Amka Kijana

seif_tanzania

Member
Nov 23, 2017
13
45
Imeaandaliwa na ndugu IDDY SEIF HARUNA

Tanzania oooh Tanzania kila mmoja wetu ni shahidi juu ya hili tunaelekea katika maadhimisho ya 56 ya sherehe za Uhuru nchini. Lakini lazima tuwe na maswalii juu ya kujibu kuhusiana na Uhuru wetu

1. Je Uhuru tuliopata tumeufanyia nini?
Leo naandika makala haya nikitizamia miaka 56 ya Uhuru VIJANA tumefanya nini?
Siasa ni mchezo mchafu ambao umekuwa ukipoteza wingi wa vijana katika taifa hili wenye uwezo fikra ya kinifu za kimaendeleo na uzalendo badala yake wamebaki wakiishi chini ya cheni ya utumwa wa kisiasi

Vijana wengi wamekuwa wakitumiwa kufanya kazi na kupambana kutimiza ndoto za watu wengine pasipo kuangalia ndoto zao. Vijana wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuhama katika vyama tofauti vya kisiasa pasipo kujua au kugundua dira na misingi yakinifu ya kimaisha yao. Vijana ni miaka 56 sasa ya sherehe za Uhuru lakini bado hawajatambu fika na vyema wao ni kina nanii..? wanatakiwa kufanya nini? na ni kwa wakati gani?..

Sera ya UZALENDO sasa kwa wingi wa vijana katika taifa hili imegeuzwa ni mtaji wamekuwa wakikesha kwenye mitandao ya kijamii kuamasisha uzalendo lakini sio ule uzalendo alikuwa akiusema Baba wa Taifa Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE wao wameona kueneza kwa njia yao ya kiutofauti ili waweze kuonekana na kutengeneza majina yao na kupambana kutafuta nafasi ya uongozi katika taifa hili

Vijana ni miaka 56 ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru lakini wengi wanaelimu kutoka vyuo vikubwa duniania lakini wamekuwa wakitazamia kupata nafasi za uongozi katika taifa hili na kujiung kwenye vyama vya siasa ili waweze kuonekana lakini wanashindwa kutumia tunu ya ujuzi walionao kwa ajili ya kulijenga taifa na kujiajiri ili kupunguza kero ya ajira katika taifa hili

Ni miaka 56 ya sherehe za maadhimisho ya Uhuru lakini vijana bado hatujui tunaenda wapii huu ni wakati wa kujikomboa wenyewe kujenga mipango endelevu kupinga na kuepuka kero za wanasiasa ili tuweze kulijenga taifa letu

AMKA VIJANA
AMKA TANZANIA

Imeaandaliwa tarehe 07.12.2017
Na ndugu IDDY SEIF HARUNA
 

Msangarufu

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,182
2,000
Seif Haruna
Ni hatua gani sasa umechukua kwa lengo la kubadili vijana wenzako kufikia mafanikio na kufaidi uhuru unaouongelea

Vijana wenzako uliosoma nao Himo na Korona anza nao kwanza kabla ya kuja hapa jukwaani

Naamini walioko jamii forum asilimia 70 wanaelimu nzuri tuu na maisha mazuri tuu sio kama wale vijana wengi uliomaliza nao mieresini ambao bhang ndio kimbilio

Anza nao kwanza wale Wanahitaji msaada mkubwa sana ndugu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom