Elections 2010 Amini usiamini : Utabiri wa mw. Nyerere watimia !! !!!

Zed

JF-Expert Member
Mar 28, 2009
430
249
:nono::nono:
“UTAJIRI unaotokana na wizi wa mali ya umma, na wizi wa fedha za kigeni na unyonyaji na uharamia wa aina mbalimbali, hautupunguzii umaskini wetu, bali unauongeza. Chama chetu hakiwezi kuikubali hali hii, na kikaendelea kuwa CCM, na wala kisitazamie kuwa wananchi wataendelea kukikubali” (Mwalimu Nyerere, Oktoba 1987).

MAFISADI KAZI KWENU WATANZANIA WAMEAMKA NA SASA WANATAKA NCHI YAO. SIKU INAKUJA TUTAWAHUKUMU NA MTAFIA MAGEREZANI MLIKOWEKA WANYONGE MLIOWAIBIA UTAJIRI WAO MKAWALAZIMISHA WAIBE KUKU ILI KUJIKIMU. Mungu ibariki Tanzania tupe nguvu ya kuendelea kupambana bila kuchoka na hawa mafisadi wanaoendelea kutuibia bila huruma !! AMEN

Swali langu kwa Mh. Raisi Kikwete: Je ulipoapa na tena ukashika msahafu na pia Katiba ya nchi, je, uliapa kulinda mali na rasilimali za Tanzania au ni kuziweka chini ya wageni na hasa mafisadi ambao sasa wanaendelea kuitafuna tanzania bila kushibisha matumbo yao ? Naomba utafakari haya na ukiendelea kuiweka Tz chini ya mafisadi, miaka 5 siyo mingi. Watanzania tutakuhukumu siku moja kwenye mahakama zetu au zile za kimataifa !!!!

Tukiunge mkono chama kitakachopambana kwa nguvu zote ili Tanzania iwe ni nyumbani kwa watoto wote wa Tanzania. Naamini kwa watoto wawili wa Mw. Nyerere kugombea nafasi kwenye chama cha Chadema kunaashiria kitu fulani. Jamani Watanzana. We need to learn the sines of our Times. Let's join our forces to liberate our Counrty. No body else from outside will liberate us. Umoja ni nguvu !! Mpaka tupandishe bendera ya matumaini mapya kwa watoto wa Tanzania tutakapo waangusha mafisadi na kupandisha bendera mpya ya Matumaini:israel::israel::israel::israel:

DM
 
Ccm mafisadiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Dr Slaa kaangushwa na mawakala uchwara waliohongwa na CCM!!!
 
Mapambano bado yanaendelea na safari hii yatapamba moto mara dufu mpaka kieleweke. Pamoja na uchakachuaji uliofanywa na mafisadi, mwaka huu majimbo yote muhimu yamekamatwa na wananchi kupitia chama chao cha chadema. Hiyo ni mvua ya rasharasha. Mvua kamili na ya mawe ni 2015
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom