Amini Uwezo Wake tu!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
Amini Uwezo Wake tu!

Kama kunyesha mvua siku ya harusi yako ni baraka basi hawa maharusi kutakuwa kulikuwa na mafuriko maana maharusi wanafanana, huwa sichoki kutazama hii picha.

Watafiti Wanasema kwamba ukiona kosa moja kwa mke wako au mume wako, hutakiwa kuliangalia na kuliwekea sura kamili au hutakiwi kulipa uhai badala yake lipe jina na liweke kando kwa jaribu kulinganisha na uzuri wake au mambo matano mazuri kuhusu yeye (positive traits).


Kwa mfano unajikuta mume wako au mke wako amewaka hasira kwa jambo dogo tu hadi unahisi dunia umebadili mwelekeo, hata hivyo badala ya kuanza kufikiria hizo hasira zake Unachotakiwa kufanya ni kujiambia mwenyewe kwamba:

“ Ni kweli ana hasira hata hivyo ni mwanamke/mwanaume anayenijali, anayenipenda, anayewajibika, ni mbunifu na anajua kuniridhisha chumbani”.



Kumbuka strongest relationships ni zile ambazo partners wanaweza kujenga picha ya uzuri wa mwenzake (idealized/illusioned) kuhusu uwezo wake na si udhaifu.


Kwa kuufuta udhaifu au kuondoa mawazo kuhusu udhaifu wake na kuweka uwezo wake au uimara wake (strength) unahusanisha information muhimu za kufanya mke wako au mume wako awe mzuri zaidi na ukampenda zaidi.


Kwa miaka zaidi ya 100 hekima na busara iliyodumu na ambayo hata wengine wanaamini ni ile kwamba kinyume cha uzuri ni ubaya.

Hii ina maana kwamba Ukitaka kujua uzuri wa kitu basi unatafuta ubaya wake kwanza.

Ukitaka kujua furaha ni kitu gani au ina thamani kiasi gani unajaribu kumchunguza mtu mwenye huzuni kwanza.

Watoto ambao wanatumia madawa ya kulevya hutumika kujua namna ya kuwalinda watoto wasiotumia madawa ya kulevya wasijiingize kwenye hivyo vitendo.


Watoto ambao ni watoro shuleni hutumika kujifunza kuwafanya watoto wengine wawe na mahudhurio mazuri.


Linapokuja suala la ndoa si kweli kwamba ili kujifunza ndoa kuwa nzuri au kusiwe na talaka basi ni vizuri kujifunza ndoa ovyo au ndoa ambazo zimeishia kwenye talaka.


“Bad is not always the opposite of good”


Ukweli ni kwamba linapokuja suala la ndoa Ukitaka kujenga ndoa nzuri au imara unahitaji kujifunza kutoka ndoa imara na si ndoa ovyo au zile zimeishia kwenye talaka.


Vitu vinavyopatikana kwenye ndoa imara havina uhusiano na vitu vilivyosababisha ndoa ovyo kuwa ovyo kwani ndoa imara zina siri yake ambayo si kinyume cha ndoa ovyo.


Ndoa imara ni zile ambazo mwanandoa mmoja au wote huwa na picha kamili ya mwenzi wake, huwa na sifa ambazo amezijenga kwa mwenzi wake ambazo ukweli ni kwamba inawezekana kwamba mwenzi wake hana ila yeye huamini anazo na ni kuwa positive kwamba anamfaa.

Ndoa imara na zinazodumu ni zile ambazo mwanandoa huamini katika uimara au uwezo wa mke wake au mume wake hata kama huo uwezo hana.

Unaweza kuona kama ni utani au contradiction hata hivyo ndio ukweli.


Nina amini mke wangu ni caring, nina amini mke wangu ni sweetie, nina amini mke wangu ananifaa, nina amini mke wangu ni mzuri, nina amini mke wangu ni mchapa kazi, nina amini mke wangu ni mrembo, nina amini mke wangu ananifaa hata kama hizo sifa hana kwa kuwa naamini basi ninavyoamini ndivyo itakuwa na nitakuwa na furaha kuliko kuwaza vinginevyo.
 
asante sana kwa ujumbe murua,
nakupa big up mwanawane. itasaidia wengi nami nikiwepo katika kundi hilo.
be blessed
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom