. Hatuwezi kuwanyima watanzania wote chanjo kwa mawazo ya wachache! na haziuzwi madukani au hospitalini! Mimi binafsi nimepigwa chanjo March 5, 2021 sina tatizo lolote mpala leo!
Nani kakuambia kuwa hao walioanza kuchanjwa hakuna vifo nchini kwao? Ingia worldometer uone jinsi watu walivyokufa huko Mauretania, Uingereza, India na kwingineko!
 
Tatizo hamueleweki, chagueni moja. Hamtaki modern medicines, acheni kila kitu sio chanjo ya polio mnataka, nyingine hamtaki.

Ubishi ndio jadi yetu, hata UKIMWI ulivyoingia tulikuwa wabishi, mpaka tulivyoanza kuzika watu wana kilo 5 ndio akili zikakubali.

Tujipe muda tutaona
Hakuna aliyesema hatutaki dawa wala chanjo nyingine. Ila hi ya corona haijafanyiwa utafiti wa kutosha na madhara yake tayari yameanza kuonekana! Hakuna ajuaye madhara ya muda mrefu ya hii chanjo! UK
 
Nani kakuambia kuwa hao walioanza kuchanjwa hakuna vifo nchini kwao ? India worldometer uone jinsi watu walivyokufa huko mauretania, uingereza, India na kwingineko!

Hakuna hata mtu mmoja aliye chanjwa amekufa kwenye Dunia hii mpaka leo. Hapa US wamechanja zaidi ya watu milioni 150 hakuna hata mmoja kafa au kulazwa. Kuna chanjo moja tu ya kampuni ya J& J ambayo wanawake sita waliumwa kati ya milioni 7 waliochanjwa lakini wote wazima . India wamechanja wachache sana mnaona yanayotokea kule
 
Muda huu wanajifanya wanatupenda sana! Kama wana nia njema watusaidie kumalizia reli ya standard gauge na mradi wa umeme wa Stiglers George!

Hivi mnakumbuka jinsi walivyoupiga vita mradi wa umeme wa Stiglers Gorge? Haya mapenzi ya Ghafla yametoka wapi?
Wasitupangie!
 
Hakuna hata mtu mmoja aliye chanjwa amekufa kwenye Dunia hii mpaka leo. Hapa US wamechanja zaidi ya watu milioni 150 hakuna hata mmoja kafa au kulazwa. Kuna chanjo moja tu ya kampuni ya J& J ambayo wanawake sita waliumwa kati ya milioni 7 waliochanjwa lakini wot wazima . India wamechanja wachache sana mnaona yanayotokea kule
Uko nyuma ya wakati!
 
Mnataka wangapi wafe ndiyo msikilize tumepoteza mpaka viongozi wa juu kabisa!!! mnashindia kusema mebeberu tulete chanjo na kupata iwe hiari tatizo liko wapi? wengine tuna wazazi wanataka chanjo.

Hatuwezi kuwanyima watanzania wote chanjo kwa mawazo ya wachache! na haziuzwi madukani au hospitalini! Mimi binafsi nimepigwa chanjo March 5, 2021 sina tatizo lolote mpala leo!
100% Watuletee Wasiotaka Wakae pembeni. Hatutaki ujinga wa Kutotumia sayansi ktk kusolve tatizo la Kiafya. Ukweli ni Kwamba hapa Bongo COVID -19 Imeramba watu wengi hadi pale kwenye Dalini. So walete asiyetaka asilazimishwe anayetaka basi ajikinge.
 
Back
Top Bottom