Amnesty International and Human Rights Watch: Hali ya ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani waongezeka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
AMNESTY INTERNATIONAL HUMAN RIGHTS WATCH
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ukandamizaji wa vyombo vya habari, watetezi wa haki za binadamu na vyama vya upinzani umeongezeka tangu mwaka 2015, zinasema ripoti mbili tofauti za mashirika ya Amnesty International na Human Rights Watch zilizotolewa leo kwa pamoja.

Ripoti zote mbili zinaeleza kwamba serikali ya Rais John Magufuli imepitisha au kutumia sheria nyingi zinazozuia uandishi huru wa habari na kuminya kwa kiasi kikubwa shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali na vyama vya siasa vya upinzani.

“Akiwa anatimiza miaka minne madarakani mwezi ujao, Rais Magufuli anapaswa kuangalia kwa makini rekodi yake ya kutumbua mfumo wa haki za binadamu nchini mwake. Serikali yake inapaswa kufuta sheria zote kandamizi zinazotumika kuminya mawazo tofauti, na isitishe kwa haraka ukiukwaji wa haki za binadamu,” alisema Roland Ebole, Mtafiti wa Tanzania wa Amnesty International.

“Sera na hatua za kupinga mabadiliko za serikali zimezuia vyombo vya habari, zimepandikiza hofu kati ya asasi za kiraia na kuminya shughuli za vyama vya siasa katika kipindi cha kuelekea chaguzi,” alisema Oryem Nyeko, mtafiti wa Afrika katika shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch. “Ukiwa umebakia mwaka mmoja tu, serikali hii inapaswa kurekebisha mwenendo huu wa ukiukwaji na ioneshe nia ya dhati ya kulinda haki ya uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika kwa amani kama inavyoelezwa katika katiba na katika mikataba ya haki za binadamu ambayo Tanzania ni mwanachama.”

Ripoti ya shirika la Amnesty International, yenye jina “The price we pay: Targeted for dissent by the Tanzanian State” [Gharama tunayolipa: Kulengwa na serikali ya Tanzania kwa sababu ya upinzani wa mawazo] na ile ya shirika la Human Rights Watch, yenye jina “As long as I am quiet, I am safe: Threats to Independent Media and Civil Society in Tanzania” [Kadri niwavyokuwa kimya, ninakuwa salama:

Vitisho dhidi ya Vyombo Huru vya Habari na Asasi za Kiraia nchini Tanzania] zilifanyiwa utafiti na kuandikwa kwa nyakati tofauti lakini matokeo yake yanafanana.

Shirika la Human Rights Watch lilihoji watu 80 wakiwemo waandishi wa habari, wamiliki wa blogu, wanasheria, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wanachama wa vyama vya siasa. Shirika la Amnesty International lilihoji watu 68 wakiwemo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kiserikali ya kimataifa, wanasheria, wanataaluma, viongozi wa dini, na mabalozi, na kupitia hukumu za mahakama, sheria za nchi, taarifa na amri za serikali.

Waligundua kwamba Rais na viongozi waandamizi wa serikali mara nyingi walitoa matamshi yanayopinga haki za binadamu, ambayo wakati mwingine yalifuatiwa na kuwachukulia hatua watu binafsi na mashirika. Matamshi hayo, yanayoenda sambamba na kukamatwa kiholela na vitisho vya kufuta usajili wa vikundi visivyo vya kiserikali, yamezuia utoaji huru wa ripoti wa waandishi wa habari na mijadala ya kijamii kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu kabla ya chaguzi zijazo.

Mashirika yote mawili yaligundua kwamba serikali ya Tanzania inadhoofisha haki ya uhuru wa kujieleza na kujumuika kwa kutekeleza sheria na kanuni kandamizi mpya na zilizopo ambazo ni kandamizi kuhusu waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na vyama vya siasa.

Tangu mwaka 2015, serikali imeongeza udhibiti kwa kupiga marufuku au kusimamisha kwa muda magazeti yapatayo angalau matano yaliyoandika habari zilizoonekana ni za kukosoa. Magazeti hayo ni pamoja na gazeti kubwa la Tanzania litolewalo kila siku kwa lugha ya Kiingereza, The Citizen, mwaka 2019, na mengine manne mwaka 2017. Tume ya Utangazaji Zanzibar pia ilikifungia kituo cha redio, Swahiba FM, mwezi Oktoba 2015 kwa sababu kilitangaza kufutwa na hatimaye kurudiwa upya kwa chaguzi za mwaka 2015.

