Ammy Ninje kutangazwa, kumrithi Salum Mayanga. Kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars na kuipeleka Kenya

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
AMI NINJE KUTANGAZWA KOCHA MKUU WA KILIMANJARO STARS, KWENDA NA TIMU KENYA, AKIFANYA VIZUIRI HUWENDA AKARITHI MIKOBA YA MAYANJA

kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), WILFRED KIDAU, leo tarehe 17/11/2017 anatarajia kumtangaza kocha msaidizi wa Taifa Stars, AMI NINJE kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars. Ninje ataiongoza Kilimanjaro Stars kwenye mashindano ya CECAFA yanayotarajiwa kuanza Jijini Nairobi kuanzia Novemba 25, 2017.

Taarifa zaidi zinasema, endapo NINJE atafanya. vizuri katika michuano hiyo, anatarajiwa kuridhi mikoba ya Kocha wa sasa wa Taifa Stars, SALUM MAYANGA ambaye pamoja na kufanya vizuri tangu ateuliwe kuinoa Taifa Stars 14/01/2017 siyo chaguo la Uongozi wa sasa wa TFF kutokana na kuteuliwa na uongozi uliopita.
Katika mechi 14 ambazo Taifa Stars imecheza chini ya Kocha Mayanga imeshinda mechi 6, imetoka sare mechi 7 na kufungwa mechi moja.

Mytake: Kutaka kumuondoa Kocha Mayanga wakati akiwa na matokeo mazuri kiasi hiki ni kutomtendea haki, kutolitakia mema soka la Tanzania na kuendeleza mchezo ule ule wa kutanguliza maslahi binafsi na kubebana bila kujali athari zake kwa wadau wa soka na soka lenyewe
 
Kweli kiongozi kabisa Manyanga hajafanya vibaya sana.Ni mijungu tuu ndio itamuondoa pale
 
Kuna timu mbili hapo Kilimanjaro Stars na Taifa stars
Nafikiri Tff wangeweka sawa hili Suala Je Mayanga atabaki kuwa kocha wa Taifa Stars au anapangiwa kazi nyingine?
 
TFF wabaguzi timu angepewa Mwambusi ana medals za VPL......mnatukosea sana
 
Huyu jamaa ana leseni A ya FIFA. Alipiga kazi pale Nottigham County FC nchini uingereza. Amecheza South Africa, Norway, America na Uingereza..

Safi sana Ammy...Ila level zake ni za kufundisha Azam, Simba na Yanga. Kocha mkubwa!
 
Back
Top Bottom