Serikali ilitumia Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kuwafungulia mashtaka waandishi wa habari na wanaharakati kwa jumbe zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii. Mnamo mwezi Novemba 2017, mahakama moja katika mji mkuu, Dar es Salaam ilimtia hatiani Bob Chacha Wangwe, mwanaharakati wa haki za binadamu kwa “kuchapisha habari za uongo,” chini ya sheria hii kwa sababu aliitaja Zanzibar kuwa ni koloni la Tanzania bara katika chapisho lake la Facebook. Hukumu yake ilitenguliwa na Mahakama Kuu kwa misingi kwamba mahakama ya chini haikuwa imeweka bayana vipengele vya kosa husika.

Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Kimtandao), zilizopitishwa mwaka 2018, zinamtaka mmiliki yeyote wa blogu au tovuti kulipa ada kubwa ya leseni ya hadi Shilingi milioni 2.1 za kitanzania (zaidi ya Dola za kimarekani 900). Sheria hii pia inaminya maudhui ya mtandaoni na kuruhusu uchunguzi wa migahawa ya intaneti bila uangalizi wa kimahakama.

Serikali ya Tanzania pia inadhibiti utafiti huru na upatikanaji kwa watu wote wa takwimu za kujitegemea kwa kutumia Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, jambo ambalo linawanyima wananchi vyanzo mbadala vya taarifa zilizothibitishwa. Wakati marekebisho yaliyofanyika kwenye sheria hiyo mwaka huu yaliondoa kipengele cha kosa la jinai kwa kuchapisha takwimu zisizokuwa za serikali, serikali bado inadhibiti nani anaweza kukusanya na kusambaza taarifa za kitakwimu na kuamua zipi ni za kweli au za uongo.

“Tunaona kuongezeka kunakotisha kwa matendo ya ukandamizaji nchini Tanzania. Serikali inawanyima wananchi haki yao ya kupata taarifa kwa kutoa ule “ukweli” tu unaoidhinishwa na serikali,” alisema Roland Ebole.

Mwaka 2018, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ililizuia Shirika la Twaweza la nchini Tanzania kuchapisha utafiti wa Sauti za Wananchi, ambao uligundua kuwa kiwango cha Rais Magufuli kuungwa mkono na wananchi kilikuwa kimeshuka kwa kiasi kikubwa. Mwaka 2017 COSTECH na Wizara ya Mambo ya Ndani walilizuia shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kufanya mkutano na waandishi wa habari ili kutangaza ripoti yake inayoelezea kwa kina unyanyasaji wa wafanyakazi wa ndani kutoka Tanzania huko nchini Oman na katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Mnamo mwezi Januari 2019, Bunge liliifanyia marekebisho Sheria ya Vyama vya Siasa na kuingiza vipengele vingi vinavyominya haki za uhuru wa kujumuika na kukusanyika kwa amani. Marekebisho hayo yalimpa madaraka makubwa Msajili wa Vyama vya Siasa kufuta usajili wa vyama, kudai taarifa kutoka vyama vya siasa, na kusimamisha uanachama wa wanachama. Marekebisho hayo pia yaliingiza kipengele kipya kinacho yataka mashirika na watu binafsi kupata idhini kabla ya kutoa elimu ya uraia, jambo linalominya haki ya raia ya kupata taarifa.

Mwezi Julai 2016, Rais Magufuli alitangaza katazo la jumla la shughuli za kisiasa hadi 2020, ikiwa ni kinyume na sheria za nchi. Katazo hilo limetumika kibaguzi dhidi ya wanasiasa wa upinzani, baadhi yao wakiwa wamekamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uongo. Mwaka 2017, watu wasiojulikana walimpiga risasi Mbunge wa upinzani Tundu Lissu, na mwaka 2018, watu wasiojulikana waliwaua viongozi wawili wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, Daniel John na Godfrey Luena. Ingawa polisi wanasema wanapeleleza mauaji haya, hadi sasa, hakuna aliyetiwa mbaroni.

“Serikali ya Tanzania lazima ifute mara moja na bila masharti mashtaka yote dhidi ya waandishi wa habari na wanasiasa wanaoshtakiwa kwa sababu tu ya kutimiza haki yao ya uhuru wa kujieleza na kujumuika,” yalisema mashirika ya Amnesty International na Human Rights Watch.

--MWISHO--
READ HR’s report: “As Long as I am Quiet, I am Safe” | Threats to Independent Media and Civil Society in Tanzania
 

Attachments

  • AFR 56.0301.2019 The price we pay ENG.pdf
    2 MB · Views: 1
  • Tanzania Report 28Oct_FINAL.doc
    56.5 KB · Views: 2
Last edited:
Huwezi amini kuna wakati hii nchi ilikuwa inaongozwa na Rais Nyerere na tulikuwa mstari wa mbele kupambana ili wengine wapate haki zao za kibinadamu. Huwezi amini sasa hivi tuna aspire kuwa Police State.

Anyways! ndege nyingine zinakuja lini twende airport kusikiliza hotuba.
 
Siku hizi hata mkiwa mnakunywa bia ukianza kuisema serikali watu wanakulazimisha uongee kwa sauti ya chini chini! haya mambo hayakuwepo haya!

Kwa sisi tusioogopa kitu ukiendlelea kuongea unaona jamaa wanasepa mmoja mmoja!

Ndo nchi ilipofika hapa. Na kwa taarifa yenu taarifa hii haitachapishwa gazeti lolote la kesho wala kusikia kwenye TV.
 
Sasa kwa nini mtu mmoja anafanya watu waishi kama wafungwa wakati mahakama ya kimataifa inaweza kusaidia tukapata katiba mpya ambayo kila mtanzania ataifaidi? (Yaani kiongozi sio mtawala na mwananchi sio mtawaliwa).

Majaji wenyewe wamekiri na wanajitahidi lakini wengine wanaishia kupokea rushwa ya pesa na vyeo.

The Hegg embu na nyinyi njooni humu jamvin mtoe mada msikie wenyewe hali ya wananchi au mtume watu wapite hata mikoa minne tu msikie kilio chao ili muokoe roho za watu mapema.

Lengo tuwe na tume ya uchaguzi na katiba huru kwa wananchi.

Tutoe pongezi kwa hawa viongozi wa Haki za binadamu na wenzao kwa kuwakumbusha walengwa.
 
Eti sheria zote zifutwe. Wakati hizo sheria hazipo je zilitusaidia kuleta maendeleo kama haya yanayofanywa na serikali ya JPM.

Tena nashauri ziongezwe sheria na zipewe ukali zaidi ili wapuuzi wachache kama waliomzushia kifo Mh. Rais wakamatwe vinzuri na kupewa adhabu kali.

Ni ujinga kuendekeza the so called uhuru usiokuwa na mipaka.
 
Fasta fasta,
Kabla hamjatoa hizi comment muwe mnaangalia hizo nchi mnazoshabikia zinafanya mabaya mangapi na hawaguswi na the so called Mahakama ya Kimataifa. Libya imefanywa nini na je walioifanya hivyo wamechukuliwa hatua gani?

Iraq, Afghanstan na nchi nyingine nyingi tu wameziharibu lakini kimya. Huko huko Marekani watu weusi wanauwawa mchana kweupe lakini haya yanayojiita mashirika ya upuuzi yamekaa kimya wala darubini zao hazimuliki huko.
 
CodeDesigner,
Swala la sheria sio la upande mmoja ni kwa pande zote Serikali na Wanachi kwa pamoja kuzingatia sheria na kanuni. Hivyo wote Ni muhimu kufuata sheria na sio kukandamiza upande mmoja
 
Waambieni hao amnesty international human rights watch kuwa waende spain wakawasaidie wale viongozi wa catalonia wanaotaka kujitenga walioko ndani mpaka sasa watoke ndo waje huku tz na izo haki za wazitakazo.

Kama wanashindwa kuwaambia ukweli wazungu basi wafunge mabakuli yao mana hayana maana yoyote kwetu zaidi ya kumpigia mbuzi gitaa
 
Back
Top Bottom